Mwanafunzi NIT, Julius Warioba ahukumiwa mwaka mmoja jela kwa kuchapisha maudhui mtandaoni bila leseni

Mwanafunzi NIT, Julius Warioba ahukumiwa mwaka mmoja jela kwa kuchapisha maudhui mtandaoni bila leseni

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,410
Reaction score
4,988
Mwanafunzi wa mwaka wa pili, Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, Julius Warioba (23), amehukumiwa kulipa faini ya Sh5m au kwenda jela mwaka mmoja, baada ya kukiri kuchapisha maudhui mtandaoni bila leseni kutoka TCRA.

***
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam nchini Tanzania, imemhukumu mwanafunzi wa mwaka wa pili, Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Julius Warioba (23) kulipa faini ya Sh5 milioni au kwenda jela mwaka mmoja.

Ni baada ya kukiri shtaka la kuchapisha maudhui katika Mtandao bila kuwa na leseni kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Warioba ambaye ni mshereheshaji (MC) anadaiwa kuchapisha maudhui kupitia Televisheni ya mtandaoni ( Tv online) inayojulikana kwa jina Mc Warioba, bila kuwa na kibali kutoka TCRA wakati wakijua kuwa ni kinyume cha sheria ya Mtandao.

Mbali na faini, Mahakama hiyo, imetaifisha kompyuta aina ya Apple na simu ya mkononi aina ya Iphone ambavyo vilitumika katika kuchapisha maudhui hayo.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo amefanikiwa kulipa faini na hivyo kukwepa kifungo.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatatu Agosti 26, 2019 Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Janeth Mtega baada ya mshtakiwa kutiwa hatiani.

Hakimu Mtega amesema mshtakiwa ametiwa hatiani kama alivyoshtakiwa, hivyo atatakiwa kulipa faini hiyo au kutumikia kifungo.

" Mahakama imekutia hatiani baada ya kukiri kosa lako, hivyo utalipa faini ya Sh5 milioni na ukishindwa kulipa faini hii, utatumikia kifungo cha miezi 12 jela," amesema Hakimu Mtega.

Hakimu Mtega amesema mbali na mshtakiwa huyo kulipa faini, mahakama imeamuru kompyuta na simu moja ya mkononi ya mshtakiwa huyo itaifishwe.

Awali, wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon akisaidiana na Batilda Mushi amedai kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa shauri hilo umekamilika na wako tayari kumsomea mshtakiwa huyo maelezo ya awali.

Simon baada ya kueleza hayo, alimsomea Warioba shtaka lake.

Mc Warioba, baada ya kusomewa shtaka lake, alikiri na ndipo mahakama hiyo ilipomtia hatiani mshtakiwa huyo na kumhukumu kulipa faini hiyo au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela.

Hata hivyo, kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Simon aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali dhidi mshtakiwa huyo, ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia ya kuchapisha maudhui katika Mtandao bila kuwa na leseni kutoka TCRA.

Mc Warioba alifikishwa Kisutu kwa mara ya kwanza, Mei 7, 2019, kujibu shtaka hilo katika kesi ya jinai namba 116/2019.

Katika kesi ya msingi, Warioba anakabiliwa na shtaka moja la kuchapisha maudhui katika Mtandao bila kuwa na leseni kutoka TCRA.

Tukio hilo anadaiwa kutenda kosa hilo, kati ya Januari 2016 na Aprili 30, 2019 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

Inadaiwa katika kipindi hicho, Warioba alichapisha maudhui kupitia Televisheni ya mtandaoni (Tv online) inayojulikana kwa jina Mc Warioba, bila kuwa na kibali kutoka TCRA wakati wakijua kuwa ni kinyume cha sheria ya Mtandao

Chanzo: Mwananchi
 
contents.
Nieleweshe zaidi please (ingawa huwa tunapishana sana humu)
Soma hii extract from google na nidadavulie
The objective the writing is the main difference between content writing and journalism.

What's the difference between content writing and journalism?

Apart from that the style and tone of writing is also different.

Goal of Journalistic Writing

  • The goal is to inform and educate the public about latest events.
  • Some journalistic writing are also aimed to persuade people to form particular opinions through biased reporting. This is true especially true when it comes to Indian media.
Goal of Content Writing

Content writing is usually done as part of content marketing and search marketing (seo).

sasa hapo unaposema content huoni umeniacha njia panda?
 
Napiga picha mie ndio mzazi wake! Jamani watoto nyie jifunzeni kusoma alama za nyakati. Kila utakalo kulifanya fikiria mara mbili. Ona sasa, mie mzazi ndie ninayeumia.... kwa nini lakini hamsikii wala hamjifunzi kwa wengine?? sheeenzyy taipu... Penye uharo unatia maji!!!! utazoaje sasa!
 
acha woga,
 
Nieleweshe zaidi please (ingawa huwa tunapishana sana humu)
Soma hii extract from google na nidadavulie
The objective the writing is the main difference between content writing and journalism.

What's the difference between content writing and journalism?

Apart from that the style and tone of writing is also different.

Goal of Journalistic Writing

  • The goal is to inform and educate the public about latest events.
  • Some journalistic writing are also aimed to persuade people to form particular opinions through biased reporting. This is true especially true when it comes to Indian media.
Goal of Content Writing

Content writing is usually done as part of content marketing and search marketing (seo).

sasa hapo unaposema content huoni umeniacha njia panda?
Kwa Kiingereza maudhui ni content(s). Hilo ndio nijualo. Hayo mengine ni mambo ya kimtazamo tu.
 
Back
Top Bottom