Mwanafunzi wa IFM adhalilishwa na Walinzi wa Ikulu kisa kupiga picha maeneo ya ikulu

Kasinja jr

JF-Expert Member
Aug 4, 2017
1,034
1,792
Imeniuma sana nikiwa natokes Hazina muda wa saa saba mchana nikapita maeneo ya Ikulu kwa mbele mara nyuma yangu alikuwapo mwanafunzi we Chuo cha usimamizi wa fedha, akapiga picha msafara wa mtu mzito aliyekuwa anaelekea kituo cha uwekezaji karibu na Bunge la Tanzania ofisi ndogo za Dar es salaam,

Binti huyo amepigwa ngwala na kurushwa kichura chura na walinzi wa Ikulu wenye sura kama za wanyarwanda na uniform maalum

Amevutwa Nywele kwa kudhalilishwa na raia tuliokuwa tunashuhudia tukiamuliwa kuondoka Mara moja, wakabaki na binti huyo,

Kwa haraka haraka maskini inaonekana alikuwa binti wa mwaka wa kwanza wa kutoka mikoani ambaye hakujua madhara ya jambo alilofanya,

Hapo nimeona wamekosea kumburuta hivo, wangeweza kumwambia afute picha hizo na kumuachia kwa kumuelimisha

Kasinja
 
Ndio umeshauza Ng'ombe zako huko kijijini, ili umlete mwanao asome chuo kikuu dar, chukulia ndio MWANAO huyo kafanyiwa hivyo, akitoka hapo unajikuta inabidi upitishe MCHANGO ili umpeleke hospitali akatibiwe. Hapo hapo ushatiliwa ngumu katika MAFAO YAKO. Uliowachagua wakakuwakilishe BUNGENI ndo hivo tena wanaleta TAARABU kulinda Ugali wao.

Inasikitisha sana, mungu amsaidie

Mara Paap, binti wa watu ndio inatokea anarudisha namba kwa "Sir. God". Kesho magazeti dunia nzima lazima yaandike hio habari, vyuo vikuu mara utaskia wanafunzi wana andamana na kugoma, haki za binaadamu nao hawatataka wapitwe kutoa tamko, vyama vya upinzani nao ndio balaa.

Ni afadhali hata angepelekwa polisi kwa kosa hilo, kuliko kuchukua SHERIA MKONONI.

Au labda sheria inawapa ruhusa hio ya kupiga raia hao jamaa???? Japo sijawahi kuona sheria ya hivyo maishani.
 
Imeniuma sana nikiwa natokes Hazina muda wa saa saba mchana nikapita maeneo ya Ikulu kwa mbele mara nyuma yangu alikuwapo mwanafunzi we Chuo cha usimamizi wa fedha, akapiga picha msafara wa mtu mzito aliyekuwa anaelekea kituo cha uwekezaji karibu na Bunge la Tanzania ofisi ndogo za Dar es salaam,

Binti huyo amepigwa ngwala na kurushwa kichura chura na walinzi wa Ikulu wenye sura kama za wanyarwanda na uniform maalum

Amevutwa Nywele kwa kudhalilishwa na raia tuliokuwa tunashuhudia tukiamuliwa kuondoka Mara moja, wakabaki na binti huyo,

Kwa haraka haraka maskini inaonekana alikuwa binti wa mwaka wa kwanza wa kutoka mikoani ambaye hakujua madhara ya jambo alilofanya,

Hapo nimeona wamekosea kumburuta hivo, wangeweza kumwambia afute picha hizo na kumuachia kwa kumuelimisha

Kasinja
Acheni huu ujinga Yani huyo binti sio mtanzania Wala sio raia. Nakilichomkuta ni adhabu yake. Hivi kweli hajuwi pale watu hawapigi picha Acheni kuweka mambo yakipumbavu mkijuwa sheria hata mm nimesoma ifm hivyo wacha atolewe ushamba nisawa nakuingia eneo la jeshi pasipokujuwa lazima yakukute yakukuta ila Usije simulia maana ni haki yako. Nenda pale st peter upige picha ile ndege kwenye mzitu alafu ndipo uje kusema nn kitakupata
 
Back
Top Bottom