Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Kenya auawa kwa kupigwa shoka kichwani na mpenzi wake kisa kumuambukiza VVU

moyafricatz

JF-Expert Member
Nov 27, 2015
2,900
4,865
Binti aliyekuwa anasoma chuo kikuu cha MOI ameuawa kwa kukatwa na soka na kijana aliyekuwa mpenzi wake

Tukio hili la kutisha limetokea leo tarehe 09 Aprili 2019 nchini Kenya ambapo Mwanafunzi huyo wa Chuo Kikuu cha Moi nchini Kenya(pichani) alikuwa njiani bila kujua alifuatwa na gari kwa nyuma pasipo yeye kujua na mpenzi wake (huyo kijana anayevuja damu) ghafla kijana huyo akiwa anaendesha gari hiyo alisimamisha gari na kushuka akiwa ameshika shoka na kumpasua nalo kichwani kwa nyuma mara mbili msichana huyo na kumsababishia kifo hapo hapo.

Taarifa zisizo rasmi zinasema kuwa kijana huyo alifanya tukio hilo baada ya kugundua binti huyo alikuwa na virusi vya Ukimwi ila hakumwambia kwahiyo alimuambukiza kwa makusudi.

Wananchi wenye hasira kali walimvamia kijana huyo na kumpa kipigo kikali kabla ya Polisi kutokea na kumuokoa kisha kuondoka nae kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

Taarifa hii ndio inayotikisa mitandao ya kijamii nchini Kenya Citizen TV Kenya wameripoti, INASIKITISHA SANA

R. I. P mrembo
IMG-20190412-WA0011.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuweni na heshima na ustaarabu basi. Sio jambo la busara kuanika picha ya marehemu hivi kama wanigeria. Ungeeka picha yake nyingine, akiwa hai na picha ya huyo mhuni aliyefanya kitendo hicho pia. Cc. Moderator.
 
Ila yataka moyo sana,Sikubaliani na kuukatisha uhai wa mtu,Ila sio siri hili Janga mtu akakubebesha makusudi unaweza ukamkata koromero kwa mikonom
 
Ila yataka moyo sana,Sikubaliani na kuukatisha uhai wa mtu,Ila sio siri hili Janga mtu akakubebesha makusudi unaweza ukamkata koromero kwa mikonom

Ahaaa haaa haaa
Usijipe pressure ndg. Ukimwi si tisho tena. Miaka ya 90's ndiyo ilikuwa shida. Saa hii mwenye ukimwi na asiye nao wote draw ngoma.
 
Back
Top Bottom