Mwalionaje hili la kupongeza hadharani Polisi walioua? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwalionaje hili la kupongeza hadharani Polisi walioua?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Congo, Jan 8, 2010.

 1. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,272
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Luninga jana usiku na magazeti ya leo yametoa picha za Polisi walioua majambazi pale magomeni majuzi wakipongezwa hadharani.
  Suala zima la kupongeza hao Polisi sio baya lakini nahofia pale jambo hilo linapofanyika hadharani tena kwa sherehe. Tujue kuwa jambo la kuua binadamu sio jema hata kama anayeuawa ni jambazi. Nazungumzia lile tendo la kuua binadamu. Sio suala la kutambia. Kama jeshi la Polisi limeua majambazi, basi, walioua wanatakiwa kutojulikana kabisa. Kama ni kupongezwa, ingetangazwa tu kuwa wamepongezwa lakini bila kujulikana kwa wananchi ni nani aliyepongezwa.
  Tukumbuke kuwa hao waliouawa wana familia zao ambazo zinaweza kulipiza kisasi au kundi lile la majambazi linaweza kuwa na mtandao mkubwa zaidi ya wale waliouawa hivyo likalipiza kisasi baada ya kuwatambua wale waliohusika na mauaji ya wenzao.
  Kwa wenzetu huwa naona Polisi wakiwa wamevaa "ninja" ili wasitambulike kirahisi.
  Kwa wanajeshi (JWTZ), sikuwahi kusikia mwanajeshi akitamba kuwa wakati wa vita aliua watu kadhaa. Ndio maadaili yao. Kuua sio kuzuri hata kama ni lazima kufanya hivyo.
  Tusiwaonyeshe vijana wetu hadharani pale wanapokuwa wametumia ujasiri wao kulinda usalama wa raia. Ndugu zao, majirani, Polisi wenzao, hata wakienda baa sasa wanajulikana "yule aliua jambazi".
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  mie naona sawa tu je hayo majambazi yangewataimu wao na kuwaua ingekuwa vip?
   
 3. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  It's good.....hata ya Zombe tuliyajua kupitia pongezi hizo hizo
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,333
  Likes Received: 22,181
  Trophy Points: 280
  Polisi wa tanzania wana leseni ya kuua.
  Hata usipokuwa jambazi wanakuunganishia tu kuwa ulikuwa jambazi na wamekufukuza toka posta hadi mbezi kwa msuguri huku mkirushiana risasi,
  wakati ukweli ni kuwa wewe ulikuwa umetoka kibaruani na polisi wamekuvizia ili wamwage damu yako.
  Mwaka jana miezi karibuni na mwishoni, mfanya biashara maarufu tundduma aliuawa na polisi kwa kusingiziwa kuwa ni jambazi.
  Baada ya kifo chake wananchi wa tunduma walifanya sana fujo hadi kikosi maalum kutoka mbeya mjini kikatumwa tunduma.
  Baada ya mazishi hamna hatua yoyote polisi waliyoichukua dhidi ya wauaji na huo ukawa ni mwisho wa mchezo.
   
 5. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Muuwaji hakubaliki, Hata awe polisi kwa kisingizio cha ujambazi. Uliye muulia ndungu yake akipata nafasi na wewe atakuuwa.
   
 6. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #6
  Jan 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Wanastahili kupandishwa na VYEO - Yule Dada angepelekwa CCP kuwa mkufunzi na wale wengine waweza kupewa u-OCD ili waweze kufanya kazi kwa uzuri zaidi

  Salute
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Jan 8, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  salute
   
 8. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #8
  Jan 8, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,272
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Soma vema ujumbe wangu, utanielewa nazungumzia nini.
   
 9. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #9
  Jan 8, 2010
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MIMI nafikiri wamewaexpose kwa majambazi.hawatakuwa salama sana kama kabla ya tukio.wangewapongeza na kuwapa pesa hizo lakini picha nyuso zao zingefunikwa
   
 10. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #10
  Jan 8, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Kamanda Kova hapa amechemsha.
  That was a stupid move kuwapongeza askari hadharani na nyuso zao kuonekana na majambazi wote nchini.
  Ukijua ujambazi utaelewa kuwa kuna mtandao wao na wakati mwingine ni nchi nzima au kimkoa, na Polisi wanalijua hili fika.
  Ni kuhatarisha maisha ya vijana wale , hasa yule dada, ingawaje na mimi nawapongeza sana kwa kuwafanyia kweli majambazi yanayo tutesa hapa nchini.
   
 11. O

  Omumura JF-Expert Member

  #11
  Jan 8, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kuuwa majambazi ni safi sana, problem ni kuwa expose kwa jamii!
   
 12. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #12
  Jan 9, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,195
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Zamani wakati nchi ilikuwa nchi kulikuwa na watu wanaitwa coroners kazi yao ilikuwa kuchunguza vifo kama hivyo. Sasa hivi hicho cheo hakipo na polisi wanafanya wanavyotaka kama ni jambazi si jambazi sio juu yao.

  Kuna haja ya kurudisha utaratibu ule wa zamani (coroners), hata kama walikuwa majambazi kweli, walitakiwa kukamatwa sio kuuwawa, kwa nini kila siku majambazi wauawe badala ya kukamatwa?????? Jamani huu sio upungufu wa utendaji kwenye jeshi letu la polisi.
   
 13. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #13
  Jan 9, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,195
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Anachemsha kila siku huyo upolisi wake ni wa kizamani sana. unategemea nini.

  Gwakisa naomba nitofautiane nawe kuwa haitakiwi kupongeza polisi kwa kuuwa. Kwa kufanya hivyo ni kuonyesha kuwa hawawezi kazi. Kazi ya polisi ni kukamata wahalifu sio kuua, ukikamata mhalifu mmoja unapata source ya information kubwa sana lakini ukiuwa jambazi unakosa important information na kuna element ya revenge. Hebu pitia magazeti uone ni mara ngapi polisi wamekamata majambazi kila siku wanajibishana na majambazi na lazima majambazi wote wafe.

  Hamuoni kuwa kuna pattern fulani ya elimination,

  Sioni sababu ya kuwapongeza polisi kwa hilo hata kama ni majambazi bado wana haki zao, mbona mafisadi wanaochota mamilioni wao wanapewa haki zao?????
   
 14. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #14
  Jan 9, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
   
 15. M

  Mende dume Member

  #15
  Jan 9, 2010
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dear FirstLady1, am missing something. sijaua kama nimekupenda wewe au ninapenda hoja zako. really i enjoy reading you, with some more guys.

  teh teh teh
   
 16. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #16
  Jan 10, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Tanzania itself is a police state, what do you expect?

  Mtu aliyejiuzulu kwa uzembe wa kuua vibibi Shinyanga kwa kushukiwa uchawi akaenda kuwa rais, unategemea nini?
   
 17. kebepa

  kebepa Senior Member

  #17
  Jan 10, 2010
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 134
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kupongezana hatukatai, kwani ni njia mojawapo ya kupeana motisha katika kazi ngumu inayowakabili ya kupambana na majambazi ambapo ukizubaa umeuawa wewe. Lakini haya wayafanye kiofisi bila kushirikisha vyombo vya habari. Kwani kuua mtu hata kama ni jambazi sio kitu ambacho kinapokelewa kwa tafsiri nzuri miongoni mwa jamii. Nikubaliane na wote wanaosema kuwa kova amechemsha!
   
 18. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #18
  Jan 10, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Suala la kuua majambazi wakati wa mwalimu lilikuwa nadra sana kulisikia katika vyombo vya habari. Sina uhakika kuwa polisi walikuwa hawaui ila ninachojua ni kuwa sijawahi kusikia. Inawezekana na Technology ya wakati huo hasa katika umiliki wa silaha haramu. Ila kitendo cha kuwa-puplicize hawa askari kwa kufanya kazi ambayo waliyo ajiriwa kuifanya kuna madhara mengi sana kwa Taifa na Usalama wa Raia kuliko faida.

  1. Ni kweli kabisa kuwa polisi ni lazima wapewe motisha, na motisha pekee ungekuwa kutoka kwa mwajiri wake kwa kumuongezea kipato cha kila mwezi (walipwe vizuri hasa baada ya kujua kuwa wapo katika risk ya kupoteza maisha kwa ajili ya usalama wa raia wema- high risk-high return)na kumuendeleza katika mbinu za kujihami na kuzuia uhalifu kuliko hivi vimichango vya watu wachache kwa mkupuo.

  2. Kitendo cha kuwaonesha sura zao kuwa hawa ndiyo walioua binadamu wenzao(regardless ni majambazi, au vibaka) ni ishara tosha kwa jamii kuwa hawa ni wakatili na ni watu wa kuogopwa kwani wanaweza kukuchomoa nafsi wakati wowote, kitu kitakachowanyima social love from public

  3. Kitendo cha kuwapongeza hawa kwa kuua watuhumiwa wa uhalifu(Ninasema ni watuhumia kwani under rule of law they are not guilty until convicted by court of law) kitachochea "dark justice" kuwa mtu hata akitaka kujilinda kutokana na uhalifu kama ana silaha halali halafu akabadilishiwa kibao na wahalifu kuwa jambazi basi ni hukumu yake ya kifo toka polisi ambao watakuwa na shauku ya kuua ili wapongezwe.

  4. Kwa kuwatambulisha polisi hawa kwa jamii ni wazi kabisa usalama wao umekuwa-impaired, kwani kama mdau alivyosema, hawa majambazi ni miongozi mwa watanzania wenzetu tunaoishi nao mtaani(sio aliens) hivyo ndugu, jamaa au majambazi wenzao wanaweza kujaribu kulipiza kisasi kwa wahusika

  5. Mwisho, hili linaweza kuwa "demotivating factor" kwa Polisi wengine mikoani wanaofanya kazi za hatari zaidi, ila tu kwa kuwa hawapo Dar kwenye Publicity hawawezi kupongezwa na hivyo kupunguza ari.

  Pongezi ni muhimu kuzitoa hasa kwa watu wanaotimiza wajibu wao kama walivyofanya hawa, lakini huu utamaduni wa michango kwa ajili publicity ni hatari sana na haufai kwanza unadhalilisha serikali na jeshi zima la polisi kama chombo cha dola. Pongezi pekee ni kwa serikali kufanya yafuatayo

  1. Kuwapatia makazi mazuri na yenye hadhi si vi baracks ambavyo tokea vijengwa havijapigwa rangi, vyoo vimeziba, maji hayatoki, sewerage system zimeziba.

  2. Kuhakikisha kuwa Polisi wanalipwa vizuri tena ikibidi hata 40% tu ya wabunge ambao hawana risk yoyote ya kupoteza maisha.

  3. Kuwapatia vifaa vya kisasa kabisa ambavyo vitaongeza survivability yao na success ya kukamata majambazi bila kuuwa hata kama wanasilaha za moto.

  4. Kuwakatia bima endapo mtu anapoteza kiungo kazini basi ajue kuwa hatosota katika siku zake za maisha zilizobaki, badala ya kulipwa milioni tatu na kustaafishwa.
   
 19. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #19
  Jan 10, 2010
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Polisi kuua majambazi maana yake ni kushindwa kufanya kazi zao kwa uimara na ustadi.. inaonekana wanajichukulia sheria mikononi... kwani wao ndio mahakama iliyoamuru kwamba majambazi lazima yapatikane dead or alive...

  Nani aliwapa kibali cha kuua majambazi hao jeshi la polisi.. inafaa wayakimbize hadi na helikopta maana najua wanazo na wakifanya hivyo majambazi yatafikiria mara mbili mbilikwenda kuiba .. hii ya kuyaua si nzuri maana kwanza polisi wanapoteza inteligence juu ya network nzima ya mtandao wa kiharifu... halafu katika utawala wa sheria... everyone is pressumed innocent until proved othewise... yawekana kabisa kwamba hao waliouwawa hawakufanya ujambazi kwa hiari yao.. labda walilazimishwa na kwa precedent iliyowekwa na mkuu Raisi na kwamba kama ukiiba na kurudisha mali basi hutakiwi kufikishwa mahakani , sasa ya nini kuwauwa majambazi... inafaa yakamatwe na yaanze kutajana na sio kuyaua..

  Au labda pia mkono wa mabosi wa polisi umo maana kama ukiyakama na yakaanza kuwataja mapolisi wanaoshirikiana nao.. itakuwa soo nyingine.. hivyo ni vema yauwawe tu...
  Ndio yale yale ya kombe na Chigumbi..

  Pili.. nafikiri hata akina magufuri pia hawakufikiria vizuri maana utawapongezaje polisi kwa kuua? polisi kazi yao ni kutunza usalama wa raia na hao pia waliouwawa ni raia.. halafu tutajuaje kama kweli ni majambazi bila uchunguzi huru? ni mambo ya kitoto sana kuwapongeza kwani kukamata majambazi au wahalifu ndio kazo hasa ya polisi vinginevyo inatoa picha ya kwamba huwa hafanyi kazi na ikitokea wamefanya ndio huko kupongezana!!
   
 20. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #20
  Jan 10, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Tanzania hatuna "rule of law"

  Hata wenzetu hapa hawaelewi "rule of law" ni nini.

  Kova natumaini -natumaini, get it?- anaelewa "rule of law" ni nini. Lakini naona anaona kama ni kitu fulani abstract na academic ambacho hakina uhusiano na the immediate efforts to restore law and order and cultivate a positive direction in Tanzanian criminology.

  Worse still anajua Tanzania hamna press, middle class wala civil society ya ku-condemn hizi authoritarian if not Orwellian moves.I mean ua majambazi wote, lakini wape fair trial kwanza.Au hata kama unawaua in the heat of combat against crime, usipongeze polisi wazi hivi, kwa sababu kuua katika heat of battle against crime however necessary, hakuna baraka za a free trial.Kwa hiyo kama kupongezana basi angalau mfanye huko Police officers mess, msituletee mess hadharani.

  Msifanye kama kila mtu hajui "rule of law" ni nini. Hii tabia kesho itafanya Kamanda Kova atume vijana wake waende kuua wapinzani wake wa kisiasa/kibiashara na keshokutwa kuwasifia kwa kazi nzuri.
   
Loading...