Mwanafunzi wa Chuo afariki katika mazingira tata!

Mwanafunzi wa Chuo afariki katika mazingira tata!

TANMO

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2008
Posts
12,046
Reaction score
12,542
IMG20141220WA0003.jpg

Binti mbichi aliyejulikana kwa jina la Neema Malimbwi (pichani) ambaye alikuwa mwanafunzi wa Chuo cha Kodi Tanzania (ITA) ambacho kipo chini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kilichopo Mikocheni jijini Dar amefariki dunia kwa madai ya kulishwa sumu kwenye kinywaji.

Marehemu Neema alikuwa binti wa profesa wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Morogoro (Sua), Rogers Malimbwi.

Tukio hilo la kusikitisha linatajwa kutokea usiku wa Alhamisi, Desemba 18, mwaka huu wakati Neema anarudi hosteli maeneo ya Kijitonyama, Dar ambapo alikuwa akiishi.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, siku ya tukio, Neema alikuwa na marafiki zake wavulana kwa wasichana kwenye onesho la muziki wa B Band inayomilikiwa na Banana Zorro ambapo akiwa huko saa 7 usiku aliendelea kuchati na marafiki zake waliokuwa hosteli akitumia ukurasa wake wa Facebook akiwaambia kuwa alikuwa ‘kiwanja' akiponda raha.

Habari zinadai kuwa, marehemu Neema usiku huo alikuwa akihama maeneo mbalimbali akiwa na vijana ambao baadhi ya marafiki zake wanadai huenda walihusika na kumtilia sumu kwenye bia alizokuwa akinywa.

mane.jpg

Habari zaidi zinasema kuwa, Neema akiwa na wenzake wakirudi hosteli, njiani alianza kulalamikia kutojisikia vizuri.

"Alikuwa njiani na wenzake wakirudi kulala, akaanza kulalamika kwamba hajisikii sawasawa, ikabidi wenzake wamkimbize Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu wa Kinondoni, Palestina, Sinza, Dar ambako waliambiwa kuwa kutokana na hali yake kuwa mbaya wampeleke kwanza Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini' jijini Dar ili kupata hati ya matibabu (PF3)," kilisema chanzo kimoja.Chanzo hicho kikaendelea kudai kwamba, walipofika Mabatini waliambiwa waende Kituo cha Polisi Oysterbay.

Ikazidi kudaiwa kuwa, Polisi Oysterbay walitoa msaada kwa haraka ambapo sasa ikabidi Neema akimbizwe Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu Kinondoni, Mwananyamala ambako alifariki dunia.

Mwili wa Neema ulihifadhiwa kwenye mochwari ya Mwananyamala kabla ya kusafirishwa juzi kwenda Morogoro kwa mazishi yaliyofanyika jana.

Kumbukumbu zilizopo kwenye makabrasha ya gazeti hili zinaonesha kuwa, Juni Mosi, mwaka jana, mama mzazi wa Neema, Elizabeth Malimbwi alifariki dunia kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar na mwili wake kwenda kuzikwa Morogoro.

Tangu kifo cha mama yake, baadhi ya madenti wenzake wanasema, Neema amekuwa akiishi maisha ya mawazo sana na muda mwingi alikuwa akiutumia kunywa pombe kiasi kwamba, darasani ilikuwa mara chache sana kuhudhuria.

Akizungumza na gazeti hili juzi, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Camillius Wambura alikiri kuwa na taarifa hizo."Ni kweli taarifa za kifo cha mwanafunzi huyo ninazo, mpaka sasa jeshi la polisi linasubiri ripoti kamili ya uchunguzi wa madaktari kuhusiana na kifo chake," alisema Kamanda Wambura.


Chanzo: GlobalPublishers


---Gone too soon, Poleni wafiwa....

Mapendo,
TANMO.
 
Mungu ailaze roho ya huyu Binti mahali alipojichagulia yeye mwenyewe enzi za Uhai wake
 
Daah kifo bana alikuwa katoka kunywa pombe poleni waf iwa lakini wazazi simamieni hapa enyi wazazi waleeni watoto wenu katika njia ipasayo nao hawataiacha mpaka uzeeni.

walee tu ila kifo akichagui
 
walee tu ila kifo akichagui

Ms neddy sawa hakichagui lakini Mungu hapendi watu wake waangamie sio vifo vyoote Mungu ana husika shetani nae anataka wafuasi wake wawe wengi na ndio maana kama wewe ni mkristo Biblia imeandikwa maisha ya binaadamu ya kuishi ni miaka 70 zaidi ya hapo ni shida na mateso meengi , na dhambi ndio inayoleta mauti sote tutakufa sikatai huyo mtoto bado ni mdogo sana na ukijaribu kuchunguza miaka ya nyuma ulikuwa huwezi sikia mtoto au kijana amekufa ni nadra sana lakini kutokana na maasi kuongezeka vifo siku hizi vimekuwa vya kawaida badala ya wajukuu kumzika bibi au babu wezee ndio wamegeuka yatima wanazika watoto, wajukuu na vitukuu.
 
Ms neddy sawa hakichagui lakini Mungu hapendi watu wake waangamie sio vifo vyoote Mungu ana husika shetani nae anataka wafuasi wake wawe wengi na ndio maana kama wewe ni mkristo Biblia imeandikwa maisha ya binaadamu ya kuishi ni miaka 70 zaidi ya hapo ni shida na mateso meengi , na dhambi ndio inayoleta mauti sote tutakufa sikatai huyo mtoto bado ni mdogo sana na ukijaribu kuchunguza miaka ya nyuma ulikuwa huwezi sikia mtoto au kijana amekufa ni nadra sana lakini kutokana na maasi kuongezeka vifo siku hizi vimekuwa vya kawaida badala ya wajukuu kumzika bibi au babu wezee ndio wamegeuka yatima wanazika watoto, wajukuu na vitukuu.

ni kuomba rehema tu
 
Isingekuwa mlolongo wa PF3 labda wangeweza kumuokoa!
Kwa nini wasi control hali ya mgonjwa kwanza?

kweli mkuu,Ifike wakat serikal ilione hili,kwanini kusiwekwe utaratibu kila hospital ya wilaya kukawa na ofisi ya kutoa hizi PF 3??nakumbuka nshapata shida sana na majeruh wa ajal kwa kuzungushwa nenda kituo hik,ukifika nenda kule,,kuna haja ya kulitazama hili vifo vingi vnatokea kwa kukosa huduma kwa wakati!!!!
 
Daah kifo bana alikuwa katoka kunywa pombe poleni waf iwa lakini wazazi simamieni hapa enyi wazazi waleeni watoto wenu katika njia ipasayo nao hawataiacha mpaka uzeeni.
Kwa hili unawaonea wazazi hawawezi kuwa na vijana wao muda woote
 
Watu wa psychology inabidi waanze kuajiriwa vyuoni na shule za sekondari, kwani chanzo chawezekana kikawa ni msongo wa mawazo kilichompelekea kujihusisha na utumiaji wa pombe kwa wingi. Swala la msongo wa mawazo halina tiba zaidi ya counselling au ushauri nasaha. Lala pema peponi dada Neema.
 
Isingekuwa mlolongo wa PF3 labda wangeweza kumuokoa!
Kwa nini wasi control hali ya mgonjwa kwanza?

Mkuu yaani hizi pf3 ni shida!! Kuna kipindi miaka ya nyuma jamaa aliumia karibia na mwenge (dsm)nikamchukua kumuwahisha
Hospitali nilijuta....nilipita kituo cha mwenge wakaniambia niende kijitonyama wao wameishiwa, kijitonyama nao wakaniambia niende kwa ali maua, kule nako wakaniambia niende osterbay, osterbay ilibidi kumsubiri aliyekuwa na form kwa zaidi ya nusu saa!! Imagine jamaa damu ilikuwa inamtirirka muda wote huo!!

a
 
hapo maswala ya pf3 jamani mgonjwa kama anaumwa sana atibiwe kwanza jamani hii nchi hi
lakini pia kuna mtu aliwahi kusema kama una kiasi kikubwa cha pombe ukienda kutibiwa mafactar wanashindwa kukupa ,saada maana kama kidonge ukipewa kinaeza kikakumaliza

by the way she is cute


R.I.P ney...pole baba neema
 
Back
Top Bottom