Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,522
- 24,010
Huyu bwana akuwahi kusikika hapo nyuma isipokuwa kwenye tukioa la Richmond ambapo alionekana kuwa ni shujaa sana. Mimi nakumbuka nilipenda sana kumfahamu huyu mtu ni nani kwa kipindi hicho akiwa kwenye kilele kisiasa.
Sasa amekuwa kama mpira wa makaratasi anapigwa huku na kule toka wizara moja kwenda nyingine na kila aendako anafanya vituko. Ni nani alimlaani Mwakyembe? Mwakyembe alijilaani yeye mwenyewe alipokubali kutumika na wanasiasa mbali mbali wakiwepo akina sitta, kikwete na wengine waliofuatia.
Baada ya hapo alichuja kwa haraka sana na mpaka sasa kutolewa kwenye uwaziri wa katiba na sheria kupelekwa kwenye uwaziri wa michezo, sanaa na habari ni mwendelezo wa yeye kuendelea kushindwa na kupoteza kabisa sifa azlizokuwa nazo miaka ile ya 2008-2009.
Kama ningekuwa yeye ningesema siasa basi. Ningepumzika kwa heshima. Najua anakoelekea ni kuja kupewa ukuu wa wilaya tu huko mbeleni. Najiuliza mwakyembe Mwakyembe umepatwa na nini?