wakuu habari za kazi. leo Kata ya ipinda wilayani kyela kuna hali tete mpaka muda huu, kuna wagombea kumi nafasi ya ubunge kupitia CCM akiwemo mwakyembe na Jana kampeni zilianza leo ikiwa ni mwendelezo Kata ya ipinda.
SAA 7 wakianzia Kata ya Muungano pale asubuh ambako Mh.Mwakyembe alizomewa na akasema wametumwa hao vijana.
ivyo ilipofika zamu ya Kata ya ipinda akagoma kufanyia hapo maana ndipo ngome ya CHADEMA ilipo ivo akataka mkutano ufanyikie lupaso ambako no mbali kidogo. ndipo wagombea wengine Tisa wakasusia mkutano huo. mpaka mda huu hakuna kinachoendelea zaidi ya malumbano.
tutapeana updates zaidi
Upande wa ccm kule kyela hakuna anayeweza kushindana na mwakyembe najua yeye ndio atasimamishwa kugombea ubunge na hakuna mgombea wa chadema anayeweza kumwangusha mwakyembe..
Mgiriki usimjdanganye Mwakyembe ili kumlia hela zame, wewe hukai kyela, Mwekyembe huku kwetu ni zilipendwa danganyaneni huko huko Dar
mkuu nilichokwambia ndio ukweli wa mambo....
Kama huniamin subir baada ya kura tutafutane,,.
...Ukwelii ndio huo. DR. H. M. Ni material ya kitaifaa..
Kuna wenzako walisema kama mtu wao akishindwa wauwawe,kua makini.
Upande wa ccm kule kyela hakuna anayeweza kushindana na mwakyembe najua yeye ndio atasimamishwa kugombea ubunge na hakuna mgombea wa chadema anayeweza kumwangusha mwakyembe..
Jamani huyu ndo waziri mkuu wetu mtarajiwa ati. Wana Kyela msituangushe tunawaomba sana.