Mwana mpumbavu ni mzigo kwa mamaye! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwana mpumbavu ni mzigo kwa mamaye!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Masanyaraz, Aug 6, 2011.

 1. M

  Masanyaraz Member

  #1
  Aug 6, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unapo zungumzia nchi zilizokua mstari wa mbele kutaka uhuru wa nchi za kiafrika,hautakosea ukitaja TANZANIA.
  Katika nchi za kusini,mashariki na kati mwa AFRIKA,Ilipasa nchi kama tanzania iwe mstari wa mbele katika maswala kama ifuatavyo;
  1)kiuchumi,kwasababu tunarasilimali za kila aina,
  mfano;rasili mali ardhi pamoja na rasilimali watu,ambapo enzi za utumiaji watu katika maendeleo ya kilimo kulikua na mafanikio!serikali ilikua ina akiba ya kutosha ya vyakula na ikitokea kunashida ya chakula mahali fulani,kilikua kinapatikana chakula bure kwa wananchi.
  Maswala ya kukimbilia mijini kwa kigezo cha kutafuta maisha hakikuwepo kwasababu ya kuwepo na ajira ardhi ya kutosha etc.
  2)madini;nchi yetu ina aina ya madini zaidi ya nane,ikiwema na urenium ambayo muda si muda yataanza kuchimbwa.
  Lakini cha ajabu bado tuna tegemea wahisani katika bajeti zetu,
  mf;nchi ya botswana wanamadini ya akiba ambayo ni ghafi ya kuweza kuilisha nchi yao kwa miaka mitatu!
  Tafakari,kama nchi hii ingeweza kutumia rasilimali tulizopewa na mungu,tungeendelea kuwa omba omba hata kwa fedha za mishahara ya watumishi wake!MZIGO HUU NA LAWAMA HIZI NI KWANANI,au tuseme amekosekana wa KUMFUNGA PAKA KENGELE?
  Nawasilisha.
   
Loading...