magnifico
JF-Expert Member
- Jan 14, 2013
- 9,905
- 21,212
Mi nakumbuka siku fulani mwaka nimesahau niliwahi kukutana na uzi jamaa anawadiss Wanafunzi wa vyuo wanaoning'iniza vitambulisho hata wakiwa nje ya chuo. Basi akatokea jamaa akamquote "Kwani kuna tatizo? Kama unaona wanafaidi na wewe chukua kadi yako ya bima ning'iniza shingoni". Aisee nilicheka sana siku ile.
Pia kule kwenye uzi wa wazee wa mikeka kuna jamaa povu lilimtoka kisa kuna mwanachama dau lake aliliweka kwenye mtindo huu 10k. Niwe mkweli nimeshakutana na matukio ya kukurupuka ila huyu ndugu yangu alitia fora. Yeye alidai huo ni ulimbukeni kutumia k(akiwa na maana ya Kenyan Shilling) badala tsh.
Ila baada ya ubishani mkali jamaa akasema alikuwa anatujaribu tu.
Vipi wewe tukio gani limewahi kukufurahisha,kuchekesha ama kukushangaza?