The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 4,780
- 8,155
Hakuna jambo lililoumiza akili za Watu kwa miaka mingi kama Mada hii. Kwa karne nyingi mwanadamu amekuwa akihangaika sana kutaka kufahamu yeye ni nani. Hata hivyo kumekuwa na majibu tofauti yanayoelekeana, na leo hii nimeamua kukufahamisha.
Nitaenda kukufundisha mwanadamu ni nani kwa kutumia Nyanja kuu tatu, ambazo ni sayansi, dini na Utamaduni, Na mwisho ninatoa hitimisho lenye kutoa mwanga kwa upana wake.
NYANJA YA KWANZA: MTAZAMO WA KISAYANSI
Sayansi inasema: Mwanadamu si Mwili, chukulia mfano wa Jinsi simu yako ilivyo. Simu yako si muonekano wa nje. Muonekano wa nje ( Hardware) ni sehemu ndogo sana katika simu yako ya mkononi. Sehemu yenye uzito katika simu ni software, Hardware inatambulishwa kama motherboard ama chombo pekee cha kubebea Hii energy Ama nishati.
Vivyo hivyo, mwanadamu Ni Software ( nishati) ambayo hubeba taarifa zote za mtu, kama vile Nishati ndani ya simu inavyoweza kubeba taarifa za simu yako. Katika sheria Ya Uhifadhi wa Nishati,
"Nishati haiwezi kuumbwa wala Kuangamizwa, bali yaweza kubadilishwa kutoka hali moja kwenda hali nyingine"
sheria hii inatoa mwanga kuwa kuna uwezekano wa Nishati iliyopo ndani ya mwili wa Mwanadamu kutokuumbwa wala kuto-angamizwa baada ya kuzaliwa na kufa kwake, bali Kubadilika kutoka katika hali moja kwenda hali nyingine. Nisielezee sana hii nyanja, nihamie nyanja ya pili ili kupata mwanga wa hii nyanja ya kwanza.
NYANJA YA PILI: MTAZAMO WA KIDINI.
Katika mtazamo wa kidini, mwanadamu anatambulishwa kama muunganiko wa Mwili (udongo) na Roho ( nishati). Vitabu vya dini Vinatoa Ufafanuzi mzuri kuwa mwanadamu ili aweze kuwa hai Physically, ni lazima Roho ambayo ni nishati iungane na mwili ambao kisayansi tumeutambulisha hapo kabla kama mother-board ama Chombo cha kuibebea hii nishati.
Asili ya Roho Hii ama nishati hii ni Mungu mwenyewe. Maandiko humtaja Mungu kama Roho. Ni wazi kwa mujibu wa dini kuwa Mungu Hakuumbwa wala hawezi kufa , Na hivyo sayansi inapata Kuingiliana vema na dini kuwa "nishati haiwezi kuumbwa wala kuharibiwa, bali hubadilishwa kutoka katika hali moja kwenda katika hali nyingine".
Dini hufundisha kuwa mtu hufa, lakini haifundishi kuwa Roho Ama Nishati hufa.. Mara nyingi nishati hurudi katika asili yake ya awali yaani kwa Mungu. Hii inatoa picha gani, inatoa picha ya wazi kuwa mwanadamu anapokufa, nishati ndiyo hutoka ndani ya mwili, na mwili kubaki bila utambuzi. Nishati hii kwa kuwa ndiyo hubeba maarifa yote ya Mwanadamu, basi huondoka nayo na kuuacha mwili bila maarifa. Hivyo Maandiko yanafundisha kuwa mwisho wa dunia, ataziangamiza Hizi Nishati kwa kuwa Yeye ndiye chanzo chake.
Je kuna ushahidi katika vitabu vya dini? Ndio, kitabu cha henoko kimeitaja Roho ya habili ikilia kwasababu ya Ndugu yake kaini alyemuua, kitabu cha mwanzo kikiitaja damu ya habili ikilia pia. Kitabu cha mathayo kimemtaja Lazaro na Ibrahimu, kitabu cha Ufunuo kikizitaja roho za waliouawa kwa ajili ya ushuhuda zikilia kwasababu ya Kulipiwa kisasi.
Je hapa kuna muunganiko gani kati ya Sayansi na dini?
Katika tafiti zilizowahi kufanywa kwa watu waliokaribia na umauti wao, watu hawa walidai kujiona wakitoka nje ya miili yao na kujihisi wenye uwezo mkubwa tofauti na walivyokuwa katika ubinadamu wao. Hii inaashiria kuwa, kuna uwezekano wa Nishati kuishi ndani ya mwili, na kuweza kuondoka ndani ya mwili ikiwa na utambuzi kamili.
NYANJA YA TATU: MTAZAMO WA KIJAMII.
katika jamii zetu za Afrika, kumekuwa na shuhudu kutoka kwa watu hasa wakati wa usafirishaji wa Marehemu bila kufanya taratibu za jadi. Waliokiuka taratibu hizi Kwa kusafirisha maiti bila kufuata taratibu za jadi, wamekuwa wakikutana na misuko suko mingi njiani.
Je ushuhuda huu unahusiana na Nyanja za juu?
Ndio, Kwa upande wa kisayansi, waafrika wamekuwa wakifanya mambo ya jadi ili kubadili nishati kutoka hali moja kwenda hali nyingine ili Mwili wa hii nishati uweze kusafirishwa kiurahisi. Hata hivyo hakuna ushahidi wa Wazi wa namna nishati hii inavyobadilishwa, lakini mara nyingi hutumia njia za jadi zijulikanazo na wengi kama ushirikina ili kurahisisha Shughuli hii ya Kusafirisha Marehemu.
Kwa ujumla, nyanja zote tatu zinaingiliana katika mtazamo wa Mwanadamu na kutoa taswira ya wazi kuwa, Mwanadamu ni nishati (Energy) ijulikanayo kama Roho katika dini, ambae anaishi ndani ya Mwili.
Mwili unapokoma ama kufa, Nishati hii huondoka na utambuzi wote, ikiuacha mwili bila utambuzi wowote. Nishati hii huwa na uwezo upitao uwezo wa kawaida, na kwa karne nyingi mwafrika amekuwa akiibadilishwa kutoka katika hali moja hadi hali nyingine kwa njia ya Matambiko na tamaduni nyingine za kiroho, ili isiweze kuleta madhara kwa binadamu walio hai.
Nini tuelewe? Vema, Uelewa wa wazi ni kuwa mwanadamu hafi, kinachokufa ni mwili pekee na Yeye huendelea kuwa hai ila nje ya mwili kama nishati..
Nishati hii hubaki na utambuzi wake wote..