jd41
JF-Expert Member
- Aug 23, 2015
- 3,756
- 4,842
Wanabodi salaam!.
Naomba niende moja kwa moja kwenye mada yangu ambayo imekuja kwa mtindo wa swali. Hii ni kutokana na uungwaji mkono wa Mbowe kwa wajumbe wengi wa mkutano mkuu wa CHADEMA kwa kupata ushindi mzito, kweli Mwambe hakuifahamu nguvu ya mshindani wake mkuu?, au aliifahamu ila akaamua kujitumbukiza huko makusudi ili akishindwa apate sababu ya kuondokea?.
Pia, kauli iliyowahi kutolewa na mwenyekiti wa CCM kumkaribisha Mwambe arudi nyumbani, naona kama Mwambe aliamua kutafuta sababu ya 'kijanja' zaidi
kuondokea CHADEMA na isionekane ni kwasababu ya ushawishi aliopewa na mwenyekiti wa CCM, ili kuficha ukweli uliowazi kwamba ni salama zaidi kwake kugombea jimbo lake kupitia tiketi ya CCM alipokaribishwa na mwenyekiti wake kuliko kubakia CHADEMA ambapo nafasi ya ushindi ni finyu kutokana na tuliyoyashuhudia kwenye chaguzi ndogo zilizopita miaka ya karibuni.
Kutokana na taarifa zilizopo, Mwambe hakuwepo ukumbini wakati wa kumtangaza mshindi, licha kuitwa mara tatu lakini hakuweza kuonekana. Hii inaweza kuwa ni kwasababu alishapenyezewa matokeo, lakini kiungwana kwasababu aliamua kwa utashi wake kugombea, bila kushawishiwa na yeyote, nilitegemea angekuwepo mpaka mwisho wa uchaguzi kutangazwa matokeo ili nae kama mshindani aweze kutoa salamu zake. Hii inadhihirisha kumbe Mwambe hana ujasiri huo aliokuwa anajinasibu nao wakati wa kampeni, kama angepewa chama angeweza vipi kukiongoza, kama jambo dogo tu la kuvumilia kutangazwa matokeo lilimshinda?!
Sent using Jamii Forums mobile app