Mwambie Mbunge wako akae kimya

Mwambie Mbunge wako akae kimya

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
Mtu mmoja kanitext hivi inbox;

SWALI: "Kaka mimi niko shirika..... (akataja jina la shirika). My basic sallary is TZS 3,231,000/= je kwa punguzo la paye leo nitanufaika kiasi gani?

JIBU: Kabla ya leo ulikua ukilipa PAYE 11% zidisha kwa 720,000/= 79,200/=. Kisha chukua ur BS 3,231,000/= toa 720,000/= then zidisha kwa 30% (ambayo ni excess charges) utapata 753,300/=. Ukijumlisha na ile 79,200/= ya PAYE utapata 832,500/= (jumla ya kodi).

Baada ya leo itakuwa PAYE 09% zidisha kwa 720,000/= 64,800/=. Then chukua your BS 3,231,0000/= toa 720,000/= then zidisha kwa 30% (ambayo ni excess charges) utapata 753,300/=. Sasa jumlisha na ile 64,900/= ya PAYE utapata 818,200/= (jumla ya kodi).

Sasa chukua kodi uliyokua ukilipa zamani 832,500/= kisha toa kodi mpya utakayoanza kulipa sasa hivi 818,200/= utapata jumla ya Shilingi 14,300/=.

Maana yake ni kwamba umepunguziwa Shilingi 14,000/= ambayo haitoshi hata kununua nyama kilo 3.

#MyTAKE
Nashauri Rais angepunguza percentage ya excess charges kwa wenye mishahara inayozidi 720,000/=. Maana kupunguza PAYE halafu excess charges (gharama ya zidio) ni 30% bado ni unyonyaji.

Kwa mfano huyu jamaa anayelipwa 3,231,000/= hata asingepunguziwa PAYE, badala yake akapunguziwa gharama ya zidio angalau akakatwa 10% hesabu yake ingekua hivi.

11% times 3,231,000/= ni sawa na 79,200/=. Then kwenye excess charges angekatwa 10% ya zidio. Yani 3,231,000/= minus 720,000/= times 10% ingekua 251,100/=. Kwahiyo angekatwa PAYE 79,200/= jumlisha gharama ya zidio 251,100/= jumla 330,300/=.

Lakini sasa hivi analipa 818,200/= na hapa ni baada ya punguzo la PAYE leo.

Hii ina maana kwamba punguzo hili la PAYE ni kiini macho tu. PAYE haina effect kama EXCESS CHARGES (gharama ya zidio) kwenye mishahara inayozidi 720,000/= itaendelea kuwa 30%.

Kama Rais angepunguza Excess charges angalau zikafika 10% kutoka 30% ziliko sasa hivi, ingekua na maana kubwa sana kuliko kupunguza PAYE.

Kwa kifupi ni kuwa punguzo la PAYE litawanufaisha zaidi wenye mishahara chini ya 720,000/= lakini kwa wanaolipwa zaidi ya hapo hakuna benefit ya maana. Hata hao wanaolipwa bellow 720,000/= bado watanufaika kidogo sana.

Nimeona nitoe ufafanuzi huu kwa sababu baadhi ya watu wameanza kumsifu Rais kwa punguzo hili la PAYE. Hadi wabunge wa upinzani nao wamebebwa na mkumbo huu na kuanza kuimba nyimbo na mapambio. Labda kwa sababu wabunge hawalipi kodi ndio maana hawajui sisi watumishi tunaathirika vipi.

Ukiona Mbunge yeyote anashangilia punguzo hili elewa tu kwamba anapenda namba lakini hajui hesabu. Kwahiyo jitahidi kumkumbusha hesabu kwa kutumia kanuni nilizozieleza hapo juu. Kupunguza PAYE wakati gharama za zidio ziko palepale ni kiini macho tu.

Yani Rais JPM alichofanya ni kutulazimisha tukatae ongezeko la mshahara. Maana kila ukiongezewa mshahara Serikali inakula 30% ya ongezeko hilo.

NB: Kuna watu wanaweza kuhoji mbona wapinzani waliomba PAYE ipunguzwe? Ni kweli tuliomba PAYE ipunguzwe tangu mwaka 2011 atleast isome single digit. Lakini single digit in both PAYE and Excess charges. Yani kama PAYE ni 09% basi na excess charges ziwe 09% pia. Sio kupunguza PAYE peke yake wakati excess charges zimebaki paleale. Na hizo ndizo zinazoumiza.

Kwa mfano wa huyo jamaa hapo juu ingekua excess charges zimepunguzwa angekatwa almost laki 3 kwenye mshahara wake. Lakini kwa punguzo hili la JPM bado ataendelea kukatwa laki 8 na ushee. Sasa hapa kuna punguzo gani?

Waambieni wabunge wenu wanaoshangilia punguzo la PAYE kuwa kazi bado. Wakomae ili gharama ya zidio (excess charges) ipungue kutoka 30% iliyopo sasa hivi hadi angalau 10%. Hapo ndio tutawaelewa. Otherwise wafunge midomo yao maana wanashanglia jambo wasilolijua.

Sio wa CCM sio wa UKAWA wote wako partial informed. Plz tell them to fight ili gharama ya zidio (exces charges) ipungue, otherwise let them shutup tuendelee kuumia kama tulivyozoea.

Sioni fahari yoyote Mbunge wa UKAWA au wa CCM kufurahia PAYE kupunguzwa wakati binafsi nimepunguziwa kiasi kisichozidi 14,000/= ambayo suruali moja ya "Jeans".

Nimeamua kusema hivi maana naona wabunge wengi wa UKAWA wanacheza ngoma ya Magufuli. Wanaanza kujitapa mara Upinzani tulishauri jambo hili tangu mwaka 2011,wengine wanapiga picha hadi hotuba ya kambi ya upinzani iliyozungumzia jambo hilo. Waambieni wakae kimya na wasiendelee kuongea vitu wasivyovijua.

Sina nafuu yoyote niliyopewa kwa kupunguziwa 02% kwenye PAYE wakati excess charges ni 30%. Ningewaona wabunge ni wa maana zaidi kama wangemshawishi Rais apunguze vyote viwe 09% sio kushangilia wakati watumishi tunaendelea kuumia.

Mwambie mbunge wako akae kimya.

Malisa GJ.!
 
Huyu Malisa akae kimya asijifanye mjuaji wa kila kitu. Mmekuwa watu wakulalamika kila kitu, a journey starts with a single step
 
Mkuu Mwanahabari Huru nadhani umesahau kutoa kiasi cha Sh. 170,000/= ambazo hazitozwi kodi! Hivyo jumla ya kodi anayotozwa huyo mwenzetu ni kama 775,000/=!
 
Huyu Malisa akae kimya asijifanye mjuaji wa kila kitu. Mmekuwa watu wakulalamika kila kitu, a journey starts with a single step

Pambana na hoja si kupambana na mtu. Aliyoyasema hapo juu yana maana sana. Weka na wewe hoja zako tukusikie sio kumwambia mwenzako mjuaji kama vile kuwa mjuaji ni dhambi.
 
Huyu Malisa akae kimya asijifanye mjuaji wa kila kitu. Mmekuwa watu wakulalamika kila kitu, a journey starts with a single step
Hoja yako ni nini hapa?!
 
Huyu Malisa akae kimya asijifanye mjuaji wa kila kitu. Mmekuwa watu wakulalamika kila kitu, a journey starts with a single step
Acha wivu wa kike,Malisa ana akili mingi,huwezi hata kuthubutu kujibu hoja yake bali unakuja na kelele tupu!Hayo aliyoyasema ni kweli au si kweli au hujui kilichozungumzwa?
 
Mtu mmoja kanitext hivi inbox;

SWALI: "Kaka mimi niko shirika..... (akataja jina la shirika). My basic sallary is TZS 3,231,000/= je kwa punguzo la paye leo nitanufaika kiasi gani?

JIBU: Kabla ya leo ulikua ukilipa PAYE 11% zidisha kwa 720,000/= 79,200/=. Kisha chukua ur BS 3,231,000/= toa 720,000/= then zidisha kwa 30% (ambayo ni excess charges) utapata 753,300/=. Ukijumlisha na ile 79,200/= ya PAYE utapata 832,500/= (jumla ya kodi).

Baada ya leo itakuwa PAYE 09% zidisha kwa 720,000/= 64,800/=. Then chukua your BS 3,231,0000/= toa 720,000/= then zidisha kwa 30% (ambayo ni excess charges) utapata 753,300/=. Sasa jumlisha na ile 64,900/= ya PAYE utapata 818,200/= (jumla ya kodi).

Sasa chukua kodi uliyokua ukilipa zamani 832,500/= kisha toa kodi mpya utakayoanza kulipa sasa hivi 818,200/= utapata jumla ya Shilingi 14,300/=.

Maana yake ni kwamba umepunguziwa Shilingi 14,000/= ambayo haitoshi hata kununua nyama kilo 3.

#MyTAKE
Nashauri Rais angepunguza percentage ya excess charges kwa wenye mishahara inayozidi 720,000/=. Maana kupunguza PAYE halafu excess charges (gharama ya zidio) ni 30% bado ni unyonyaji.

Kwa mfano huyu jamaa anayelipwa 3,231,000/= hata asingepunguziwa PAYE, badala yake akapunguziwa gharama ya zidio angalau akakatwa 10% hesabu yake ingekua hivi.

11% times 3,231,000/= ni sawa na 79,200/=. Then kwenye excess charges angekatwa 10% ya zidio. Yani 3,231,000/= minus 720,000/= times 10% ingekua 251,100/=. Kwahiyo angekatwa PAYE 79,200/= jumlisha gharama ya zidio 251,100/= jumla 330,300/=.

Lakini sasa hivi analipa 818,200/= na hapa ni baada ya punguzo la PAYE leo.

Hii ina maana kwamba punguzo hili la PAYE ni kiini macho tu. PAYE haina effect kama EXCESS CHARGES (gharama ya zidio) kwenye mishahara inayozidi 720,000/= itaendelea kuwa 30%.

Kama Rais angepunguza Excess charges angalau zikafika 10% kutoka 30% ziliko sasa hivi, ingekua na maana kubwa sana kuliko kupunguza PAYE.

Kwa kifupi ni kuwa punguzo la PAYE litawanufaisha zaidi wenye mishahara chini ya 720,000/= lakini kwa wanaolipwa zaidi ya hapo hakuna benefit ya maana. Hata hao wanaolipwa bellow 720,000/= bado watanufaika kidogo sana.

Nimeona nitoe ufafanuzi huu kwa sababu baadhi ya watu wameanza kumsifu Rais kwa punguzo hili la PAYE. Hadi wabunge wa upinzani nao wamebebwa na mkumbo huu na kuanza kuimba nyimbo na mapambio. Labda kwa sababu wabunge hawalipi kodi ndio maana hawajui sisi watumishi tunaathirika vipi.

Ukiona Mbunge yeyote anashangilia punguzo hili elewa tu kwamba anapenda namba lakini hajui hesabu. Kwahiyo jitahidi kumkumbusha hesabu kwa kutumia kanuni nilizozieleza hapo juu. Kupunguza PAYE wakati gharama za zidio ziko palepale ni kiini macho tu.

Yani Rais JPM alichofanya ni kutulazimisha tukatae ongezeko la mshahara. Maana kila ukiongezewa mshahara Serikali inakula 30% ya ongezeko hilo.

NB: Kuna watu wanaweza kuhoji mbona wapinzani waliomba PAYE ipunguzwe? Ni kweli tuliomba PAYE ipunguzwe tangu mwaka 2011 atleast isome single digit. Lakini single digit in both PAYE and Excess charges. Yani kama PAYE ni 09% basi na excess charges ziwe 09% pia. Sio kupunguza PAYE peke yake wakati excess charges zimebaki paleale. Na hizo ndizo zinazoumiza.

Kwa mfano wa huyo jamaa hapo juu ingekua excess charges zimepunguzwa angekatwa almost laki 3 kwenye mshahara wake. Lakini kwa punguzo hili la JPM bado ataendelea kukatwa laki 8 na ushee. Sasa hapa kuna punguzo gani?

Waambieni wabunge wenu wanaoshangilia punguzo la PAYE kuwa kazi bado. Wakomae ili gharama ya zidio (excess charges) ipungue kutoka 30% iliyopo sasa hivi hadi angalau 10%. Hapo ndio tutawaelewa. Otherwise wafunge midomo yao maana wanashanglia jambo wasilolijua.

Sio wa CCM sio wa UKAWA wote wako partial informed. Plz tell them to fight ili gharama ya zidio (exces charges) ipungue, otherwise let them shutup tuendelee kuumia kama tulivyozoea.

Sioni fahari yoyote Mbunge wa UKAWA au wa CCM kufurahia PAYE kupunguzwa wakati binafsi nimepunguziwa kiasi kisichozidi 14,000/= ambayo suruali moja ya "Jeans".

Nimeamua kusema hivi maana naona wabunge wengi wa UKAWA wanacheza ngoma ya Magufuli. Wanaanza kujitapa mara Upinzani tulishauri jambo hili tangu mwaka 2011,wengine wanapiga picha hadi hotuba ya kambi ya upinzani iliyozungumzia jambo hilo. Waambieni wakae kimya na wasiendelee kuongea vitu wasivyovijua.

Sina nafuu yoyote niliyopewa kwa kupunguziwa 02% kwenye PAYE wakati excess charges ni 30%. Ningewaona wabunge ni wa maana zaidi kama wangemshawishi Rais apunguze vyote viwe 09% sio kushangilia wakati watumishi tunaendelea kuumia.

Mwambie mbunge wako akae kimya.

Malisa GJ.!

Watanzania weshaumia sana toka huko nyuma, angalau bia tano sasa zinapatikana. Hata hivyo 2020 sio mbali ngoja iingie serikali ya watu maana hii itatoka tu madarakani kwani itakuwa imeshaharibu sana.Kwa nini adui yako akikosea katika uwanja wa vita umwambie? mwache aendelee kukosea wewe umuue kirahisi. Kelele zote za nini kumwambia amekosea wakati wewe shida yako ni kummaliza?
 
  1. NSSF- 10%
  2. NHIF=3%
  3. HESLB=8%
  4. vYAMA VYA WAFANYAKAZI=3%
  5. PAYE IN EXCESS=23%
Jumla ya makato yote yanakaribia 50% ya mshahara wa mfanyakazi..
 
kwa elimu yake ya hapa na pale sina hakika kama mbunge wangu kubenea analijua hili ulilolizungumzia.
 
Wanasiasa na usanii wa maisha kwa waliokupa kura zao ili uboronge na kuchoronga mishahara yao.
Ndugu zangu wahehe wanaita hii kitu "lutitu" yaani unanunua gunia zima la viazi ukiiomba lutitu unapewa kiazi kimoja. Ni bora angutuacha tu bila kututangazia eti mishahara yetu midogo inamuuma wakati sio.
 
Watanzania weshaumia sana toka huko nyuma, angalau bia tano sasa zinapatikana. Hata hivyo 2020 sio mbali ngoja iingie serikali ya watu maana hii itatoka tu madarakani kwani itakuwa imeshaharibu sana.Kwa nini adui yako akikosea katika uwanja wa vita umwambie? mwache aendelee kukosea wewe umuue kirahisi. Kelele zote za nini kumwambia amekosea wakati wewe shida yako ni kummaliza?
Tatizo maumivu mengi ...wanapata walala hoi...
 
Ukishazoea maumivu ndio yanakuwa maisha. Mbwa kulala nje ndio maisha yake. Halafu kwa nini utake wapate nafuu, wacha wapate shida ili ukija na unafuu wakuone wewe ndio mwokozi na wapate kuona tofauti. Raha haina maana kama shida zisingekuwepo au unasemaje mtani wangu Mndorwe?
 
Acha wivu wa kike,Malisa ana akili mingi,huwezi hata kuthubutu kujibu hoja yake bali unakuja na kelele tupu!Hayo aliyoyasema ni kweli au si kweli au hujui kilichozungumzwa?
Malisa ana akili nyingi !!! Kama unamfahamu kitambo na kama una uwezo wa kupima kiasi cha akili utakuwa uko sahihi lakini si kwa arithmetics hizi za PAYE. Ni sawa na kauli iliyowahi kutolewa na Mh. Sofia Simba juu ya Lowasa mbele ya bunge alipotamka "Lowasa ni mwanaume"
 
Mkuu sasa nyama kilo 3 yote ya nini????
[emoji12] [emoji12]
 
Ukishazoea maumivu ndio yanakuwa maisha. Mbwa kulala nje ndio maisha yake. Halafu kwa nini utake wapate nafuu, wacha wapate shida ili ukija na unafuu wakuone wewe ndio mwokozi na wapate kuona tofauti. Raha haina maana kama shida zisingekuwepo au unasemaje mtani wangu Mndorwe?
Mtani inaumiza....hiz kod....nilishawahi fanya kaz Hapa A2Z Arusha ,najua uchungu wa kodi...unalipwa 80000 ila waondoka ,na 40000....her sasa mm ni machinga.......ila inauma sanaa......nadhani tukibana matumizi ,na tukiwapunguzia mishahara walio juu...tuwajali hawawanyonge ,

Back
Top Bottom