Luninga jana usiku na magazeti ya leo yametoa picha za Polisi walioua majambazi pale magomeni majuzi wakipongezwa hadharani.
Suala zima la kupongeza hao Polisi sio baya lakini nahofia pale jambo hilo linapofanyika hadharani tena kwa sherehe. Tujue kuwa jambo la kuua binadamu sio jema hata kama anayeuawa ni jambazi. Nazungumzia lile tendo la kuua binadamu. Sio suala la kutambia. Kama jeshi la Polisi limeua majambazi, basi, walioua wanatakiwa kutojulikana kabisa. Kama ni kupongezwa, ingetangazwa tu kuwa wamepongezwa lakini bila kujulikana kwa wananchi ni nani aliyepongezwa.
Tukumbuke kuwa hao waliouawa wana familia zao ambazo zinaweza kulipiza kisasi au kundi lile la majambazi linaweza kuwa na mtandao mkubwa zaidi ya wale waliouawa hivyo likalipiza kisasi baada ya kuwatambua wale waliohusika na mauaji ya wenzao.
Kwa wenzetu huwa naona Polisi wakiwa wamevaa "ninja" ili wasitambulike kirahisi.
Kwa wanajeshi (JWTZ), sikuwahi kusikia mwanajeshi akitamba kuwa wakati wa vita aliua watu kadhaa. Ndio maadaili yao. Kuua sio kuzuri hata kama ni lazima kufanya hivyo.
Tusiwaonyeshe vijana wetu hadharani pale wanapokuwa wametumia ujasiri wao kulinda usalama wa raia. Ndugu zao, majirani, Polisi wenzao, hata wakienda baa sasa wanajulikana "yule aliua jambazi".
Suala la kuua majambazi wakati wa mwalimu lilikuwa nadra sana kulisikia katika vyombo vya habari. Sina uhakika kuwa polisi walikuwa hawaui ila ninachojua ni kuwa sijawahi kusikia. Inawezekana na Technology ya wakati huo hasa katika umiliki wa silaha haramu. Ila kitendo cha kuwa-puplicize hawa askari kwa kufanya kazi ambayo waliyo ajiriwa kuifanya kuna madhara mengi sana kwa Taifa na Usalama wa Raia kuliko faida.
1. Ni kweli kabisa kuwa polisi ni lazima wapewe motisha, na motisha pekee ungekuwa kutoka kwa mwajiri wake kwa kumuongezea kipato cha kila mwezi (walipwe vizuri hasa baada ya kujua kuwa wapo katika risk ya kupoteza maisha kwa ajili ya usalama wa raia wema- high risk-high return)na kumuendeleza katika mbinu za kujihami na kuzuia uhalifu kuliko hivi vimichango vya watu wachache kwa mkupuo.
2. Kitendo cha kuwaonesha sura zao kuwa hawa ndiyo walioua binadamu wenzao(regardless ni majambazi, au vibaka) ni ishara tosha kwa jamii kuwa hawa ni wakatili na ni watu wa kuogopwa kwani wanaweza kukuchomoa nafsi wakati wowote, kitu kitakachowanyima social love from public
3. Kitendo cha kuwapongeza hawa kwa kuua watuhumiwa wa uhalifu(Ninasema ni watuhumia kwani under rule of law they are not guilty until convicted by court of law) kitachochea "dark justice" kuwa mtu hata akitaka kujilinda kutokana na uhalifu kama ana silaha halali halafu akabadilishiwa kibao na wahalifu kuwa jambazi basi ni hukumu yake ya kifo toka polisi ambao watakuwa na shauku ya kuua ili wapongezwe.
4. Kwa kuwatambulisha polisi hawa kwa jamii ni wazi kabisa usalama wao umekuwa-impaired, kwani kama mdau alivyosema, hawa majambazi ni miongozi mwa watanzania wenzetu tunaoishi nao mtaani(sio aliens) hivyo ndugu, jamaa au majambazi wenzao wanaweza kujaribu kulipiza kisasi kwa wahusika
5. Mwisho, hili linaweza kuwa "demotivating factor" kwa Polisi wengine mikoani wanaofanya kazi za hatari zaidi, ila tu kwa kuwa hawapo Dar kwenye Publicity hawawezi kupongezwa na hivyo kupunguza ari.
Pongezi ni muhimu kuzitoa hasa kwa watu wanaotimiza wajibu wao kama walivyofanya hawa, lakini huu utamaduni wa michango kwa ajili publicity ni hatari sana na haufai kwanza unadhalilisha serikali na jeshi zima la polisi kama chombo cha dola. Pongezi pekee ni kwa serikali kufanya yafuatayo
1. Kuwapatia makazi mazuri na yenye hadhi si vi baracks ambavyo tokea vijengwa havijapigwa rangi, vyoo vimeziba, maji hayatoki, sewerage system zimeziba.
2. Kuhakikisha kuwa Polisi wanalipwa vizuri tena ikibidi hata 40% tu ya wabunge ambao hawana risk yoyote ya kupoteza maisha.
3. Kuwapatia vifaa vya kisasa kabisa ambavyo vitaongeza survivability yao na success ya kukamata majambazi bila kuuwa hata kama wanasilaha za moto.
4. Kuwakatia bima endapo mtu anapoteza kiungo kazini basi ajue kuwa hatosota katika siku zake za maisha zilizobaki, badala ya kulipwa milioni tatu na kustaafishwa.