Mwalimu aliyefahamika kama Sospeter Ogo wa shule ya sekondari Itiryo iliyopo wilaya ya Tarime tarafa ya ingwe, ameuawa kikatili kwa kuchomwa mkuki shingoni na vijana wanaojiandaa na tohara.
Marehemu ameuawa mida ya saa 1 asubuhi akitoka kuwasindikiza wenzake waliokuwa wanaenda kusimamia mtihani shule jirani ya Bungurere, ndipo vijana hao walipomsimamisha wakimtaka awape hela na aliposema hana wakamchoma mkuki shingoni na kufariki pale pale.
Vijana hao wanaojiandaa na tohara ambao wamekuwa wakitembea na mikuki na sime wamekuwa tishio katika eneo hilo, kwani wamekuwa wakiomba pesa kwa nguvu toka kwa bodaboda na watu wengine na endapo huna basi unapigwa au kuharibiwa pikipiki yako.
Hata hivyo jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata baadhi ya watuhumiwa wa mauaji hayo.