Mwalimu mpya majanga!

Mwalimu mpya majanga!

mkolaj

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2014
Posts
3,023
Reaction score
1,092
Ni katika shule ya msingi limbende iliyopo halmashauri ya mtwara vijijini mkoa wa mtwara tumempata mwalimu mpya wa daraja la tatu A na tangu alipoti hapa kituo cha kazi hadi leo ametimiza wiki moja hivi, lakini cha kushangaza huyu mwalimu pamoja na ugeni wake katika kazi na hata katika jamii amekua akifanya mambo yake kanakwamba ana muda mrefu hapa, anakunywa pombe ovyo ovyo, anavuta bangi bila kujificha na mbaya zaidi akienda kunywa huchelewa kurudi nyumbani, huwa anarudi usiku wa saa tano hadi saa sita na huwa anatugongea ili tumfungulie na hufanya hivyo, na tumejaribu kuongea nae sisi walimu wenzake ili aache hiyo tabia lakini haonyeshi kubadilika. Naomba ushauri wenu wana jf kuhusu hili tatizo. Huyu mwalimu anatoka mkoa wa mara wilaya ya musoma. Ushauri tafadhari....
 
mwache bhana,mtafutie chumba chake mana wanawake wa huku watamtaka sana huyu,wenyewe tunawaita wa maj chumvi watamchanganya hela zote atazmalizia huko!karbu mtwara mjin mkuu
 
Kwa jina lingine mleta mada naweza kukuita mbea,
Unajua taarifa ulizotoa zinamuhusu mtu mwenye dhamana ktk jamii?
Lengo lango ni kumdhalilisha.
Ni vyema ungetueleza mapungufu yako wewe ulionayo kwanza then utueleze ya mwenzako. AU wewe uko perfect kwa kila jambo?
TAFAKARI
 
Privacy iheshimiwe, angekuwa anatembea na wanafuni sawa ungeripoti lakini masuala binafsi kusema kweli hayakuhusu, kama anachofanya mmehisi ni kibaya mmemshauri hajawaelewa, ulipaswa kukaa kimya dunia ni darasa tosha.

Kitu kingine fanyeni mpango kila mtu awe na nyumba yake, mnakubalije kuishi HOSTELI?
 
Ivi we mleta mada ni wa kike au wakiume?mana hata siku hizi wanawake wameacha umbea.
 
hayo n mambo ya mtu binafsi hukupaswa kumvunjia heshima kiasi.hichi, zaidi wewe uliye post ndo kituko.
 
Kwa jina lingine mleta mada naweza kukuita mbea,
Unajua taarifa ulizotoa zinamuhusu mtu mwenye dhamana ktk jamii?
Lengo lango ni kumdhalilisha.
Ni vyema ungetueleza mapungufu yako wewe ulionayo kwanza then utueleze ya mwenzako. AU wewe uko perfect kwa kila jambo?
TAFAKARI
HAPO HAJAMDHALILISHA,ametoa uhalisia wa huyo mwalimu aliyekosa maadili..na ndiye anaishi nae katika mazingira hayo..sasa ukisema mtoa taarifa ni mbea kwa styli hii unakosea!
 
Hata mimi namuona ni mbea tu kwani alienda kumuomba pesa ya pombe au bangi?
 
Ulevi,bangi na tabia mbaya ndiyo syllabus za vitendo zilizoko vyuoni siku hizi.
 
Hata mimi namuona ni mbea tu kwani alienda kumuomba pesa ya pombe au bangi?
kwa maana hiyo unapoa taarifa au hata tu kuomba ushauri kwa jambo kama hilo ni mbeya..basi kama ni ivo humu jf wengi wambea!!!
 
kunywa pombe ovyo ovyo ndo kivipi??
yaan manake time yote upo nduki tu.. ganja plus tungi {inawezekana gongo} maana ashasema nmwalimu mwnyw wa kuuule kwa kina arrrroooh ..na sipati picha class!!
 
kwa maana hiyo unapoa taarifa au hata tu kuomba ushauri kwa jambo kama hilo ni mbeya..basi kama ni ivo humu jf wengi wambea!!!

Jamii tunayoishi imejaa kila aina ya mambo sio kila jambo liletwe ktk forums.Ina maana siku mkeo akipika maharage yasipoiva utaleta huku tukushauri nini?
 
taarifa yenyewe ni public intrest inayohusu elimu wanayopewa watoto wetu na hawa walimu wasiojitambua..sasa kama unata ziletwe stori za kina wema sijui kanunua pafyum ya milionon...hizo ndo cyo ishu kuzileta..
 
Back
Top Bottom