Mwalimu kizimbani kwa kutamani mwanafunzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwalimu kizimbani kwa kutamani mwanafunzi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Sep 18, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  MWALIMU Ally Msanga [39] wa Shule ya Msingi Makumbusho ya jijini Dar es Salaam, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na shitaka la kutaka kumuingilia kimwili mwanafunzi wake wa miaka 14

  Mtuhumiwa huyo alipandishwa mahakamani jana Mbele ya Hakimu Susan Kihawa, na upande wa mashitaka ulikuwa ukiongozwa na Mwendesha Mashtaka, Mohamed Kilongo.

  Kilongo alidai kuwa, mshitakiwa alitenda kosa hilo kati ya Mei na Septemba mwaka huu katika eneo la shule hiyo.

  Kilongo alidai kuwa, mwalimu huyo alikuwa akitaka kumuingilia wmanwafunzi wake wa darasa la sita [jina linahifadhiwa] na alikamatwa wakati akitaka kumuingilia kimwili mwanafunzi huyo.

  Alidai kuwa, Mei mwaka huu, mwalimu huyo alimuita mwanafuzni huyo ofisini kwa lengo la kumfanyia masahihisho kwa maswali ambayo aliyakosa kati ambayo aliyompa mwnafunzi huyo pekee na badala yake mwanafunzi huyo alipongia alianza kumshika sehemu za mwili ikiwemo na sehemu za siri.

  Kilongo aliendelea kudai kuwa, Septemba mwaka huu, mshtakiwa huyo alitenda tena kosa kama hilo alimuita tena mwanafunzi huyo na kumvua sketi yake bila ridhaa kwa lengo la kumuingilia kimwili na kuonekana.

  HAta hivyo Mshtakiwa alikana mashitaka hayo, na alirudishwa rumande kwa kukosa dhamana, atarudishwa tena mahakamani hapo Septemba 30, mwaka huu, kwa kesi hiyo kutajwa

  chanzo: NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
   
Loading...