Nimeleta uzi Jana wa
Mwanae hanitaki kabisa, nifanyeje? kuomba ushauri kuhusu huyu kijana ambae naishi na mama yake nyumba moja, na tunaishi na huyu kijana pia mwenye miaka 21, mimi Nina 34 na mpenzi wangu ana 51.
Lakini kinyume na matarajio yangu nimetukanwa sana kwenye uzi huo kwamba nimefuata pesa kwa mama huyo, kwamba mimi ni marioo.
Nimesikitishwa sana hivyo naomba kusahihisha.
(1) Wakati wanafungua chuo huyu kijana aliombwa na mama yake akakae hostel ili tupate nafasi ya kupumua mle ndani lakini akakataa, lengo la kukataa ni kutaka kutuvurugia mapenzi yetu, na ameapa atayavuruga tu kwa namna yoyote ile.
(2) Huyu kijana ana baba yake aliyemkimbia mama yake na kwenda kuoa mwanamke mwingine, sasa mama yake nae akiwa na mpenzi kuna ubaya?
Na kwanini basi asiende kuishi kwa baba yake Dar?
Hadi ang'ang'anie hapa na kutuletea fujo?
Isitoshe mimi ini mkubwa kwake 34 kwa 21 ni tofauti kubwa sana ya umri, mimi sio age mate wake, mnaobeza tofauti hiyo mnanishangaza sana.
(3) Ingekuwa tunazungumzia mwanaume ana miaka 80 na binti miaka 18 msingeona ajabu, tena akina dada wangekuwa wanashabikia kabisa, lakini inapotokea mwanamke ndie mkubwa inakua ajabu!
Sielewi kwanini mnakua hivyo.
Huyu mwanamke wangu anajiweza kimaisha na ameamua kunisaidia mimi kimaisha kama mpenzi wake ambae nilikuwa najikongoja kimaisha, kuna ubaya? Mbona mwanaume tajiri anapomsaidia binti maskini maisha hamsemi?
Ikiwa kinyume chake ndio mnasema? Wakati kuna thawabu nyingi sana mwanamke akifanya hivyo. Nimemvumilia sana huyu kijana na nimefika mwisho, hawezi kunitangaza mimi mtaa mzima na kunidhalilisha kwa ndugu na jamaa, mbona alipotaka kufukuzwa na mama yake mimi niliingilia kati?
Mimi pia ni mafia, nafanya utu tu, sasa utu huo nauvua ngoja tuone sasa na nyinyi wanaume wenzangu humu ndani inakuwaje mnashindwa kuniunga mkono na kunipa support kwa jambo hili?
Mnaungana na watoto wa kike kunishambulia badala ya kunishauri njia nzuri ya kutatua hili tatizo. Mimi na mpenzi wangu tulitaka kufunga ndoa siku nyingi ili tuweze kuishi kwa amani na upendo lakini kutokana na huyu kijana mama yake anaahirisha kila Mara, anajaribu kunivurugia.
Ngoja tutaona, nimechoka sasa.