Mwana FA: Muziki wa Ma group ulishafeli, hauwezi kurudi tena

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,059
Mwana Fa amadai kwa sasa muziki wa ma group hauwezi kulipa tena kutokana na hali ya uchumi wa muziki kwa sasa, ametolea mfano wa ma group ya muziki ya Marekani waliyokuwa wameyaiga kama D12 yalivyokufa na wasanii wake kubaki solo kwa kuwa ma group kiuchumi haulipi

 
Mwana fa kaongea kama mtu aliye filisika kiwawazo huwezi kutole mfano wa magrup ya mziki wa Marekani na vitu vya kipuuzi

Magrup mengi ya Marekani wanajitenga kutokana na maslai binafsi na siyo kuwa magrup ya Music wa Marekani haulipi! Marekani si sawa na bongo unatoa albuni unauza copy kumi!
 
Ni kitu cha kweli.

Zamani wangeweza kuuza Albam na wakapata hela pia ila siku hizi mambo yamekuwa tofauti na makundi yanavunjika.

FA kasema kitu ambacho kipo Leo hii hakuna makundi yenye nguvu kwenye bongo flava tofauti na zama zile.
 
Mbona kuna groups kadhaa bado wanakamua pamoja; Naughty by Nature, De La, Lost Boyz, Migos, Weusi(they're pretty much a group), P Unit(?).

Ubinafsi una nafasi kubwa sana katika kuvunja groups, zaidi ya uchumi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom