Mwalimu Julius Nyerere alikuwa nabii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwalimu Julius Nyerere alikuwa nabii

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Magobe T, Oct 15, 2011.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Neno nabii linatoka na neno la Kiebrania nābî au prophētēs (kwa Kiingereza prophet) mtu mwenye maono (visionary, seer) na mwenye ujumbe wenye mantiki (rational speech) na unaogusa jamii kwa ujumla wake hasa kwa kutoa ujumbe wenye usasa (God’s now message) kwa watu husika.Mwalimu Julius Nyerere ni mmoja wa viongozi wachache duniani, ambaye anakidhi vigezo vya kuwa nabii kwa taifa letu na Afrika nzima kutokana na mchango wa maisha yake binafsi (uadilifu wake) na uongozi wake uliotukuka (kuonesha njia).

  Alitumia elimu yake kwa manufaa ya wote – alikuwa akiwafundisha wakulima namna ya kutayarisha mashamba
  yao kutokana na majira ya mwaka maana alijua jiografia ya nchi na majira yake vizuri.
  Mwalimu alisisitiza maadali kwa viongozi wa umma na alitaka maendeleo yatokane na ushiriki wa wananchi katika kufanya kazi halali kwa juhudi na maarifa ili waweze kujitegemea. Alisisitiza ili tuendelee tunahitaji ardhi, watu, siasa safi na uongozi bora. Alikemea rushwa (adui wa haki) na uporaji wa raslimali za nchi kwa manufaa ya watu wachache. Aliona ni bora utajiri unaotokana na mali asili usubiri Watanzania waweze kuutumia wao wenyewe kuliko kuuweka rehani kama ilivyo sasa hivi.Ni wazi msisitizo wake kuhusu maadui watatu wa maendeleo – ujinga, umaskini na magonjwa – bado ni hai kwa maana hakuna maendeleo ya kweli kama maadui hao watatu bado wana nguvu.

  Mchango wake katika kupiga vita adui ujinga kwa kupanua wigo wa elimu hadi ya watu wazima ni kitu cha kujivunia.
  Raslimali za nchi yetu zinaporwa mchana na usiku na viongozi wanaopaswa kukemea hali hii wamekaa kimya. Baadhi yao walisubiri Mwalimu atutoke ndipo waoneshe makucha yao vizuri maana walijua hakuna atayeweza kuwanyooshea kidole na hawakuthubutu kufanya hivyo wakati akiwepo maana angewakosoa na kama walifanya walifanya kwa kujificha sana tofauti na ilivyo leo hii.Tunavyoadhimisha miaka 50 ya Uhuru na 12 tangu atutoke, hotuba zote za Mwalimu zina ujumbe wa usasa (kila hotuba aliyoitoa inaigusa jamii kwa sasa) – ni hotuba za kinabii tu zina ujumbe wa aina hii.

  Sikiliza hotuba zake alizozitoa miaka ya 1950s, 1960s, 1980s na 1990s zote zina ujumbe wa sasa na hazikinzani na ndiyo maana kila hotuba yake wananchi wanapenda kuisikiliza kwa vile inawagusa kutokana na yale yanayotendeka leo hii katika nchi yetu: haki imekuwa ya kununua, raslimali za nchi zinaporwa na viongozi walioko madarakani wanahalalisha uporaji huo, matajiri wanazidi kuwa matajiri na maskini kuwa maskini, ukabila, udini na utengano vimeanza kutunyemelea.
   
 2. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Jamani inatosha Nyerere alikuwa mtu makini rais wetu wa kwanza.

  Amekua tena Nabii hii kwangu ni ujinga
   
 3. ERIC JOSEPH

  ERIC JOSEPH JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Apumzike kwa aman mzee wetu huko aliko
   
 4. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  alikuwa mtoto wa mganga
   
 5. V

  Vonix JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 1,987
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  ALIKUWA NA MAONO!!!!!??????yaani nabii???weweee lala tu nabii anaanzisha kitu baadae kinafeli??sawa alikuwa na maono akaanzisha azimio la arusha then??????lilifeli na yeye alijua kuwa alifanya makosa kuwafukuza wakoloni mapema kabla uchumi wa nchi kuimalika.kuhusu elimu pia naona kama unajifurahisha nani alileta mfumo wa elimu wa jinsi hii yaani primary unasoma kiswahili masomo yote kiingereza kama somo linalojitegemea,ukiingia secondary masomo yote kiingereza kiswahili kama somo linalojitegemea utaratibu huu wa elimu huoni unakasoro kubwa sana???? uliusikia wapi kwingine kama si hapa tu ??alichokuwa anakifanya alikijua sana na alijua kwa kufanya hivyo angezalisha majinga mengi mno na ndio inavyotokea hadi leo,mtu anamaliza fomu four haelewi chochote aliishia kukariri tu ambako hakukumsaidia.Labda ukiniambia kuwa Nyerere alikuwa mzuri kwa kutoa hotuba sawa hapo sina pingamizi lakini usimamizi wa kitu anachokisema sifuli.
   
 6. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #6
  Oct 15, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Tafakari vizuri! Soma vizuri historia ya unabii kuanzia Musa. Nani aliyewafikisha waana wa Israeli nchi ya ahadi, Musa? Manabii wote walifaulu missions zao (as you know them)? Chukulia Yesu mwenyewe: did he succeed in his mission and did even his close disciples understand and implement what he taught them? Ukisha jibu hayo maswali sasa uje kwa Nyerere na uone kama failure disqualifies one from being a prophet. Niulize: je hata Mungu amefaulu jinsi alivyotaka wanadamu wawe (wamjue yeye kama Mungu wa kweli na wamtumikie yeye tu)?
   
 7. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ok, sijui kama unakumbuka Nyerere aliiacha nchi ikiwa kwenye hali ganii?

  Kama angekuwa Nabii mwenye "maono ya Kiungu", basi ningetarajia kuwa Utawala wake ungeifanya Tanzania iwe kwenye hali nzuri sana kiuchumi, lakini matokeo yalikuwa ni kinyume kabisa, aliiacha nchi ikiwa kwenye uchumi hoi taabani...
   
 8. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #8
  Oct 15, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,250
  Likes Received: 10,430
  Trophy Points: 280
  mjukuu wangu yawezekan ulisemalo likawa kweli kwani siku nyerere anazaliwa kulikuwa na mvua ndio maana akapewa jina la kambarage,vile vile siku ya mazishi yake pale Butiama mvua ilinyesha.kwa sisi wazee wa zamani hizi zaweza kuwa ishara za kinabii.
   
 9. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #9
  Oct 15, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Taratibu jama! Nyerere utamuona nabii kama tu una uelewa wa kiujima. Mtu unaposema eti aliona rasilimali za nchi ziachwe ili zije kutumiwa na wananchi wenyewe wakati wananchi haohao anawanyima elimu kuna unabii gani hapo? Hiyo elimu yenyewe ilikuwa kuwafundisha watu kusoma na kuandika tu ndiyo maana upeo wa Watanzania wengi wakati anaachia madaraka ulikuwa mdogo mno.
  Angekuwa nabii angemchagua Mwinyi kuongoza nchi, mtu ambaye uongozi wake ndiyo ulioasisi ufisadi?
  Watanzania tujifunze kuangalia mbele, hivi vilio vya kumlilia Nyerere havimsaidii mtu ndiyo maana kila mwaka utasikia kuna kongamano la kumuenzi lakini nani ameona matunda ya hayo makongamano zaidi ya watu kutupigia kelele za kijamaa kwenye TV?
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,661
  Trophy Points: 280
  Unasahau kwamba duniani kulikuwa na matatizo mbali ya kiuchumi ambayo yaliitingisha dunia nzima nzima hata nchi za Magharibi na pia Mwalimu kwa kuamua kufuata siasa ya Ujamaa nchi za magharibi zilimpiga vita sana ili asifanikiwe lakini pamoja na hayo yote hata siku moja hakukubali masharti mbali mbali ya IMF na WB eti ya kuunusuru uchumi wa Tanzania. Kuanzi awamu ya Mwinyi tulikubali masharti mengi ya IMF & WB kama vile kushusha thamani ya shilingi yetu, ubinafsishaji wa nashirika yetu mbali mbali na pia kuwakaribibisha (wawezekaji) mimi hawa huwaita wachukuaji maana sioni kama Watanzania tunafaidika kwa lolote tangu hawa wakaribishwe rasmi nchini.
   
 11. V

  Vonix JF-Expert Member

  #11
  Oct 15, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 1,987
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Makobe T.unaenda mbali sana kama unadiliki kuulinganisha unabii wa Mussa ,Yesu Kristo na Mungu fikiri mara mbili.Unabii wa Nyerere unajengwa kwenye dhana ipi???Ni kweli Musa hakufanikiwa kwani yeye hata kanani hakuiona lakini ujue Mungu aliongea na Musa kila kila hatua toka misri hadi jangwani Yesu kristo vilevile aliongea na Mungu hatua kwa hatua hata akiwa msalabani. Nabii Nyerere kama unavyodai aliongea na Mungu hatua kwa hatua jinsi alivyopaswa kuiongoza nchi hii hivyo hufeli kwake kulibarikiwa???kabla hujamhusisha Mungu na nabii wako fikiri kifimbo chake,na husisha matukio siku ya mazishi yake pale butiama labda kama hukufuatilia mambo ya ajabu sana yalitokea.
   
 12. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #12
  Oct 15, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Ukisoma uwasilishaji wa mada hii utaelewa ni kwa misingi gani unabii wake umejengwa. Nanukuu tena nilichoandika: "Neno nabii linatoka na neno la Kiebrania nābî au prophētēs (kwa Kiingereza prophet) mtu mwenye maono (visionary, seer) na mwenye ujumbe wenye mantiki (rational speech) na unaogusa jamii kwa ujumla wake hasa kwa kutoa ujumbe wenye usasa (God's now message) kwa watu husika.Mwalimu Julius Nyerere ni mmoja wa viongozi wachache duniani, ambaye anakidhi vigezo vya kuwa nabii kwa taifa letu na Afrika nzima kutokana na mchango wa maisha yake binafsi (uadilifu wake) na uongozi wake uliotukuka (kuonesha njia).

  Alitumia elimu yake kwa manufaa ya wote – alikuwa akiwafundisha wakulima namna ya kutayarisha mashamba
  yao kutokana na majira ya mwaka maana alijua jiografia ya nchi na majira yake vizuri.
  Mwalimu alisisitiza maadali kwa viongozi wa umma na alitaka maendeleo yatokane na ushiriki wa wananchi katika kufanya kazi halali kwa juhudi na maarifa ili waweze kujitegemea. Alisisitiza ili tuendelee tunahitaji ardhi, watu, siasa safi na uongozi bora. Alikemea rushwa (adui wa haki) na uporaji wa raslimali za nchi kwa manufaa ya watu wachache. Aliona ni bora utajiri unaotokana na mali asili usubiri Watanzania waweze kuutumia wao wenyewe kuliko kuuweka rehani kama ilivyo sasa hivi.Ni wazi msisitizo wake kuhusu maadui watatu wa maendeleo – ujinga, umaskini na magonjwa – bado ni hai kwa maana hakuna maendeleo ya kweli kama maadui hao watatu bado wana nguvu.

  Mchango wake katika kupiga vita adui ujinga kwa kupanua wigo wa elimu hadi ya watu wazima ni kitu cha kujivunia.
  Raslimali za nchi yetu zinaporwa mchana na usiku na viongozi wanaopaswa kukemea hali hii wamekaa kimya. Baadhi yao walisubiri Mwalimu atutoke ndipo waoneshe makucha yao vizuri maana walijua hakuna atayeweza kuwanyooshea kidole na hawakuthubutu kufanya hivyo wakati akiwepo maana angewakosoa na kama walifanya walifanya kwa kujificha sana tofauti na ilivyo leo hii.Tunavyoadhimisha miaka 50 ya Uhuru na 12 tangu atutoke, hotuba zote za Mwalimu zina ujumbe wa usasa (kila hotuba aliyoitoa inaigusa jamii kwa sasa) – ni hotuba za kinabii tu zina ujumbe wa aina hii.

  Sikiliza hotuba zake alizozitoa miaka ya 1950s, 1960s, 1980s na 1990s zote zina ujumbe wa sasa na hazikinzani na ndiyo maana kila hotuba yake wananchi wanapenda kuisikiliza kwa vile inawagusa kutokana na yale yanayotendeka leo hii katika nchi yetu: haki imekuwa ya kununua, raslimali za nchi zinaporwa na viongozi walioko madarakani wanahalalisha uporaji huo, matajiri wanazidi kuwa matajiri na maskini kuwa maskini, ukabila, udini na utengano vimeanza kutunyemelea."

  Kulinganisha na Musa, Yesu na Mungu ni kutaka kukuonesha kuwa "kushindwa" kufanya kitu fulani siyo kutokuwa nabii. Afterall, Musa mwenyewe alimwambia Mungu kuwa akiongea na pharao hatamsikiliza maana hajui kuongea ila Mungu alimwahidi kumsaidia. Nyerere inawezekana alishindwa kulifanya taifa liendelee kiuchumi lakini sidhani pia alishindwa kuonesha moyo wa utaifa na uzalendo ambao Watanzania wengi leo wanalia nao. Nabii (katika context yangu) ni kule kuwa na "message ya usasa" something that challenges you and me to do more katika taifa letu kuliko ilivyo sasa hivi kuwa kiongozi maana yake ni kuwa fisadi na bossy!
   
 13. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hivi kujua kuwa eneo fulani mvua itanyeshwa wakati gani, na mazao yepi yanafaa sehemu ipi ni unabii? sasa kama kwa Nyerere kusema hivyo amekuwa Nabii sasa akina Isaac Newton, Michael Faraday, Albert Einsten, Galileo Galilei, Aristotle na Plato si tutawaita Manabii Wakuu kama sio miungu kabisa?shame...

  Sijui kwa upande wako Nabii ni mtu wa namna gani, ila kwa mafundisho ya Ki-Biblia, Nabii ni Mtu Anapewa ujumbe na Mungu na kuupeleka kwa watu wengine kama Mungu atakavyomuagiza/alivyomuagiza, sasa kwa hili, Sijui kama Nyerere amewahi kusema popote kuwa alikuwa anapewa maagizo na Mungu.

  Nakumbuka kwenye hotuba yake ya kutimiza miaka 75, Mwl Nyerere alipata kuongea mbele ya wakati wake kwa kusema nanukuu "NINA UHAKIKA, NITAMUONA RAIS WA NNE AKIINGIA MADARAKANI", yaani atakuwepo hai mpaka atleast 2005. Lakini kumbe mawazo yake sio sawa na mawazo ya Mungu, ata mwaka 2000 hakufika.

  Nasharia, miaka michache ijayo wengine pia watasema Mkapa ni "Nabii" kwa sababu aliwahi kusema "Kwa wale wasio tayari kujituma na wale wanaoingojea serikali iwafanyie kila kitu, hao wataachwa nyuma kimaendeleo," na imekuwa kweli.
   
 14. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #14
  Oct 15, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  uganda wanataka kumpa utakatifu kama mama Teresa wa India!kwa maoni yangu nyerere hana una bii wowote
   
 15. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #15
  Oct 15, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mchakato wa kupewa utakatifu si wa Uganda ni Kanisa katoliki Tanzania .Waganda hawatoa utakatifu kwa mujibu wa wakatoliki ila mchakato ndani ya Kanisa ndiyo utakaofanya aitwe mwenye heri na kuitwa Mtakatifu .
   
 16. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #16
  Oct 15, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hapa wengi wanaposikia neno "NABII" wanfikiri ni la kidini, Nabii ni sifa ya mtu aliyonayo kwa kutamka "maono-vision" alionayo ili watu waelewe kitakachokuja kutokea hapo baadaye na madhara yake kama hatua kadhaa hazitachukuliwa, na usichanganye na watabiri! Neno Nabii ni kama maneno mengine ktk lugha na sio kidini tuu! Mbona hamsemi hata kwenye dini kuna walimu wa neno, walimu wa sheria na wachungaji ambao hata kwa wafugaji wapo?

  Msibishane sana Mwl. Nyerere alikuwa na maono ndo maana hotuba zake zinakuwa ni very current na hali ya sasa nchini. Vasco da Gamba je, hotubazake zina maono? Mkaa hapa naye? Mzee wa Ruksa alitoa hotuba inayoishi leo japo anamvi nyeupe kama Nyerere? Jibu unalo. Nyerere was the Prophet!
   
 17. y

  yaya JF-Expert Member

  #17
  Oct 15, 2011
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu, ujinga ni kutokujua kitu au jambo linalohitaji akili kidogo tu ya tafakuri. Nadhani you're obsessed too much onto religious matters than day to day life, otherwise you'd need very little sense to understand what the gentleperson meant when he said Mwalimu was a prophet.
   
 18. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #18
  Oct 15, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hapa ndipo ulipopotoka, kwa definition hii almost wote wenye busara, wote wanaowaongoza watu, na Wanataaluma woote utawaita Manabii...

  Nikwambie tu, Nabii ni zaidi ya "Mtu anayeona mbali" (who can sees the future), Nabii ni Mtu Aliyechaguliwa na Mungu kuufikisha Ujumbe wake kwa Watu kwa niaba ya Mungu Mwenyewe, kwa kifupi ni Nabii ni Msemaji wa Mungu (God's Spokesman).

  ...Sasa kama Nyerere alikuwa ni God's Spokesman, wewe wasema...
   
 19. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #19
  Oct 15, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Walimu wanakazi sana, inaonekana wewe ni mgumu wa kuelewa lakini mwepesi wa kukariri kama kasuku. Maono yanaweza kutoka kwa Mungu hata Shetani! Waganga wa jadi wanaotoa unabii ama utabiri ni mawakala wa Ibilisi. Nakubaliana na aliyesema JK Nyerere ni Nabii wa siasa Tanzania!

  Tatizo mkishakaririshwa madrasa hakuna kuchambua na kufikiri tena. Usilete definition za kwenye nyumba za ibada hapa!
   
 20. m

  mpiganaji86 Senior Member

  #20
  Oct 15, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naungana na vonix mia kwa mia kwan nyerere alikuwa mshirikina hata alivyokufa kule butiama kwenye kaburi lake yalitokea manyani ya ajabu na milio ya ajabu mpaka maaskari walinzi wakakimbia,hana lolote la unabii nyerere ni mlozi mkubwa na tapeli kwani alikataza watu wasiwe na tv ,tv anayo mwenyewe ikulu kesho anaitisha mikutano na kuwaambia wananchi ameona nchi fulan itatokea vita kumbe yeye kashaona kideoni sasa huo ndio unabiii ?
   
Loading...