Mwampamba kawaangukie wana wa Mbozi

Mwampamba kawaangukie wana wa Mbozi

Noboka

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2011
Posts
1,246
Reaction score
626
Naamini sarakasi za PM7 mtazimaliza huko kwenye chama chenu kama nilivyoona tamko la Mnyika humu ndani. Nimepita hapo Vwawa - Mbozi, nikakaa kwenye Bar moja ukweli Mwampamba unapaswa urudi ukaongee na wananchi wako wa Mbozi.
Zoezi ambalo nimekuta linaendelea pale juu yako si zuri sana, inaonekana vijana waliokupigania na kukufiksha hapo ulipo mwaka 2010 wakati unagombea ubunge sasa wameamua kupambana na wewe tena kukuangamiza kisiasa si kimwili wala kiroho. Wanatumia utaratibu uleule wa kuchangishana lakini safari hii wanachingishana ili waweze kurudufunakala za baadhi ya matusi ambayo umekuwa ukiporomosha kwa viongozi wako ili wasambaze vijijini, naTatizo kubwa wanasema uliwatukana na kuwaambia ni wanafiki wakati wanajua wao ndio waliokuwa wanakununulia hata maji ya kunywa kwa kuchangishana vihela vidogo kama sh. 50, 100 n.k. Kuliko kuendelea kupambana huku kwenye mitandao binafsi ningekushauri ukaweke mambo sawa huko kwako kwani kisiasa bado una nafasi na umri unakuruhusu. Siamini kama Zitto au Habibu ana ugomvi na wapiga kura wake, ila wewe wapiga kura wamegawanyika hasa vijana ambao unafahamu walikupigania sana hata kama hukufanikiwa kuchaguliwa.
Ni ushauri tu
 
Misukule haielewi kitu mkuu Noboka. Hapo ni sawa na kumpigia mbuzi marimba
 
Last edited by a moderator:
Upate ubunge wa wapi? Nani kakudanganya sio vijana walimpigania bali walikipigania chama kama unataka kuamini mwambie agombee Kupitia Chama cha CHAUMA ambacho yeye ni MUASISI, Huyo dogo anakiburi sana hafai hata kuwa Mbunge wa MAZEZETA. Na msijidanganye kwamba atajirekebisha kwani kuna mtu alisoma naye META SEC na DUCE alisema kwa jinsi alivyokuwa akivuta bangi mpaka walikuwa wanamwita GANZI. Na habari kutoka huko kwao zinasema dogo huyo mwampamba aliwaambai wana MBOZI kuwa akipiga MRIZI KAMA ANAITA MBWA WATU WA MBOZI WANAMFUATA sasa vijana wana hasira naye hata KUMTANDIKA.
Kibaya zaidi kuna mtu ambaye analitaka hilo jimbo na anamkakati mkali kweli Nimesahau jina lake ila najua ni ENGINEER fulani.
HAKIKA HARAMU NI HARAMU TUU.
 
Misukule haielewi kitu mkuu Noboka. Hapo ni sawa na kumpigia mbuzi marimba

bangladesh-rats.jpg
 
Mbona nasikia keshasema siasa basi tena, anarudi kwenye fani yake ya zamani ya kukata viuno.

Mkuu hapo kwenye nyekundu sina uhakika ila ninajojua Mwampamba kitaaluma ni Mwl. ingawa nasikia ualimu aliacha ili kujikita kwenye chama zaidi. Pamoja na hayo hata kama hataki siasa bado kufikia muafaka na vijana wenzake hapo Mlowo, Vwawa na viunga vyake bado ni jambo la msingi
 
Hakuacha kwa ajili ya chama!.. Alipangwa kagera na kuripoti kazini, akapokea mshiko kisha akasepa na hela za serikali. Kimsingi serikali ingekuwa makini hivi sasa angekuwa lupango au mafichoni!..
 
Huyu bwana mdogo nilisoma Nae shule ya msingi MLOWO ninamuelewa vizuri, na sidhani Kama atakuwa amebadirika (bangi) kwake nikawaida.
 
daaa hatare ndo mana anaakili ndogo sana, sasa chabema tulianzaje kuwapitisha watu matabulalaza kama mwambamba
Kwenye kundi la mamba kenge hawakosekani, ni rahisi kuwabaini na kuwatimua coz siku zote wao hudumaa na kuendelea kuwa kenge..!
 
Jamani wanaJF,

Kwa kupitia thread hii, naomba niwajuze kitu kwa wasiofahamu. Lkn msiniite mkabila.

Mengi sana yamesemwa hivi karibuni kuhusu Mwampamba, Shonza, Mchange na Saa8. Shonza na Mwampamba wanatoka Mbeya. Kwa bahati au nzuri, watu wengi wanajua kuwa Mbeya kuna Wanyakyusa tu. Hapana, Mbeya kuna makabila mengi tu kama Wasafwa, Wandali, Wanyiha, Wabungu, Wanyakyusa, Wanyamwanga, n.k.

Kwa taarifa ya wale wasiojua, Mwampamba na Shonza ni Wanyiha kutoka Mbozi.

Samahani kwa niliowakwaza.
 
Huyu bwana mdogo nilisoma Nae shule ya msingi MLOWO ninamuelewa vizuri, na sidhani Kama atakuwa amebadirika (bangi) kwake nikawaida.

Kuvuta avute Mbowe akivuta Mwampamba inageuka nongwa
 
Jamani wanaJF,

Kwa kupitia thread hii, naomba niwajuze kitu kwa wasiofahamu. Lkn msiniite mkabila.

Mengi sana yamesemwa hivi karibuni kuhusu Mwampamba, Shonza, Mchange na Saa8. Shonza na Mwampamba wanatoka Mbeya. Kwa bahati au nzuri, watu wengi wanajua kuwa Mbeya kuna Wanyakyusa tu. Hapana, Mbeya kuna makabila mengi tu kama Wasafwa, Wandali, Wanyiha, Wabungu, Wanyakyusa, Wanyamwanga, n.k.

Kwa taarifa ya wale wasiojua, Mwampamba na Shonza ni Wanyiha kutoka Mbozi.

Samahani kwa niliowakwaza.
Kwa hiyo hapa umetaka tujue nini? funguka.

Mkuu Mawenzi, kwani kuna mtu akiwatuhumu watu wa Mbeya kwa ujumla? Pia sidhani kama kabila kwa jinsi yoyote linahusika na matendo haya yaliyotokea na kuwahusisha hawa au ulitaka kuleta ujumbe gani?
 
Jamani wanaJF,

Kwa kupitia thread hii, naomba niwajuze kitu kwa wasiofahamu. Lkn msiniite mkabila.

Mengi sana yamesemwa hivi karibuni kuhusu Mwampamba, Shonza, Mchange na Saa8. Shonza na Mwampamba wanatoka Mbeya. Kwa bahati au nzuri, watu wengi wanajua kuwa Mbeya kuna Wanyakyusa tu. Hapana, Mbeya kuna makabila mengi tu kama Wasafwa, Wandali, Wanyiha, Wabungu, Wanyakyusa, Wanyamwanga, n.k.

Kwa taarifa ya wale wasiojua, Mwampamba na Shonza ni Wanyiha kutoka Mbozi.

Samahani kwa niliowakwaza.

KAMANDA mwampamba sio mnyiha ni MMALILA kwa ASILI ila wazazi wake wamekaa mbozi. nina ndgu yangu anamfahamu hata baba yake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom