Sexer
JF-Expert Member
- Oct 22, 2014
- 8,368
- 8,072
Kwa masikitiko makubwa tukio tajwa hapo chini limetokea Chuo cha SAUT mwanza ambapo mwanafunzi wa jinsia ya kiume ,alienda kumtembelea mpenzi wake chuoni SAUT bweni la RUGAMBWA,baada ya kufika katika kuangalia simu ya mpenzi wake alikuta sms ya mwanaume mwingine ambapo,alichukia na kuamua kuondoka na simu ya mpenzi wake.
Alichokifanya binti huyo aliita MWIZI, watu walikuja na kupiga bila kuuliza.
Alichokifanya binti huyo aliita MWIZI, watu walikuja na kupiga bila kuuliza.
View attachment 325893Ukweli ni kwamba huyo jamaa na huyo demu ni wapenzi wa muda mrefu na pia jamaa sio mwanafunzi ni raia wa kawaida anayehusika na mambo hasa ya modeling na amekuwa akiandaa event mbalimbali kama mtakuwa na kumbukumbu vizuri kuna kipindi kulitokeaga shindano la MISS ALBINISM lililofanyika Mwanza huyu jamaa alikuwa miongoni mwa wahusika wa hilo shindano,na siku tatu zilizopita huyu jamaa alitoka kumzika baba yake mzazi.
Kilichotokea hapo ni baada ya jamaa kwenda hosteli za wanawake ambazo zipo ndani ya chuo ambapo ndipo alipokuwa akiishi huyo demu wake, katika kukagua simu ndipo akakuta sms za utata, ukatokea ugomvi katika mabishano demu akasema atamwita mwizi kama utani kweli demu akaita mwizi.
Jamaa kwa kuogopa na sababu hakuwa na kitambulisho ndipo akatoka mbio, hapo ndipo alipoharibu wananzengo na wanachuo bila kujali wakaanza kupiga na mpaka wanafika polisi alikuwa kapigwa sana, alipelekwa kituoni kutoa maelezo. Baada ya hapo ndipo tukapata taarifa kafariki na hiyo ni sababu ya kipigo.
Kinachofanywa na uongozi wa chuo ni kutaka kuonesha huyo binti hana makosa ili kuondoa uhasama na wananzengo ila ukweli utabaki kuwa huyo jamaa na mwanamke walikuwa wapenzi.