Mwalimu akutwa mtupu shuleni Lindi


M

mazegezege

Member
Joined
Mar 11, 2012
Messages
27
Points
0
M

mazegezege

Member
Joined Mar 11, 2012
27 0
WANA JF HII IMEKAJE?
MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Rutamba, Wilaya ya Lindi amekutwa akiwa na nguo za ndani pekee katika usingizi mzito kwenye kibao cha shule hiyo huku akiwa hajitambui kwa madai ya kilichomkutana kinahusishwa na imani za kishirikina.

Tukio hilo limetokea juzi usiku baada ya mkazi mmoja wa kijiji hicho, Juma Mbilemoto kumkuta mwalimu huyo akiwa kwenye kibao hicho wakati alipokuwa anamsindikiza nduguye,Aisha Mbilimoto aliyekuwa anasafiri kuelekea Dar es Salaam.

Akizungumzia tukio hilo, shuhuda huyo alisema alimkuta mwalimu huyo akiwa amelala chini ya kibao cha shule akiwa na nguo ya ndani tu (chupi)huku akikoroma kutokana na kuwa na usingizi mzito.Alisema awali hakumtambua mtu huyo lakini baada ya kumkaribia alimtambua kuwa alikuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo na ndipo alipochukua jukumu la kumwamsha ili amvalishe kanga, lakini aliikataa na kuondoka kwenda nyumbani kwake akiwa kama alivyokutwa
Kwa upande wao walimu wa shule hiyo walisema kuwa, wamekosa molari wa kufanya kazi kutokana na kitendo alichofanyiwa mwalimu mwenzao.

Akizungumza kwa niaba ya walimu wenzake mwalimu wa taaluma wa shule hiyo, Francis Milanzi alisema walimu shuleni hapo wamekosa amani na kuwasababishia kuzihama nyumba zao kwa muda na badala yake kwenda kukesha kwenye ofisi za walimu tangu tukio hilo litokee.

Ofisa elimu wa Wilaya ya Lindi, Cosmas Magigi alisema amepokea taarifa za tukio hilo kwa huzuni na amewaomba walimu kuwa na subira wakati utaratibu wanalishughulikia suala hilo.

Magigi aliongeza kuwa ofisi yake itafanya utaratibu wa kumhamisha mwalimu huyo na kumtafutia shule nyingine huku akiwataka wakazi wa eneo hilo kujenga ushirikiano na watumishi ili waweze kutekeleza majukumu yao.
Hili ni tukio la pili kutokea katika halmashauri hiyo mwaka huu ambapo la kwanza lilitokea April katika Shule ya Sekondari Ruhokwe, mwalimu wa shule hiyo alilazwa kwenye kibao cha shule akiwa uchi wa mnyama.

SOURCE!! Mwananchi, December 15 2012
 
chitambikwa

chitambikwa

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Messages
3,938
Points
1,195
chitambikwa

chitambikwa

JF-Expert Member
Joined Nov 8, 2010
3,938 1,195
Elimu maeneo ya pwani ni balaa
 
brasy coco

brasy coco

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2012
Messages
1,457
Points
2,000
brasy coco

brasy coco

JF-Expert Member
Joined Apr 25, 2012
1,457 2,000
wa Africa kwa Uchawi noma sijui kama hawajamnaninii
 
Msenyele

Msenyele

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2012
Messages
332
Points
195
Msenyele

Msenyele

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2012
332 195
Wasiwe wanavichapa vitoto, ni noma kama haujaaga vizuri kwa home.
 
dedam

dedam

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2011
Messages
846
Points
195
dedam

dedam

JF-Expert Member
Joined Jan 5, 2011
846 195
kuna mwalimu mmoja alitaka kuhama shule ikishindikana, siku moja usiku akachukua wembe akajinyoa upande mmoja kesho yake asubuh brek ya kwanza kwa mwalimu mkuu. mwalimu mkuu kuona vile akaona balaa hili brek ya pili kwa D.E.O,naye akaona balaa hilkijana akapewa uhamisho fasta. ubunifu mwingne noma.
 
B

Bepali

Senior Member
Joined
Oct 29, 2012
Messages
180
Points
0
B

Bepali

Senior Member
Joined Oct 29, 2012
180 0
kusini ndio mana hakuendelei milele sabab ya roho mbaya.
 
Kibanga Ampiga Mkoloni

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2007
Messages
16,712
Points
2,000
Kibanga Ampiga Mkoloni

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2007
16,712 2,000
Hii SAYANSI hii hiii!
 
K

Kachangamtoto

Member
Joined
Dec 4, 2012
Messages
82
Points
125
K

Kachangamtoto

Member
Joined Dec 4, 2012
82 125
ndo mana vijana wa sikuiz hawataki kusoma education
 
Mzito Kabwela

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2009
Messages
17,820
Points
2,000
Age
36
Mzito Kabwela

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2009
17,820 2,000
Watu wa Lindi ni waumini wazuri sana wa dini yao sasa ushirikina sijui kwa nini wanauendeleza
 
Money Stunna

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Messages
13,097
Points
1,500
Money Stunna

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2011
13,097 1,500
mijitu,mitoto ikishirikiana na wazazi wao hawataki kusoma
 
Katavi

Katavi

Platinum Member
Joined
Aug 31, 2009
Messages
40,821
Points
2,000
Katavi

Katavi

Platinum Member
Joined Aug 31, 2009
40,821 2,000
Huyo mwalimu ni mwanamke au mwanaume!
 

Forum statistics

Threads 1,285,027
Members 494,367
Posts 30,847,695
Top