Mwanafunzi UDOM akamatwa akiwa na misokoto 826 ya bangi

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linawashikilia watu wawili kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi akiwamo mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Nelson Matee (24) ambaye ni mwanafunzi wa kozi ya uuguzi mwaka wa nne.

4b90fcd6d69faad529c322673a3c301a.jpg


Akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake, kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema kuwa mwanafunzi huyo alikamatwa Mei 9 mwaka huu kufuatia msako mkali uliofanywa na jeshi hilo chuoni hapo ambapo mtuhumiwa alikutwa na jumla ya misokoto 826 ya bangi yenye uzito wa kilo 2.8 akiwa ameiweka kwenye mifuko ya nailoni chumbani kwake.

Mambosasa amesema kuwa mtuhumiwa alipohojiwa alisema kuwa amekuwa akifanya biashara hiyo ya kuuza bangi kwa kipindi cha miaka minne tangu alipojiunga na chuo hicho na kwamba alikuwa akiwauzia wanafunzi wenzake.
 
Mwanafunzi wa mwaka wa nne Chuo Kikuu cha Dodoma kozi ya Uuguzi Nelson Gaspal Matee amekamatwa na misokoto 800 ya bangi, amekuwa akiwauzia wanafunzi wenzake hapo chuoni.
Chanzo ITV Habari.
 
Wanafunzi wa udom punguzeni uhuni wa kutukia bangi. Habar zinaeleza kua mwanafunzi wa UDOM Akamatwa na mihadarati ya bangi kg 2na nusu.
Aidha kamanda polisi wa mkoa huo ameagiza kuanza kufanya msako kwa wanafunzi wenye matumizi ya bangi. Jiangalieni Sana nyie wanafunzi
 
Leo mwanafunzi wa UDOM anayesoma fani ya udaktari mwaka wa 4, amekamatwa na polisi na zaidi ya misokoto 800 ya bange na amedai kwamba 100% ya wateja wake ni wanafunzi wenzake. Jamani tunaelekea wapi mbona taifa letu linaangamia kwa kukosa maarifa?
 
Mwanafunzi wa mwaka wa 4 fani ya uuguzi amekamatwa na misokoto 800 ya bangi.Amekiri na kudai wateja wake ni wanafunzi wenzake wa hapo Udom.RPC Mambosasa amesema zoezi la kuwakamata watumiaji linaendelea chuoni hapo.Source ITV Habari
 
Mwanafunzi wa mwaka wa nne Chuo Kikuu cha Dodoma kozi ya Uuguzi Nelson Gaspal Matee amekamatwa na misokoto 800 ya bangi, amekuwa akiwauzia wanafunzi wenzake hapo chuoni.
Chanzo ITV Habari.
Ha ha ha huyu mwanafunzi ni hewa
 
Ukipiga hesabu kwa msokoto mmoja labda anauza kwa sh 500 ukizidisha kwa hyo misokoto 800 jumla analamba kama laki nne na pengine ndan ya siku tatu mzigo umeisha fikiria kwa mwezi sijui atakuwa anakula shingapi...
Ila Mshika mawili moja.... dogo angekomaa na shule tu maana mpka hapo kashajiharibia future yake
 
Haya yote yamesababishwa na serikali ya CCM kuwanyima wanafunzi mikopo hadi wanafikia hatua ya kutafuta mbinu mbadala za kujikimu. Serikali ilaaniwe kwa ufedhuli huu inaowafanyia watoto wa wakulima.
 
Back
Top Bottom