Mwakyembe, tunataka watuhumiwa wote wa ufisadi washtakiwe

simon mato

JF-Expert Member
Sep 27, 2015
926
500
Ndugu wanajamvi;

Ni wakati umefika ukweli utuweke huru kabsaa. Mahakama ya mafisadi ilikuwepo kwenye agenda na kuhubiriwa kila kona ya nchi kwenye ilani ya CCM na utekelezwaji wake utakavokua.

Sitaki niongee mengi sanaaa lakini waziri wa sheria hawezi kutupepesa macho tena waziwazi bila aibu kuwa hiyoo mahakama imekosa kesi za kusikiliza huu ni uwendawazimu ambao ata kichaa uwezi kumdanganya hivi!

Maswali yangu kwa MWAKYEMBE:

1. je ni ufisadi upi anauzungumzia ni baada ya tarehe 25 october 2015 au kabla ya hapo! Tunamtaka hatoke nje hadharani atupe majibu!

2. Je kama ni baada ya october 2015 mbona kuna kesi zimetokea za kuhujumu uchumi kama Bossi wa NIDA, TPA , TRA yule aliyekuwa anachakachua mamilioni kwa dakika! Au hawa si watanzania? au mafisadi wana sura!! Atoke nje hatupe majibu hadharani!!

3:Kama ufisadi anaouzungumzia ni kabla na baada ya uchaguzi, Mbona MWAKYEMBE umesikika kwenye viuga tofauti hadi kwenye media ukihubiri ufisadi wa LOWASHA nashangaa umeufyata kana kwamba hujawahi kusikia ata jina la EL. Janja janja hatutaki toka nje utupe majibu hadharani!!

4:Nikimnukuu aliyekuwa msemaji wa ccm kabla hajateuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa njombe Mhe.OLESENDEKA amesikika akisema ata CHADEMA wahangaike vipi! Aliyekuwa mgombea wao kupitia UKAWA ni mteja mzuri kwenye mahakama ya mafisadi kwahyo ajiandae psychologically hili limetamkwa kwenye vuguvugu la UKUTA kama mtakumbuka!!! Tunamtaka Olesendeka hatoke nje hadharani atupe majibu!!!

5:Kama mnachukulia kuwa ufisadi ulianza baada ya 25 october 2015 na mahakama itaanza kazi kwa watuhumiwa wa kuanzia baada ya hapo? Naomba majibu ya kuridhisha mnaonaje ata wanafunzi waliotumia mikopo ya Elimu ya juu wasamehewe mara moja maana sisi wote ni watanzania tena bora ata hawa waliokuwa wanafanya kazi serikalini na kupiga dili za tumbo hao wanafunzi kuna wengine hadi mda huu hawajaariwa wanasota mtaani!! Naomba majibu ya kutosha MWAKYEMBE!!!

yangu kwa leo ni hayo tuuh nisipopewa majibu ya kutosha ndani ya masaa 48 nitaanzisha operation ya "SINA IMANI NA SERIKALI YA AWAMU YA TANO" kwa sababu mimi nilimpigia mgombea wa CCM kura kutokana na alivyokuwa anajipambanua kupambana na ufisadi na alivopiga hatua hadi kuanzisha mahakama ya mafisadi kwa hela za kodi za wanyonge iweje ikose kazi tena wakati watuhumiwa wapo mtaani wanadunda? Katika hili ukweli utaniweka huru na mwenye akili kamili atajua nimezungumzia nini!!!

Ni wakati umefika kuacha siasa nyepesi kwenye masuala magumu katika taifa hili tuwe na utu na uzalendo katika taifa letu.

Ni wako kijana mtiifu, mzalendo na mwanaharakati wa kweli katika taifa hili.
 
Major

JF-Expert Member
Dec 20, 2007
1,867
2,000
Yeye mwenyewe anatakiwa atumbuliwe. Kwani ile ishu ya mabehewa below standard imekwisha?
 
mzalendo15

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
1,367
2,000
Mganga siku zote hawezi kujiganga licha ya kuwa na zana zote. Hizi ni ndoto za mchana maana katika ukoo huu wa mafisadi wengine bado wananyadhifa Kubwa katika nchi hii. Na mkuu mwenyewe alishasema hafukui makaburi anaogopa anaweza akakuta suti take humo.
 
kinje ketile

JF-Expert Member
Dec 12, 2015
617
1,000
Olesendeka unamwonea tu,mbona wengi walisema kuwa Mh yule Fisadi.umesahau list of shame iliyozungushwa mikoa yote
 
demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
5,407
2,000

Watendaji a serikali ndio waigizaji wakuu....

Aliyeiandika Script ni Mtukufu JPM
 
Bakeza

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
337
250
Nasikia kuna kiwango cha fedha ili kesi ikidhi kuingia kwenye mahakama ya mafisadi labda hapo ndo pana tatizo walioitwa mafisadi wote hawajakidhi viwango. Nawaza tu
 
treborx

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
4,634
2,000
Wana Kyela wameshamsikia. Tunamsubiri aje 2020, ili tumchinjie baharini. Lakini kabla ya hapo, lazima kwanza tumfilisi kwa kula fedha zake zote atakazopata baada ya bunge kuvunjwa. Hiyo ndiyo namna ya kuwakomesha hawa watu.
 
Bakeza

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
337
250
Nasikia kuna kiwango cha fedha ili kesi ikidhi kuingia kwenye mahakama ya mafisadi labda hapo ndo pana tatizo walioitwa mafisadi wote hawajakidhi viwango. Nawaza tu
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
33,607
2,000
Simon Mato kuna siku nilikuambia kwenye siasa umezijua wakati wa haya mafuriko ya Lowassa na Magufuli 2015, ila ukamwaga povu la hatari. Sasa ndio utaijua ccm ni nini na hivyo viwanda ulivyoambiwa wenzio wanaanza kubadili maana na kusema eti viwanda ni kama cherehani, blenda nk. Watu waliahidi kupambana na mafisadi kwani ndio ilikuwa chukizo la wananchi na kilichowapa ushindi ni tume na sio kura za watu.

Kwa kukusaidia hiyo mahakama ni kiini macho kwani washitakiwa wakubwa wa hiyo mahakama ni hao waliojifanya kuianzisha. Nakuhakikishia ikianza kazi kama itatenda haki basi tutaingia kwenye uchaguzi mpya kabla ya 2020. Wenzako wameanzisha mahakama ya mafisadi kwa ajili ya wapinzani, wamekuta hawazidi wawili na ni toka hukohuko ccm. Baada ya kuuona ukweli wa wateja wa mahakama wakaita ni makaburi. Sasa ww unataka wafukue makaburi watakayoshindwa kufukia? Napenda ufahamu huko ulipo ili ufit inabidi uwe mnafiki, kinyume na hapo ujue umeingia choo cha kike.
 
orthogonal

Member
Aug 9, 2016
99
150

Mkuu umepiga mahali sahihi kwa wakati sahihi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom