Mwanafunzi kutoka Nigeria apigwa India

Mwanafunzi kutoka Nigeria apigwa India

Babu wa Kambo

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2016
Posts
559
Reaction score
808
Wizara ya mambo ya nje nchini India inasema imeitisha taarifa kutoka kwa maafisa wa jiji la Hyderabad baada ya mwanafunzi kutoka Nigeria kushambuliwa Jumatano.

Mwanafunzi huyo alitibiwa hospitalini na baadaye kuruhusiwa kuondoka.

Wiki iiyopita, kijana kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo alipigwa na kuuawa mjini Delhi.

Kisa hicho kiliwafanya mabalozi wa nchi za Afrika kutishia kususia sherehe za kuadhimisha siku ya Afrika nchini India ingawa baadaye walibadilisha msimamo wao.

Baada ya kuripotiwa kwa kisa hicho, maduka ya raia wa India katika mji mkuu wa Dr Congo, Kinshasa yalivamiwa na kuporwa.

CHANZO: BBC Swahili
 
Back
Top Bottom