Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma (Mwana FA) muziki wa singeli unashika na unakubalika maeneo mengi hadi nje ya nchi lakini pia ni muziki ambao asili yake ni Tanzania hivyo ametaka Watanzania kuwaunga mkono Wasanii wa singeli, kuusafisha muziki huo, kuwaelekeza bila ukali Wasanii wanapokosea ili kuufanya muziki huo uwe bora zaidi na utambulisho wa Taifa.
Akiongea wakati wa mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Mwinjuma amesema "Wabunge kadhaa hapa wameongea toka asubuhi kwa hisia nyingi kuelezea jinsi ambavyo kuna sintofahamu juu ya kwanza singeli kuwa muziki wa Taifa lakini halikadhalika maudhui yanayobebwa kwenye aina hii ya muziki, hakuna Mtu yoyote aliyesema mahali popote kwamba tunataka kuifanya singeli kuwa muziki wa Taifa"
"Tuliona muziki huu umeshika na unakubalika maeneo mengi ikiweno nje ya nchi, Mimi binafsi nimewahi kwenye maonesho ya singeli nje ya nchi na muziki huu unafanya vizuri sana, ukweli ni kwamba hakuna Mtu yoyote kutoka sehemu nyingine yoyote Duniani anayeweza kuja kudai kwamba singeli ina asili ya nchini kwao, kimsingi singeli ina asili ya kutoka Tanzania"
"Tulikuwa tunawasaidia Vijana hawa kuubrand muziki wa singeli na kuusafisha, uhuni unaosemwa upo kwenye singeli Mimi kama Mwanamuziki najua uhuni upo kwenye miziki yote na Vijana hawa wanahitaji maelekezo na sio kususwa kama ambavyo tunasema kwa ukali"
Pia, Soma: Profesa Kabudi atangaza kusambaza Singeli Dunia Nzima. Atatumia njia gani? Anajua mwenyewe