leo katika mikutano miwili iliyofanyika jimboni kwake Mhe Mwakyembe amewaliza watu baada ya kuamua kuvua kofia yake na gloves na miwani waone jinsi alivyoathiliwa na sumu kali. Katika hotuba yake ametumia muda kuwasihi wananchi kuacha majungu badala yake wamuunge mkono ili amalizie kipindi chake cha uongozi. Hata hivyo hakutaja watu waliomdhuru lakini aliwashukuru wananchi kwa maombi yao na madaktari kwa juhudi zao katika kuokoa uhai wake.
Utashangaa sana!Mwakyembe hajaathirika na sumu. Hebu acheni majungu. Nashangaa sana mheshimiwa waziri anatembelea Kyela kisiasa wakati ana kazi ofisini, kwani yupo leave?
amesema asijadiliwe, then anavua kofia na gloves ili watu wamuhurumie, huyu jamaa ni MNAFIKI
Hila inabidi aache uzushi na yeye na kutafuta cheap publicity, tunasikia kapitia chemotherapy huko India, nadhani unaelewa effects zake temporarily if you dont ndio hizo ( na in most cases cancer is involved). Sasa aseme what is wrong with him or who poisoned him and for what? (afadhali hata Faiza Fox, alituonya mdomo wake na kesi ya visima anaweza na yeye akapewa discipline).Utashangaa sana!
Ukitaka kushangaa zaidi na kuacha mdomo wazi hadi inzi wajae mdomoni, nenda Arumeru, utakuta Mawaziri kibao wako huko kwa mwezi mzima na walishaweka makufuli maofisini kwao!
Kajichimbia kaburi mwenyewe hakuna haja ya kumuonea huruma.
Huyu nae amezidi unafiki,kama hana la kuongea ni bora awe silent forever,anapenda sana kuhurumiwa wakati na yeye ni fisadi khaa