#COVID19 Mwalimu sichomwi chanjo ng'o na wakibadilisha utaratibu kuwa lazima basi nitakuwa tayari kuacha hata kazi

hata mimi

JF-Expert Member
Oct 17, 2017
1,356
1,437
Kuna watu wanapenda sana sifa kupitia wenzao sasa nasema rasmi hapa wazi kabisa sitakubali kuchomwa sindano ng'o (maana mmesema ni hiari)

Na hata kama mkibadili gia angani (na kufanya ni lazima kwa makundi fulani- ambapo kivyovyote walimu wataingia) basi nitakuwa radhi kuacha kazi nikafanye mambo mengine tu mtaani

Mmezoea kutupeleka peleka sana ila katika hili binafsi sikubali

Kwa ambao nimewaacha hawajanielewa hapo juu ni kwamba viongozi hawa wa wilayani huku muda mwingine wanatutesa sana na wanapaa sana majina kupitia migongo yetu watumishi

Tunachangishwa elfu tano tano za mwenge kila mwaka tena kimikwara kwelikweli... ila chaajabu mnaambiwa mchango huo ni wa hiari kuonesha uzalendo! Sasa uzalendo gani wa kulazimishwa sijui (Yale yale ya kodi ya uzalendo)

Mnapotekeleza kwa wingi jambo husika basi sifa kwa halmashauri na DC eti basi!
 
Nakuunga mkono ndugu yangu, fanya lile ambalo moyo wako itakua na amani nalo.

Vyovyote vile watakavyosema lakini hizi chanjo hizi zaidi ya mwenyezi Mungu kutusaidia hakika usalama wake Ni mdogo mno haswa kwa kizazi kitakachokutwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usichanjwe kabisa si lazima sababu wewe huitaji kwenda nje ya Tanzania. Huna watoto wala wajukuu nje, huna mpango wa kwenda Kariakoo kwenye watu wengi, hupandi daladala wala bajaj ya kushare.

Wewe umebarikiwa huendi kanisani na ukienda una barakoa na unakaa mita moja kati yako na wenzio. Mwenzio au mme wako hakai kwenye kadamnasi.

Sisi wahanga wa huu ugonjwa tuliolala miezi miwili tukanusurika, tunawajibika kujitenga na mikusanyiko na ndE
Usichomwe na usiende ila utaulizana swali na mwendazake na RC wa Kili.
 
Hawatakulazimisha....

Kapuku Mimi ninaisubiri chanjo kwa hamu kubwa....

Ikifika zamu yetu wa hali ya chini ,nitakuwa wa MWANZOMWANZO kuchomwa in shaa Allah!

#SayansiSiSiasa
#NchiKwanza
#KaziIendelee
#SiasaNiSayansi
Eti kuna somo chuo kikuu linaitwa Political Science?
 
Usichanjwe kabisa si lazima sababu wewe huitaji kwenda nje ya Tanzania. Huna watoto wala wajukuu nje, huna mpango wa kwenda Kariakoo kwenye watu wengi, hupandi daladala wala bajaj ya kushare.

Wewe umebarikiwa huendi kanisani na ukienda una barakoa na unakaa mita moja kati yako na wenzio. Mwenzio au mme wako hakai kwenye kadamnasi.

Sisi wahanga wa huu ugonjwa tuliolala miezi miwili tukanusurika, tunawajibika kujitenga na mikusanyiko na ndE
Usichomwe na usiende ila utaulizana swali na mwendazake na RC wa Kili.
Mkuu mimi nipo njia panda maana kuna waliochanjwa wamepata huo ugonjwa na wengine wamelazwa au kufa kabisa.

Nasubiri dakika ya mwisho nafsi yangu itaniambiaje, nichanjwe au nisichanjwe?
 
Kuna watu wanapenda sana sifa kupitia wenzao sasa nasema rasmi hapa wazi kabisa sitakubali kuchomwa sindano ng'o (maana mmesema ni hiari)

Na hata kama mkibadili gia angani (na kufanya ni lazima kwa makundi fulani- ambapo kivyovyote walimu wataingia) basi nitakuwa radhi kuacha kazi nikafanye mambo mengine tu mtaani

Mmezoea kutupeleka peleka sana ila katika hili binafsi sikubali

Kwa ambao nimewaacha hawajanielewa hapo juu ni kwamba viongozi hawa wa wilayani huku muda mwingine wanatutesa sana na wanapaa sana majina kupitia migongo yetu watumishi

Tunachangishwa elfu tano tano za mwenge kila mwaka tena kimikwara kwelikweli... ila chaajabu mnaambiwa mchango huo ni wa hiari kuonesha uzalendo! Sasa uzalendo gani wa kulazimishwa sijui (Yale yale ya kodi ya uzalendo)

Mnapotekeleza kwa wingi jambo husika basi sifa kwa halmashauri na DC eti basi!
point sana mkuu Mungu atusaidie
 
Usichanjwe kabisa si lazima sababu wewe huitaji kwenda nje ya Tanzania. Huna watoto wala wajukuu nje, huna mpango wa kwenda Kariakoo kwenye watu wengi, hupandi daladala wala bajaj ya kushare.

Wewe umebarikiwa huendi kanisani na ukienda una barakoa na unakaa mita moja kati yako na wenzio. Mwenzio au mme wako hakai kwenye kadamnasi.

Sisi wahanga wa huu ugonjwa tuliolala miezi miwili tukanusurika, tunawajibika kujitenga na mikusanyiko na ndE
Usichomwe na usiende ila utaulizana swali na mwendazake na RC wa Kili.
Tusitishane mkuu,
Kwanza kaugonjwa kenyewe kadogo😀

Anyway tangu mwaka jana August nipo kkoo mpaka hii leo, mazingira ya kazi yangu ni rahisi sana kupata maambukizi ila kuhusu hii chanjo nitakua wa mwisho kupata
Narudia tena nitakua wa mwisho

nasubiri nione watakaoanza watapata madhara gani kwanza, wakianza kuwashwa nitawakuna kisha navunga

ila nikiona inasaidia ndo ntakua wa mwisho mwisho
 
Mkuu mimi nipo njia panda maana kuna waliochanjwa wamepata huo ugonjwa na wengine wamelazwa au kufa kabisa.

Nasubiri dakika ya mwisho nafsi yangu itaniambiaje, nichanjwe au nisichanjwe?
Nimechanjwa nina wiki sijapata homa wala kifua kuuma.

Imani na maneno ya kulishwa yanatutesa wabongo. Ndo maana tukiaminishwa kitu tunachukulia ndo sala yetu. Use your commonsense do not rely on one said this one said that. ndo maana tunapukutika. Mwanakwenda zake alisema ni mafua kama menginei na mama wa Kili alionya kuhusu huu ugonjwa ila yeye kaondoka akijua kilichomchukua.
 
Back
Top Bottom