Mwalimu Nyerere Foundation ipo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwalimu Nyerere Foundation ipo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzawa Halisi, Aug 15, 2009.

 1. M

  Mzawa Halisi JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 500
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Miaka michache kabla ya kifo cha Nyerere, ilianzishwa taasisi iliyoitwa Mwalimu Nyerere Foundation (MNF), taasisi hii iliendelea hata baada ya kifo cha mwalimu ikiwa chini ya uenyekiti wa Salim Ahmed Salim, na mtendaji mkuu Joseph Butiku. Kwa taarifa ambazo nimeshindwa kuzithibitsha, ni kuwa taasisi hii iko chali kiuendashaji hata ilishindwa kulipa wafanyakazi wake mishahara. Na kwa kiasi kikubwa kuanguka kwa taasisi hii kumechangiwa na uzembe na kiburi cha uongozi wa juu ukiongozwa na Bw. Butiku. Inasemekana kuwa wahisani ikiwa ni pamoja na GOT waliokuwa wanaisaidia taasisi hii walishindwa kuendelea kutoa misaada baada ya viongozi wa MNF kuanza kutumia misaada hiyo nje ya malengo yaliyokusudiwa.

  Kama kuna member ana taarifa za uhakika juu ya majaaliwa ya taasisi hii naomba anifahamishe.
   
 2. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2009
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mheshiwa Mzawa Halisi,

  Majibu ya swali lako ni kwamba Mwalimu Nyerere Foundation ingalipo; bali kutokana na uongozi wake, hususan Salim Ahmed Salim na Joseph Butiku, kuwa wakweli, calling a spade a spade, GOT inasita kutekeleza ahadi zake za ruzuku. Uongozi wa MNF ni wazalendo wa kweli, jasiri na waadilifu, na hawawezi ku-adopt mbinu za kifisadi ili kuendeleza taasisi inayomuenzi Muasisi wa Taifa letu. Hata Muasisi mwenyewe angekuwa hai, angepinga ufisadi unaolenga kukipatia mapato chombo hicho.

  Ni matarajio ya wale wanaopenda maendeleo thabiti ya nchi yetu kwamba, punde si punde, mabadiliko ya kweli yaletwa na Watanzania wa kizazi kipya, wakifuata nyayo za Salim na Butiku, ili taasisi hii ya kihistoria kwa taifa isiendelee kulegalega.

  Mungu Ibariki Tanzania.
   
  Last edited: Aug 16, 2009
 3. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Si Butiku aondolowe? Nini anang'ang'ania?
   
 4. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  MNF ipo na inaendeshwa kama taasisi nyingine sizizo za kiserikali. Kwa kawaida wanakuwa na wafanyakazi kunapokuwa na miradi inayoendelea na kila inapokamilika wale wote waliokuwa wakifanyi project hiyo huondoka.

  Miradi yao ya hivi karibuni ni usuluhishi wa 'MUAFAKA' wa Zanzibar, hapo nyuma walishughalika sana na harakati za kupatanisha waRundi.
   
 5. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mbona naona kama kuna jengo jipya linajengwa pale?
   
 6. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Mkuu MH, hii ni NGO sio chama cha siasa.
   
 7. Companero

  Companero Platinum Member

  #7
  Aug 16, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
 8. Companero

  Companero Platinum Member

  #8
  Aug 16, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
 9. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #9
  Aug 16, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Juzi juzi wamesaini mktaba wa ujenzi wa jengo refu Dar, nadhjani litakuwa ndicho kitegauchumi chao
   
 10. Z

  Zanaki JF-Expert Member

  #10
  Aug 17, 2009
  Joined: Sep 1, 2006
  Messages: 544
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mambo mengi MNF yanakwama kwa sababu ya Mkurugenzi wao. Alitakiwa astaafu toka mwaka jana au mwaka juzi lkini bado kang'ang'ania tu kile kiti. Ni kweli hawana pesa hata za kulipa wafanyakazi.
   
 11. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #11
  Aug 17, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Paul Kagame na Museveni wameahidi kuhakikisha kuwa Nyerere Foundation inasalimika. Butiku is over 70 and he should not be an issue. And so is Salim. Kunatafutwa uongozi mpya utakaoweza kuendeleza pale Butiku na Salim walipofikia. Jengo la Foundation likimalizika litakuwa mradi mzuri wa kuiendesha Foundation sustainably.
   
Loading...