Mwanafunzi ajifungua mapacha watatu

M-bongotz

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,734
405
Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Mkata iliyopo kwenye mji mdogo wa Mkata Wilayani Handeni, Habiba Abdallah, amejifungua watoto watatu kwa kufanyiwa upasuaji.

Habiba alijifungua watoto hao katika Hospitali ya Wilaya ya Handeni iliyopo katika Mamlaka ya Mji wa Chanika.

Habiba alifanyiwa upasuaji huo akiwa na mimba ya miezi saba na alipata ujauzito huo Mei mwaka jana kwa mtu aliyedai kuwa ni mfanyabiashara ya machungwa kabla ya kumtoroka.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwao katika kijiji cha Kwabaya kilichopo nje kidogo ya mji wa Chanika, Habiba, alisema kuwa mwanaume huyo alimkimbia tangu alipokuwa na ujauzito wa miezi miwili, baada ya kupata taarifa ya kuwa ana mimba.

Alisema kuwa alirubuniwa na mwanaume huyo aliyekuwa akinunua machungwa katika mashamba mbalimbali ya michungwa yaliyopo katika kata za Mazingara na Mkata na kuyapeleka jijini Dar es Salaam.

Mimi huyo aliyenipa ujauzito sijui kwao ni wapi, tulionana mara ya mwisho tangu nikiwa na ujauzito wa miezi miwili. Nilipomueleza mabadiliko ya hali yangu kuwa na mimba akanikimbia na hadi sasa sijui alipo ila nahisi yuko Dar es Salaam, alisema na kuongeza:

Najutia kitendo kile kilichonisababishia kukatiza masomo yangu, natamani sana kuendelea na masomo yangu lakini sasa nimekwama. Nina hali ngumu ya kuwalea watoto hawa yaani huu ni usumbufu mkubwa ambao sikutarajia. Natoa wito kwa mabinti wenzangu hasa wanafunzi kuwaepuka wanaume walaghai, badala yake wazidishe msimamo katika kupenda masomo.

Hata hivyo, Habiba alisema kuwa anatarajia kuendelea na masomo yake mwakani, baada ya watoto wake kufikisha umri wa mwaka mmoja na kuongeza kuwa atamuachia mama yake awalee wajukuu zake ili aweze kusoma.

Mama wa binti huyo, Zaina Saidi, alisema anaiomba Serikali na mashirika pamoja na watu binafsi kumsaidia kwa hali na mali kulea watoto hao kutokana na kukosa uwezo.

Alisema baba wa binti yake alifariki dunia Desemba mwaka jana.

CHANZO: NIPASHE

My Take:
Matukio ya aina hii ni mengi sana katika jamii yetu,hizi tabia za kifataki tuacheni jamani na huku kukwepa majukumu ndio kulikonikwaza zaidi huyu bwana inabidi atafutwe na kuchukuliwa hatua stahili.[/COLOR]
 
Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Mkata iliyopo kwenye mji mdogo wa Mkata Wilayani Handeni, Habiba Abdallah, amejifungua watoto watatu kwa kufanyiwa upasuaji.
lol, pole mama ila ndio ukubwa huo!
 
Back
Top Bottom