Simon Mato kuna siku nilikuambia kwenye siasa umezijua wakati wa haya mafuriko ya Lowassa na Magufuli 2015, ila ukamwaga povu la hatari. Sasa ndio utaijua ccm ni nini na hivyo viwanda ulivyoambiwa wenzio wanaanza kubadili maana na kusema eti viwanda ni kama cherehani, blenda nk. Watu waliahidi kupambana na mafisadi kwani ndio ilikuwa chukizo la wananchi na kilichowapa ushindi ni tume na sio kura za watu.
Kwa kukusaidia hiyo mahakama ni kiini macho kwani washitakiwa wakubwa wa hiyo mahakama ni hao waliojifanya kuianzisha. Nakuhakikishia ikianza kazi kama itatenda haki basi tutaingia kwenye uchaguzi mpya kabla ya 2020. Wenzako wameanzisha mahakama ya mafisadi kwa ajili ya wapinzani, wamekuta hawazidi wawili na ni toka hukohuko ccm. Baada ya kuuona ukweli wa wateja wa mahakama wakaita ni makaburi. Sasa ww unataka wafukue makaburi watakayoshindwa kufukia? Napenda ufahamu huko ulipo ili ufit inabidi uwe mnafiki, kinyume na hapo ujue umeingia choo cha kike.