Mwalimu akamatwa na viroba vya shilingi milioni 77

McCain

JF-Expert Member
Dec 2, 2016
1,169
517
39cb9543e4368f604e195411cc7427ed.jpg

MWALIMU wa shule ya sekondari ya St Margareth wilayani Igunga amekamatwa na boksi za pombe aina ya viroba 825 akiwa amevihifadhi katika duka lake.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Hamisi Selemani alimtaja mwalimu aliyekamatwa na maboksi hayo kuwa ni John Pastory (48).

Kamanda Selemani alisema mwalimu huyo alikamatwa Machi 7, majira ya saa 5 asubuhi katika mtaa wa Mwayunge mjini Igunga.

Alisema baada ya jeshi la polisi kufanya upekuzi walifanikiwa kukamata vioroba hivyo vyenye thamani ya sh 77,136,000.

Aidha kamanda Selemani alisema mwalimu huyo ndiye alikuwa msambazaji mkubwa wa pombe aina ya viroba wilaya ya Igunga.

Nae mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mwayunge kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, Abel Shampinga alilipongeza jeshi polisi kwa kuwakamata wauzaji wa pombe za viroba na kuongeza kuwa yeye kama mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mwayunge hayuko tayari kuwatetea watu wanaovunja sheria za nchi.
 
Nauliza tu ni marufuku kuuza au kutumia?mfano tayari ninayi nyumbani /ghalani na imepigwa marufuku kuuzwa, na sababu zikiwa ni uharibifu wa mazingira na matumizi kwa vijana wadogo .
Sasa nikiamua kutumia mwenyrwe bunafsi katika birthday parties ,harusi za wajukuu wangu na vifurahisho vingine kosa?
 
Nauliza tu ni marufuku kuuza au kutumia?mfano tayari ninayi nyumbani /ghalani na imepigwa marufuku kuuzwa, na sababu zikiwa ni uharibifu wa mazingira na matumizi kwa vijana wadogo .
Sasa nikiamua kutumia mwenyrwe bunafsi katika birthday parties ,harusi za wajukuu wangu na vifurahisho vingine kosa?
Haram baba
 
Waangalie kwanaza kabla ya kuhukumiwa iwapo alinunua wakati wa kipindi halali, au baada ya katazo ndo kwa kiburi akaenda kununua.
 
Kwa mfano huyu mwl atapelekwa mahakamani kwa sheria ipi
 
Mbona sijasikia wala kuona mtu hata mmoja ameenda mahakamani kuishtaki serikali kwa kufanya Wrong Attempt
 
Sidhani kama katika hili serikali inatendea haki hao wauzaji.

Kwanini serikali isingeanza kwanza kuzuia kiwanda kuzalisha viroba.

Then wawape muda hao wauzaji wamalize bidhaa walizonazo.

Kwa sababu asilimia kubwa ya wafanyabiashara wana mikopo hivyo unapowapa muda mfupi wa kuondoa bidhaa katika soko, wanatarijia marejesho wanatoa wapi (sijashangaa yule wa dodoma alivyoamua kujiua).

Serikali inafanya kitu kizuri lakini iangalie hatua wanazochukua na madhara yake issue ya viroba ni issue ambayo ilikuwa biashara halali hivyo ili kuiondoa inahitaji muda mrefu ili kuepusha kuacha madhara makubwa kwa wafanyabiashara
 
Zote hizo zingeishia midomoni kwa watoto wetu, eh Mwenye Enzi Mungu linda watoto wetu jamani, yeleuwiii!
 
Back
Top Bottom