Mwambieni Gianni Infantino; Wallace Karia na tabia za kisiasa za kiafrika zinaua maendeleo ya soka la Tanzania

Mti Dawa

Member
Aug 10, 2022
6
20
Huku Tanzania ikitoka kupokea ugeni mkubwa wa Rais wa Shirikisho la mpira duniani FIFA, Ndg. Gianni Infantino pamoja na Rais wa CAF Bw. Motsepe, ni Karia ndie anaenekana shujaa wa kuuleta ugeni huo kaa mara ya kwanza katika historia kufanya mkutano wake katika ardhi ya kihistoria Arusha.

Kauli ya Bw. Gianni Infantino wakati Rais wa TFF akihojiwa ya kuwa "He is the best" yaani akimaanisha Karia ni Rais bora kabisa wa shirikisho ni kauli inayoonyesha namna mgeni anaweza kuja nyumbani na kumsifia baba wa kambo kwa malezi bora na nguo mpya alizowanunulia watoto wa kambo sababu tu anajua kuna mgeni atakuja hii leo.

Aliye karibu na Rais Infantino amueleze haya kuhusu Karia kabla hajaamua kumsifia.

Rais Gianni Infantino bila kujua na katika kuonyesha 'hospitality' alimsifia Karia, lakini mtu amueleze Infantino.....

1. Rais Karia anaingia mikataba ya matangazo ya vilabu bila ridhaa ya vilabu vyenyewe wala matakwa yao, hakuna shirikisho duniani linafanya wizi huu kwenye biashara ya soka duniani kote.

2. Rais Karia ndie alietoa kauli za kuwaita viongozi wengine katika familia ya soka ni "ma-Tundu Lissu" wa mpira, bila kujali wala kuzingatia kuwa mwanasiasa huyo anaetumia taswira yake kwa 'ubaya' ni kiongozi wa Taasisi nyingine ya kisiasa na kauli yake inahatarisha ufuasi wa mpira nchini kuchafuana na ufuasi wa kisiasa ndani ya nchi.

Hakuna Rais wa shirikisho la mpira lolote duniani ameshawahi kuropoka kauli za namna hii, hatujawahi sikia watu kama Osama, Trump, Obama wala aina yoyote ya wanasiasa, iwe watawala au wapinzani wakitolewa mifano mibaya ya kimpira ila Karia amefanya hivyo mbele ya mkutano wa TFF.

3. Infantino aje tumueleze kuwa Karia hakosolewi kwa mdomo wala kwa mitandao, adhabu yake ni kifungo cha maisha, miaka mitano na faini zenye kufilisi vilabu vya Tanzania ambavyo vingine hata gharama za kusafirisha timu havina, wengine mpaka wanakula ugali na maharage kambini kipindi cha mashindano, ila faini za Karia ni milioni 20.

4. Infantino aje tumueleze kuwa wakati Sepp Blatter alipofungiwa miaka kadhaa kwa kosa la rushwa huko ulaya, huku Tanzania Karia anafungia watu kujihusisha na soka maisha yote, yaani kifungo cha maisha, na ingebidi kuwepo adhabu kama kunyongwa hadi kifo tunaamini Karia angeitumia vema kwa jinsi alivyo dikteta na mbabe katika kiti cha TFF.

5. Infantino aje tumueleze, kuwa Kanuni ambazo zinatumika na TFF hazijasaliwa popote pale nchini, ni kanuni za kuchonga na zingine zinatolewa mifukoni mwa watu nje ya TFF ilimradi ni maagizo ya kundi la watu na washkaji wa Karia kutoka katika serikali.

6. Infantino aje tumueleze, kuwa tangu Karia ashike madaraka, kamati na sekretarieti za maadili zote zinamuabudu Karia, akikohoa Karia basi rungu ni kifungo.

7. Infantino tumueleze vema, kuwa TFF ndio inasimamia Ligi, ndio inasimamia timu zote za Taifa, ndio inasimamia wadhamini na kila kitu ni TFF, bodi ya ligi ni pambo tu na spika za kuzungumza kinachosemwa na Karia mwenyewe.

8. Infantino aje tumueleze, kuwa hata yeye akimkosoa Karia kwenye ukurasa wake wa Instagram atafungiwa kwa kanuni za mchongo, bila kuelezwa utofauti wake yeye kama mshabiki na mwanafamilia wa soka na chombo kilichochapisha maudhui husika.

Yaani Kurasa ya Gianni Infantino ikiposti kitu kinachomkera Karia, basi atafungiwa Infantino kutojihusisha na soka na sio ile kurasa kuchukuliwa hatua za kimamlaka ya mawasiliano.

Mwisho kabisa: Infantino atambue kuwa Karia ni gogo lililooza ambalo litaangukia watoto wa soka la Tanzania, linapaswa kuchanjwa kuni ili tuendelee na maendeleo ya soka letu, Karia ni kansa ndani ya TFF.
 
Nyinyi mashabiki ndio wahuniiiii Kwa nini mnabeba mabango ya CCM kwenda uwanjani!Vaeni nguo ,mabango yaliyoandikwa HATUTAKI SIASA VIWANJANI start jumamosi otherwise nyinyi mnapenda huo upuuzi
Kubeba mabango sio hoja katika mjadala huu, ubebaji wa mabango ni mapenzi ya mtu binafsi, huwezi mzuia mtu.
 
Hapo utasemwa umejaa kinyesi kwenye chupi yako.
 
Wasomali wana visasi sana....huyo aondoke tu kaja kuharibu radha yetu ya mpira na kuhangaika na mambo ya hovyo hovyo..
 
Msomali ni mwenzetu kwenye Chama Tawala, ila alipaswa apigwe chini sababu ni mpinzani. Wajuzi naona bado wamelala
 
Back
Top Bottom