Mwanadamu anajivunia nini?

Mwanadamu anajivunia nini?

kirisha

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2017
Posts
573
Reaction score
663
MWANADAMU ANAJIVUNIA NINI?
Nimekuwa najiuliza swali hili miaka mingi sana, na pengine ndilo lilikuwa swali lililonipa maamuzi ya kuona namhitaji Yesu kuwa mwokozi wangu. Sijui kama nawe umewahi kujiuliza pia, Eeh mwanadamu unajivunia nini?

Siku zako ni fupi sana, na zimejaa mashaka, kabla hujazaliwa hukumbuki ulikuwa wapi, umeikuta dunia bahati mbaya sana hutaishi milele, japo wadhani kama kufa ni kwa wengine mpaka unahisi hutakufa, lakini ukweli ni kwamba utakufa je! bado una cha kujivunia?

Usalama wako ni wa mashaka sana, kama una mali hulali kwa amani maana hujui majambazi wanakupangia mikakati gani, kama huna Mali pia una hofu maana hujui hata ukiugua ghafla utatibiwaje, maisha yako yamejaa hofu na wasiwasi mwingi, je! bado una cha kujivunia?

Chakula chako kina matishio mengi, kama una uwezo wa kununua chochote nafsi yako inakitamani ili ule, bado unakumbana na matishio ya sumu, sukari, na magonjwa mengi ndani ya chakula chako. Kama huna uwezo wa kupata chakula nafsi yako inakitamani ili ule, bado una tishio la kukosa virutubisho muhimu kwa mwili wako, na hii hukusababishia kukosa afya madhubuti na kukusababishia madhara mengi, Je! Bado una cha kujivunia?

Ukiufuata moyo wako kwa anasa za dunia, utajifurahisha kwa muda lakini ukweli ni kwamba baada ya anasa moyo wako hukuuma sana na hukusababishia majuto na wasiwasi, wa magonjwa, hatia, usaliti na hatari. Na kama huna uwezo wa kupata anasa za dunia unaitesa nafsi yako kutamani ambacho huwezi kukipata, na kukufanya kuwa mtumwa wa nafsi yako mwenyewe, na hii hukupotezea muda, akili, na utulivu wa maendeleo na mwisho kubakia maskini. JE! MPAKA SASA BADO UNA CHA KUJIVUNIA?

Ukiwa na cheo lawama, hulali, hutulii, hofu imekujaa, maana huna uhakika utadumu kwa muda mrefu na cheo chako. Usipokuwa nacho unajiona mnyonge na mdhaifu kwa kila mtu, unajiona kama panzi mbele ya kunguru, bado huna utulivu moyoni, japo unajitutumua sana. Je! Una kipi cha kujivunia?

Ukiwa na jina, sifa, na uwezo wa jambo lolote bado haikufanyi Uwe mtoshelevu, ndio maana unahitaji walinzi, unatembea kwa kujishtukia, na mashaka pande zote maana unajua fika si wote wanaokuwazia mema. Usipokuwa na sifa, jina na uwezo bado unajiona hujakamilika, unahisi kudharauliwa hata na wasiokudharau, ukipita wakicheka unadhani wachekwa wewe bado huna raha na hali yako. Bado tu unahisi unacho cha kujivunia?

Ukiwa tajiri mateso, ukiwa maskini shida, ukiwa unacho mashaka, ukiwa huna mnyonge, UNACHOKITAMANI WALIONACHO WANAJUTA KUWA NACHO, USICHOKITAKA KINAKUKABILI SANA, KILA UPANDE NI HOFU, MASHAKA, MAJUTO, WASIWASI, MPAKA SASA HUJIAMINI NA HUELEWI UKIFA SASA HATIMA YAKO IKOJE. JAPO WAJUA SANA UTAKAKOKWENDA. JE! BADO UNAJIVUNA?

Maandiko ya Mungu yako wazi, mwenye haki ataishi kwa imani, kwa nini usichague fungu hili? Ili hata kama unacho Uwe nacho kwa imani, na kama huna usubiri kwa imani na uridhike? KWA HALI TULIYOPO NASHAURI MKABIDHI YESU MAISHA ILI KAMA UTAJIVUNA BASI UJIVUNE KWA KUWA UNAMJUA BWANA YESU. Chukua hatua leo umkabidhi Yesu maisha yako maana kesho yako huijui. MUNGU AKUPE NAFASI ZAIDI
 
Ubarikiwe sana mtumishi, wewe ni mtu unayetafakari sana maisha na hatima ya mwanadamu. Huo ni ukweli usiopingika kwamba tumaini pekee na furaha ya ukweli hupatikana kwa Mungu. Mi huwa najiuliza inakuaje watu misibani wanakua wanyenyekevu na wapole huimba nyimbo za kumtukuza Mungu bila kujali itikadi za imani zao,lakini mara baada msiba huyarudia mambo yaleyale na kusahau kuwa kila binadamu atakufa.Tafakari chukua hatua..
Wafilipi 1:21 "Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo na kufa ni faida"
 
MWANADAMU ANAJIVUNIA NINI?
Nimekuwa najiuliza swali hili miaka mingi sana, na pengine ndilo lilikuwa swali lililonipa maamuzi ya kuona namhitaji Yesu kuwa mwokozi wangu. Sijui kama nawe umewahi kujiuliza pia, Eeh mwanadamu unajivunia nini?

Siku zako ni fupi sana, na zimejaa mashaka, kabla hujazaliwa hukumbuki ulikuwa wapi, umeikuta dunia bahati mbaya sana hutaishi milele, japo wadhani kama kufa ni kwa wengine mpaka unahisi hutakufa, lakini ukweli ni kwamba utakufa je! bado una cha kujivunia?

Usalama wako ni wa mashaka sana, kama una mali hulali kwa amani maana hujui majambazi wanakupangia mikakati gani, kama huna Mali pia una hofu maana hujui hata ukiugua ghafla utatibiwaje, maisha yako yamejaa hofu na wasiwasi mwingi, je! bado una cha kujivunia?

Chakula chako kina matishio mengi, kama una uwezo wa kununua chochote nafsi yako inakitamani ili ule, bado unakumbana na matishio ya sumu, sukari, na magonjwa mengi ndani ya chakula chako. Kama huna uwezo wa kupata chakula nafsi yako inakitamani ili ule, bado una tishio la kukosa virutubisho muhimu kwa mwili wako, na hii hukusababishia kukosa afya madhubuti na kukusababishia madhara mengi, Je! Bado una cha kujivunia?

Ukiufuata moyo wako kwa anasa za dunia, utajifurahisha kwa muda lakini ukweli ni kwamba baada ya anasa moyo wako hukuuma sana na hukusababishia majuto na wasiwasi, wa magonjwa, hatia, usaliti na hatari. Na kama huna uwezo wa kupata anasa za dunia unaitesa nafsi yako kutamani ambacho huwezi kukipata, na kukufanya kuwa mtumwa wa nafsi yako mwenyewe, na hii hukupotezea muda, akili, na utulivu wa maendeleo na mwisho kubakia maskini. JE! MPAKA SASA BADO UNA CHA KUJIVUNIA?

Ukiwa na cheo lawama, hulali, hutulii, hofu imekujaa, maana huna uhakika utadumu kwa muda mrefu na cheo chako. Usipokuwa nacho unajiona mnyonge na mdhaifu kwa kila mtu, unajiona kama panzi mbele ya kunguru, bado huna utulivu moyoni, japo unajitutumua sana. Je! Una kipi cha kujivunia?

Ukiwa na jina, sifa, na uwezo wa jambo lolote bado haikufanyi Uwe mtoshelevu, ndio maana unahitaji walinzi, unatembea kwa kujishtukia, na mashaka pande zote maana unajua fika si wote wanaokuwazia mema. Usipokuwa na sifa, jina na uwezo bado unajiona hujakamilika, unahisi kudharauliwa hata na wasiokudharau, ukipita wakicheka unadhani wachekwa wewe bado huna raha na hali yako. Bado tu unahisi unacho cha kujivunia?

Ukiwa tajiri mateso, ukiwa maskini shida, ukiwa unacho mashaka, ukiwa huna mnyonge, UNACHOKITAMANI WALIONACHO WANAJUTA KUWA NACHO, USICHOKITAKA KINAKUKABILI SANA, KILA UPANDE NI HOFU, MASHAKA, MAJUTO, WASIWASI, MPAKA SASA HUJIAMINI NA HUELEWI UKIFA SASA HATIMA YAKO IKOJE. JAPO WAJUA SANA UTAKAKOKWENDA. JE! BADO UNAJIVUNA?

Maandiko ya Mungu yako wazi, mwenye haki ataishi kwa imani, kwa nini usichague fungu hili? Ili hata kama unacho Uwe nacho kwa imani, na kama huna usubiri kwa imani na uridhike? KWA HALI TULIYOPO NASHAURI MKABIDHI YESU MAISHA ILI KAMA UTAJIVUNA BASI UJIVUNE KWA KUWA UNAMJUA BWANA YESU. Chukua hatua leo umkabidhi Yesu maisha yako maana kesho yako huijui. MUNGU AKUPE NAFASI ZAIDI
AMEEN!
 
Nimesoma sentensi ya mwanzo tu, binadamu ana mengi ya kujivunia..
 
Amen
 
Yote ni ubatili na kujilisha upepo huwezi shindana na dunia ni sawa na kuufukuza upepo, idi amini baada ya yote,kuabudiwa,kuuwa watu,kutesa,kufilisi,kubomolea watu nyumba, na kila ovu,siku za mwisho za uhai wake alijutia sana kwa Mola wake yote aliyoyatenda na kuyaona si lolote si chochote, hayana tija wala hayamsaidii.Hata uwe na PhD ya roho mbaya kuumiza,kutesa,kufunga watu nk sababu unayo nafasi sasa,siku zaja utaona ni ujinga na utoto tu.Ukishaoga damu ya MTU utotakata na utajiona mwenye hatia u mchafu hadi mwisho wa maisha yako.Hata ung'ang'ie vipi dunia utoimaliza,
 
Back
Top Bottom