Mwakyembe: Serikali haiwezi kufanya kazi bila vyombo vya habari, adai Makonda sio Kipaumbele

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970
Akiongea na waandishi wa habari leo mjini Dodoma, waziri mpya wa habari utamaduni na michezo amekaribishwa wizarani na kuzungumzia mambo mbali mbali anayotarajia kuyafanya. Miongoni mwa mambo mengine, Mwakyembe amesema serikali duniani kote haziwezi kufanya kazi bila vyombo vya habari, amedai atashirikiana nao.

Kuhusu sakata la mkuu wa mkoa kuvamia Clouds, Mwakyembe amedai japo ripoti hajaiona lakini yeye kama mwanasheria ni mwiko na hatapeleka kitu ambacho anaona hakijakamilika kwani kwa taarifa alizonazo kupitia vyombo vya habari ni kuwa taarifa yote inatokana na ushahidi wa mlalamikaji ambae ni Clouds lakini hakuna ushahidi wowote wa upande wa pili na wamekiri kuwa haukupatikani.

Amedai wanaheshimu sana kanuni za asili(Principles of natural justice) kwani mwanasheria yeyote lazima aheshimu kanuni hiyo, ameongeza kuwa mtu hawezi kuwa hakimu kwenye suala lake mwenyewe na yeye angekuwa active journalist asingeweza kulishughulikia. Pia kwa mujibu wake kanuni hio pia inasisitiza kusikilizwa upande wa pili hivyo hawezi kuwapelekea viongozi wake kitu ambacho kina upande mmoja kwa sababu itakuwa ni kuwapa kazi wao wautafute. Amesema kazi yake yeye sasa ni kutafuta upande wa pili na amedai ataupata tu.

Mwakyembe amesema jambo la Makonda sio kipaumbele kwenye wizara yake na hakuapa kwa ajili ya hilo suala peke yake na ni moja tu ya masuala mengi na hatayakwepa na atayaangalia. Amesisitiza yeye ni mwanasheria mkongwe na hawezi kufanya kosa la kupeleka taarifa ya upande mmoja viongozi wake wa juu kwani nao watamshangaa, pia hataunda kamati kwani kamati ni yeye mwenyewe na atakaa na wenzake.

Kwenye utamaduni amesema jambo kubwa ni kuendeleza lugha ya Kiswahili na amemshukuru Rais Maguful, amedai haiwezekani akaja mgeni akaongea kwa Kiingireza na sisi kutafsiriwa na ikifika zamu yetu bado tunajibu kwa Kiingereza. Amedai yeye amesoma Ujerumani na watu wanajivunia kwa lugha yao.

Amesema wajibu wao ni kuwapata vijana wanaojua lugha za kigeni na kuwalea kama wakishindwa kuwaajiri kama wizara. Amesema dunia nzima inajua nyumbani kwa Kiswahili ni Tanzania na Rais wa Jamhuri ameonyesha njia

Akiongea na waandishi wa habari leo mjini Dodoma, waziri mpya wa habari utamaduni na michezo amekaribishwa wizarani na kuzungumzia mambo mbali mbali anayotarajia kuyafanya. Miongoni mwa mambo mengine, Mwakyembe serikali duniani kote haziwezi kufanya kazi bila vyombo vya habari, amedai atashirikiana nao.

.....mbona serikali yangu ya mkoa wa Dalisalama inafanya kazi bila wanahabari japo imewamisije!!!!
 
Akiongea na waandishi wa habari leo mjini Dodoma, waziri mpya wa habari utamaduni na michezo amekaribishwa wizarani na kuzungumzia mambo mbali mbali anayotarajia kuyafanya. Miongoni mwa mambo mengine, Mwakyembe serikali duniani kote haziwezi kufanya kazi bila vyombo vya habari, amedai atashirikiana nao.

Kwenye utamaduni amesema jambo kubwa ni kuendeleza lugha ya Kiswahili na amemshukuru Rais Maguful, amedai haiwezekani akaja mgeni akaongea kwa Kiingireza na sisi kutafsiriwa na ikifika zamu yetu bado tunajibu kwa Kiingereza. Amedai yeye amesoma Ujerumani na watu wanajivunia kwa lugha yao.

Amesema wajibu wao ni kuwapata vijana wanaojua lugha za kigeni na kuwalea kama wakishindwa kuwaajiri kama wizara. Amesema dunia nzima inajua nyumbani kwa Kiswahili ni Tanzania na Rais wa Jamhuri ameonyesha njia
Mitandao ya kijamii ni sehemu ya vyombo vya habari, je hajasema neno kuihusu? Je ile laana ya kutamani shetani ashuke (kutoka wapi?) ivifungie imebatilishwa?
 
Aaanze kwanza na uhuru wa vyombo vya habari, na aanzie kwenye report ya Nape, asipolisemea hilo na kuwajibika nalo basi naye atakua hakuna anachofanya hapo wizarani zaidi ya kutetea tumbo lake na watoto wake.
 
Huyu wazir mnafk sana,nany waandish wa habar mkiandika kaz za serikal mtakuwa wapumbav wa ku2pwa! rais kasha watosa hana haja na waandish wa habar niny mnajikomba 2!

Mwakyembe ni kati ya vijana waoga na wale ambao kwao tumbo ni muhimu zaidi.Na uzuri waliongelewa na muanzilishi wa chama CCM wajitafakari.
upload_2017-3-29_12-8-33.png
 
Kwenye utamaduni amesema jambo kubwa ni kuendeleza lugha ya Kiswahili na amemshukuru Rais Maguful, amedai haiwezekani akaja mgeni akaongea kwa Kiingireza na sisi kutafsiriwa na ikifika zamu yetu bado tunajibu kwa Kiingereza. Amedai yeye amesoma Ujerumani na watu wanajivunia kwa lugha yao.

Ninaamini fika ule ugonjwa aliouugua Mwakyembe uliathiri akili za jamaa, kwa sababu amekuwa si yule Mwakyembe.
 
Amesema, yeye kama mwanasheria hawezi kupeleka kitu kama hakijakamika, Amehoji kuwa kwa nini Hiyo Ripoti imehoji mlalamikaji peke yake ambaye ni Clouds lakini hakuna mahali RC Makonda alipohojiwa?
Hata hivyo Mwakyembe hakuzungumzia suala la Makonda kuikwepa kamati kila ilipomtafuta kumhoji!

Itakumbukwa Vizuri kuwa Mwakyembe huyuhuyu amewahi kuongoza kamati ya uchunguzi wa Kibunge kuchunguza suala la mkataba wa ufuaji umeme wa Richmondi, iliyopelekea kuondoka madarakani kwa Waziri Mkuu Mstaafu mheshimiwa Lowasa, Na kilio kikuu cha Mheshimiwa Lowasa ilikuwa ni kuwa kamati hiyohiyo ya Mwakyembe haikuwahi kumhoji mahali popote!.

Hii Hapa chini ni video ya Mwakyembe akizungumza hayo!
 
Attachments

  • 17582951_1832551060402322_4328833392301834240_n.mp4
    3.1 MB · Views: 46
Back
Top Bottom