Ili uwe nabii kwanza lazima uwe mcha Mungu.Nyerere hakuwa mcha Mungu,he belonged to this world.Kwa hiyo hakuwa Nabii kwa kigezo chochote kile.
Neno nabii linatoka na neno la Kiebrania nābî au prophētēs (kwa Kiingereza prophet) mtu mwenye maono (visionary, seer) na mwenye ujumbe wenye mantiki (rational speech) na unaogusa jamii kwa ujumla wake hasa kwa kutoa ujumbe wenye usasa (Gods now message) kwa watu husika.Mwalimu Julius Nyerere ni mmoja wa viongozi wachache duniani, ambaye anakidhi vigezo vya kuwa nabii kwa taifa letu na Afrika nzima kutokana na mchango wa maisha yake binafsi (uadilifu wake) na uongozi wake uliotukuka (kuonesha njia).
Alitumia elimu yake kwa manufaa ya wote alikuwa akiwafundisha wakulima namna ya kutayarisha mashamba yao kutokana na majira ya mwaka maana alijua jiografia ya nchi na majira yake vizuri. Mwalimu alisisitiza maadali kwa viongozi wa umma na alitaka maendeleo yatokane na ushiriki wa wananchi katika kufanya kazi halali kwa juhudi na maarifa ili waweze kujitegemea. Alisisitiza ili tuendelee tunahitaji ardhi, watu, siasa safi na uongozi bora. Alikemea rushwa (adui wa haki) na uporaji wa raslimali za nchi kwa manufaa ya watu wachache. Aliona ni bora utajiri unaotokana na mali asili usubiri Watanzania waweze kuutumia wao wenyewe kuliko kuuweka rehani kama ilivyo sasa hivi.Ni wazi msisitizo wake kuhusu maadui watatu wa maendeleo ujinga, umaskini na magonjwa bado ni hai kwa maana hakuna maendeleo ya kweli kama maadui hao watatu bado wana nguvu.
Mchango wake katika kupiga vita adui ujinga kwa kupanua wigo wa elimu hadi ya watu wazima ni kitu cha kujivunia.Raslimali za nchi yetu zinaporwa mchana na usiku na viongozi wanaopaswa kukemea hali hii wamekaa kimya. Baadhi yao walisubiri Mwalimu atutoke ndipo waoneshe makucha yao vizuri maana walijua hakuna atayeweza kuwanyooshea kidole na hawakuthubutu kufanya hivyo wakati akiwepo maana angewakosoa na kama walifanya walifanya kwa kujificha sana tofauti na ilivyo leo hii.Tunavyoadhimisha miaka 50 ya Uhuru na 12 tangu atutoke, hotuba zote za Mwalimu zina ujumbe wa usasa (kila hotuba aliyoitoa inaigusa jamii kwa sasa) ni hotuba za kinabii tu zina ujumbe wa aina hii.
Sikiliza hotuba zake alizozitoa miaka ya 1950s, 1960s, 1980s na 1990s zote zina ujumbe wa sasa na hazikinzani na ndiyo maana kila hotuba yake wananchi wanapenda kuisikiliza kwa vile inawagusa kutokana na yale yanayotendeka leo hii katika nchi yetu: haki imekuwa ya kununua, raslimali za nchi zinaporwa na viongozi walioko madarakani wanahalalisha uporaji huo, matajiri wanazidi kuwa matajiri na maskini kuwa maskini, ukabila, udini na utengano vimeanza kutunyemelea.