Mwanafunzi Kidato cha kwanza abakwa darasani

Mwanafunzi Kidato cha kwanza abakwa darasani

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,247
Reaction score
25,191
Carreen-Yunus--November21-2014.jpg

Mkuu wa wilaya ya Sengerema, Carren Yunus

Mwanafunzi wa kidato cha kwanza A katika shule ya sekondari Ntunduru wilayani Sengerema mkoani Mwanza (jina limehifadhiwa, 14), amejeruhiwa vibaya sehemu za siri na shingoni kutokana na kukabwa shingoni wakati akibakwa ndani ya chumba cha darasa la shule hiyo mchana.

Tukio hilo lilitokea Novemba 15, mwaka huu mchana huku baadhi ya walimu wakidaiwa kuwapo shuleni baada ya mwanafunzi huyo kuitwa na mhitimu wa kidato cha nne ambaye anatuhumiwa kutenda kosa hilo.

Mwanafunzi huyo baada ya kuingia katika darasa hilo, alikutana na wanafunzi wawili wa kidato cha nne waliomkaba shingo na kumziba mdomo kisha kumvua nguo na kuanza kumtendea ukatili huo.

Mkuu wa wilaya ya Sengerema, Carren Yunus, alisema watuhumiwa hao lazima wapatikane na kuchukuliwa hatua za kisheria.

"Pamoja kuwasaka watuhumiwa pia lazima ufanyike uchunguzi wa kina juu ya usalama wa wanafunzi wa kike katika shule hii binafsi mchanganyiko ya bweni," alisema Yunus.

Makamu mkuu wa shule hiyo, Bahati Charles, alithibitisha kutokea kwa tukio na tayari wanafanyia uchunguzi pamoja na vyombo vya dola.
"Ni kweli tukio hilo limetokea, ni tabia tu ya vijana wa leo kukosa maadili," alisema Charles.

Polisi wilayani Sengerema imethibitisha kuwapo tukio hilo lenye jalada Seng/RB/2949/2014 ya Novemba 15, na kuwataja watuhumiwa ambao hata hivyo majina yao yanahifadhiwa.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Valentino Mlolowa, alithibitisha kutokea kwa tukio na hilo na kusema msako wa wahusika unaendelea.

Chanzo:Nipashe
 
Wakamatwe kuanzia mwalimu mkuu na waalimu wake wote; Inakuwaje uhuni kama huo kufanyika kwenye madarasa ya shule, na mwalimu anajibu kirahisi rahisi tu.

China hadi waziri wa elimu angewajibika.
 
Wakamatwe kuanzia mwalimu mkuu na waalimu wake wote;
Inakuwaje uhuni kama huo kufanyika kwenye madarasa ya shule, na mwalimu anajibu kirahisi rahisi tu.

China hadi waziri wa elimu angewajibika.

Aiseee umenikuna hii yote inatokana na serikali legelege kila kitu kinakuwa legelege.
 
Wakamatwe kuanzia mwalimu mkuu na waalimu wake wote; Inakuwaje uhuni kama huo kufanyika kwenye madarasa ya shule, na mwalimu anajibu kirahisi rahisi tu.

China hadi waziri wa elimu angewajibika.
Siku zote nasema hizi shule za kata ni mkusanyiko wa hard core criminal standard seven failures! BRN -wote wahuni aambao walikuwa wavuta bangi hawasomi wanasombwa kwa BRN kwenda sekondari!
 
Kwakweli ni tukio baya na ambalo lazima wahusika wakamatwe na waadhibiwe vikali, mama mzazi wa binti amelalamika waalimu wa hiyo shule hawakumpa ushirikiano wowote nao pia wawajibishwe, tunaomba katika hili rushwa ya aina yoyote isipewe nafasi cause itamnyima huyo binti haki yake, uchunguzi wa afya yake pia uzingatiwe..!!
 
Taratibu, kwani hujasikia shule za seminari wanalawitiana?

Ntunduru sio shule ya serikali, ni ya private, if am not mistaken mmiliki wake anaitwa mchele, shule inawahuni kibao toka enzi hizo, sijui kwa sasa kama hali yenyewe ndo hiyo.
 
Wakamatwe kuanzia mwalimu mkuu na waalimu wake wote; Inakuwaje uhuni kama huo kufanyika kwenye madarasa ya shule, na mwalimu anajibu kirahisi rahisi tu.

China hadi waziri wa elimu angewajibika.

kwani mwl ndiye aliyebaka? wewe mzazi litoto limekushinda huko halafu unampelekea mwl akalifundishe . mijitu inavuta bangi tangu nyumbani na mzazi unamwona halafu humkemei.
 
!!BRN hadi mateja wanamaliza form four...hata kama hawajui kutofautisha kati ya darasa,kichaka,chumba au choo!!ukikataa kwao maana yake umekubali!Pole mtoto uliebakwa!!Ajabu darasa lilijitenga porini au?
 
Kwa kuwa miaka haigandi omba sana lisitokee kwako.
kwani mwl ndiye aliyebaka? wewe mzazi litoto limekushinda huko halafu unampelekea mwl akalifundishe . mijitu inavuta bangi tangu nyumbani na mzazi unamwona halafu humkemei.
 
Kwakweli ni tukio baya na ambalo lazima wahusika wakamatwe na waadhibiwe vikali, mama mzazi wa binti amelalamika waalimu wa hiyo shule hawakumpa ushirikiano wowote nao pia wawajibishwe, tunaomba katika hili rushwa ya aina yoyote isipewe nafasi cause itamnyima huyo binti haki yake, uchunguzi wa afya yake pia uzingatiwe..!!
hata huyu mkuu wa shule kajibu fedhuli sana nafikiri huo utovu wa nidhamu anaousema wakawaida umgeukie yeye siku moja.....
 
Wakamatwe kuanzia mwalimu mkuu na waalimu wake wote; Inakuwaje uhuni kama huo kufanyika kwenye madarasa ya shule, na mwalimu anajibu kirahisi rahisi tu.

China hadi waziri wa elimu angewajibika.

una mawazo ya kitoto kweli wewe pole sana.
 
Siku zote nasema hizi shule za kata ni mkusanyiko wa hard core criminal standard seven failures! BRN -wote wahuni aambao walikuwa wavuta bangi hawasomi wanasombwa kwa BRN kwenda sekondari!

Mkuu hiyo shule sio ya kata ni private flani hivi tena ipo tu mjini.
 
Wanafunz siku hz hawachapwi wala kuonywa unategemea nn?, wazaz huwa watoto wao wakiguswa tu wanawapanda walimu vchwan na hata kuwashushia kichapo. Kesi za mimba za wanafunz zkiripotiwa polisi wanazmaliza kicool akafu teacher anachekwa na kuwekewa mabifu. walimu wenyewe ni masela a.k.a .com haha kaz kwelikweli.
 
Ni vigumu kuamini ila ndio imeshatokea kwa kweli inasikitisha sana
 
Wakamatwe kuanzia mwalimu mkuu na waalimu wake wote; Inakuwaje uhuni kama huo kufanyika kwenye madarasa ya shule, na mwalimu anajibu kirahisi rahisi tu.

China hadi waziri wa elimu angewajibika.

Hili ni Jambo ambalo si lakuungwa mkono ni Jambo la kulaani,lakini hoja yako, inawalakini hicho unachosema hatachina kisingetokea, Tangu lini waziri wa Elimu akawa Colokoloni wa wahuni na makahaba hio siokazi yake, mijitu imepagawa na mashetani ya zinaa hivi kilakitu kuwajibika sioni mantiki hapo.
 
We Pumbavu Sana, Unataka Mwalimu Awemo Darasani Muda Wote? Asiende Kula? We Ukiingia Ofisini Huwa Hutoki Kwenda Kula Au Kunya? Acha Kukoment Ujinga.

Ukweli ni kwamba system nzima imepwaya kwa sasa,waalimu hata wasilaumiwe, kwa sababu waalimu wanapotimiza wajibu wao wa kuwaadabisha wanafunzi kwa kywaadhibu Kuna vidudu vinaitwa HAKI ZA BINADAMU,

hawataki kusikia watoto wanachapwa wala kuwaadhibu kwa namna yoyote,wanadai TUWASHAURI TU, kwa ushahidi Kuna mwalimu anaitwa Willa wa shule ya sekondari Mgulasi iliyopo manispaa ya Morogoro, alimuadhibu mwanafunzi kwa utovu mkubwa wa nidhamu,

tena fimbo nne tu, mzazi wake alikuja juu na kumfungulia Mwl mashtaka,aliwekwa lock up na kunyanyaswa nfano wa kibaka, kwa mazingira hayo waalimu tunajivua jukumu la kusimamia nidhamu,tutafundisha tu,maswala ya nidhamu yafanywe na wazazi wao huko,kwani hii ni dharau kubwa na kudhalilisha taaluma!!!
 
Back
Top Bottom