Mwakyembe: Nipeni miezi Sita | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakyembe: Nipeni miezi Sita

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Oct 5, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  Hadija Jumanne na Deborah Ngajilo

  WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amesema wananchi wampe muda wa miezi sita ili aweze kukamilisha miundo mbinu katika sekta ya reli nchini.


  Dk Mwakyembe aliyasema hayo jana jijini Dar es salaam wakati akifungua mkutano wa pili wa wataalamu unaohusu Takwimu (Logistic) kwa Africa katika miundo mbinu.


  Mbali na kutoa muda huo, Dk Mwakyembe amekiri kuwapo kwa tatizo la usafiri hapa nchini na kuomba washiriki katika mkutano huo kutatua matatizo yanayoikumba sekta hiyo ikiwamo matumizi ya teknolojia mpya ya usafirishaji nchini, usambazaji wa mdogo wa chakula na Sekta ya Reli.


  Katika mkutano huo , Dk Mwakyembe alisema miezi sita inatosha kukamilisha ahadi ambayo aliitoa na kwamba hatua hiyo inatokana na wananchi kuhoji usafiri huo wa reli utaanza lini wakati Serikali ilitangaza usafiri huo utaanza Oktoba Mosi mwaka huu.

  “Nipeni muda wa miezi sita ili muweze kuona sekta ya reli itakavyokua imekamilika nchini, kwa kuwa sekta ya reli ni muhimu katika maendeleo ya nchi hivyo ni vyema tukaitengeneza ndani ya miezi hiyo kupitia wataalamu wetu,”alisema Dk Mwakyembe.

  “Tuacheni tufanye kazi na nyie endeleeni kutunga ngojera kuhusiana na usafiri wa reli lakini sisi tunajua tunachokifanya kwani niliposema usafiri wa reli unaanza mwezi Oktoba sikumaanisha utaanza Oktoba Mosi kwani hata Oktoba 15 ipo ndani ya mwezi huo huo,”.

  Alifafanua kwamba kwa sasa wameanza kung’oa reli na kuweka yenye uzito wenye paundi 95 ambao wanashirikiana na Benki kuu katika kubadilisha usafiri wa reli katika Mkoa wa Dodoma.


  Alisema lengo la mkutano huo ambao umehusisha mabingwa wa mfumo wa takwimu ni kujadili umuhimu wa usafirishaji hasa wa reli, mafunzo kwa wataalamu katika mambo ya miundo mbinu pamoja na usalama wa chakula na usafirishaji.


  Alisema ili soko liweze kuendelea vizuri linahitaji wasambazaji wawe na usafiri mzuri ikiwamo wa miundo mbinu mizuri ili kuwafikia watumiaji.


  Alisema mkutano huo utaongeza uzoefu kwa washiriki katika masuala ya miundo mbinu katika Afrika kwa kuwa sekta ya usafirishaji ni muhimu katika maendeleo ya uchumi dunia.


  Awali Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji nchini (NIT), Mhandisi Zacharia Mganilwa alisema lengo la mkutano huo ni kujadili jinsi ya kukabiliana na maafa yanayojitokeza kipindi cha maafa ya asili na shughuli za kibinadamu ikiwemo mafuriko.


  “Maafa ya asili ni kama mafuriko yanapotokea sehemu ambazo miundo mbinu mibovu husababisha misaada kushindwa kufika kwa wakati hivyo kama chuo kikishirikiana na wataalamu tunaweza kutatua matatizo haya na misaada au bidhaa kufika kwa wakati,”alisema Mhandisi Mganilwa.


  Mhandisi huyo alisema umuhimu wa kuwa na miundo mbinu ya reli katika kusafirisha mizigo lina hitaji kuwa na wataalamu ambao watasaidia katika kuondoa kero zinazotokea.


  Mkutano huo wa siku mbili umeandaliwa na Ubalozi wa Ujerumani ukishirikiana na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) ambapo zaidi ya nchi kumi kutoka nchi mbalimbali duniani zimeshiriki.

  Mwakyembe: Nipeni miezi Sita

  Mh. Waziri Mwakyembe Tunakupa hiyo miezi Sita Fanya vitu vyako kuhusu Reli ........
   
 2. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,319
  Likes Received: 2,605
  Trophy Points: 280
  Reli ikikaa sawa nina hakika sekta nyinginezo zitanyanyuka pia.
   
 3. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ...hii biashara ya kusema hata tar 15 ipo ndani ya oct, sijaipenda!...iko kiswahili na kichengachenga...
   
 4. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Mgema akisifiwa ............
   
 5. allantence

  allantence Senior Member

  #5
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 4, 2012
  Messages: 156
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  tusubir na tuone .
   
 6. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ila Waziri anatujua kwa ngonjera kumbe?
  Piga kazi mkuu, maneno hata kwenye khanga yapo tu.
   
 7. TZ yetu

  TZ yetu JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 369
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 60
  Unga wa ndele upo ndani ya damu za viongozi wetu........maana hiyo kauli ya kuwa hata 15 ni ndani ya oct cna hakika nayo.
   
 8. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,520
  Likes Received: 10,438
  Trophy Points: 280
  Siasa ndani ya siasa.
   
 9. m

  mamajack JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  hana lolote mwakyembe,magamba walishamaliza kazi.hiyo train ilikuwa ianza mwezi huu,lakini kimya mpaka leo kimya.
   
 10. Luno G

  Luno G JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 22, 2012
  Messages: 1,883
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  inabidi apatikane mtolewa awape unga wa rutuba
   
 11. Fyong'oxi

  Fyong'oxi JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Give him time!Yeye ni mtaalamu wa sheria tuu, ni lazima afanye kazi pia kwa kuzingatia ushauri wa wahandisi kuepusha maafa na Lawama! Be patient, vitu vizuri havitaki haraka za kisiasa!ni utaalamu pia unawekwa mbele
   
 12. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,132
  Trophy Points: 280
  Nakupa mwaka mzima, ila nataka ulete treni ya umeme
   
 13. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  tumpe muda reli iliyopo kwa kweli imechoka
  nimeona wakibadilisha tusubiri imalizike tusafiri kwa usalama na uhakika.
  ikitokea ajali tutakuwa wakwanza kulaumu kwanini aliruhusu tren kutumia miundo mbinu chakavu.
   
 14. m

  makeda JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 4, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Mi nafikiri reli iunganishiwe umeme ili kukomesha hawa wanaong'oa mataluma ya reli.ni hujuma kwa wananchi.
   
 15. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,800
  Likes Received: 2,571
  Trophy Points: 280
  Reli ipi? Reli ya kati, TAZARA au ya usafiri DAR? Maanake kuimarisha TAZARA na reli ya kati ndani ya miezi sita ni longo longo express!
   
Loading...