Mwanafunzi wa chuo kikuu Dodoma afariki akiwa usingizini

Petro Oswald

JF-Expert Member
Aug 17, 2015
2,379
1,879
Taarifa zilizopo ni kwamba, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza chuo kikuu cha Dodoma, kitivo cha Elimu anayefahamika kwa jina la Seni aliekua akisoma bachelor of education in policy planning management (BED PPM) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa usingizini.

Taarifa zinaongeza kwamba, kabla ya umauti marehemu alirudi chumbani kwake akitokea darasani alikokuwa akijisomea, ambapo alipopanda kitandani na kulala, hakuweza kuamka tena baada ya juhudi za kumuhamsha asubuhi ya leo kugonga mwamba, hali iliyopelekea wasi wasi kwa wanaroom wenzake hivyo wakatoa taarifa kwa wanafunzi wengine na uongozi wa chuo juu ya tukio hilo.

Mpaka sasa haijajulikana ni nini hasa kimepelekea kifo chake, ingawa tayari madaktari wamethibitisha kifo hicho, na sasa mwili wa marehemu upo katika hospitali ya General kwa uchunguzi zaidi chini ya uangalizi la jeshi la polisi Dodoma.

IMG-20160709-WA0017.jpg

R.I.P
 
polen sana wanafunzi kwa kumpoteza mwenzenu , poleni wafiwa kwenye hichi kipindi kigumu sana.
 
Taarifa zilizopo ni kwamba, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza chuo kikuu cha Dodoma, kitivo cha Elimu anayefahamika kwa jina la Seni aliekua akisoma bachelor of education in policy planning management (BED PPM) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa usingizini.

Taarifa zinaongeza kwamba, kabla ya umauti marehemu alirudi chumbani kwake akitokea darasani alikokuwa akijisomea, ambapo alipopanda kitandani na kulala, hakuweza kuamka tena baada ya juhudi za kumuhamsha asubuhi ya leo kugonga mwamba, hali iliyopelekea wasi wasi kwa wanaroom wenzake hivyo wakatoa taarifa kwa wanafunzi wengine na uongozi wa chuo juu ya tukio hilo.

Mpaka sasa haijajulikana ni nini hasa kimepelekea kifo chake, ingawa tayari madaktari wamethibitisha kifo hicho, na sasa mwili wa marehemu upo katika hospitali ya General kwa uchunguzi zaidi chini ya uangalizi la jeshi la polisi Dodoma.

View attachment 364536

R.I.P
R.I.P....wote mauti yanatusubiri.
 
Back
Top Bottom