MAKOLE
JF-Expert Member
- Feb 5, 2012
- 618
- 280
Kwa muda mrefu sasa waajiri wangu walinipa kibarua na kufanya kazi peke yangu hadi nikafikiria kuomba msaada kutoka kwa mabosi wangu watafute namna ya kuongeza wafanyakazi ili pindi ninapochoka au kuugua (kwa maana mimi ni mwanadamu) wafanye kazi badala yangu.
Kwa kweli waajiri wangu walikataa kata kata kuajiri wafanyakazi wengine hapa ofisini lakini mimi nikalazimisha hata wakakubali ingawa kwa shingo upande. Waliajiriwa watumishi wengi katika ofisi hii ambayo shughuli yetu kubwa ni kuendesha chombo baharini. Nimeshindwa kabisa kujizuia na nimejikuta nikiwa chanzo cha migogoro mingi hapa ofisini.
Yaelekea uzee nao unachamgia kwani waajiriwa wapya wengi ni vijana ambao wanao uwezo wa kwenda kasi sawa na mawimbi ya bahari yaendavyo. Najihisi sasa nimekuwa kikwazo. Wakati mwingine nalazimika kuwafitinisha hawa waajiriwa wenzangu kwa muajiri wetu ili nionekane bado nahitajika na nina umuhimu sana chomboni, hivyo hawa waajiriwa wenzangu hukabiliana na matatizo na wanatazamwa kwa jicho baya na hawa waajiri wetu.
Katika hali ya kawaida ndugu zangu wana JF, natakiwa kufanya nini ili walau basi nami nitazamike mwenye busara pamoja na mvi zangu nilizonazo kichwani?
Msaada tafadhali!