Mwakyembe atengewa Sh. bilioni 500

Mwakyembe atengewa Sh. bilioni 500

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803

Thursday, March 28, 2013

Na Salome Kitomary

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imepitisha bajeti ya Wizara ya Uchukuzi, ambayo imetengewa zaidi ya Sh. bilioni 548; kwa ajili ya kushughulikia miradi ya maendeleo na matumizi ya kawaida, huku kipaumbele kikiwekwa katika ujenzi na uboreshaji wa viwanja vya ndege na usarifi wa reli, kwa mwaka mpya wa fedha wa 2013/2014.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Peter Serukamba, kati ya fedha hizo, Sh. bilioni 390. 5 zimetengwa kwa ajili ya kushughulikia miradi ya maendeleo, wakati Sh. bilioni 158.4,zimetengwa kwa matumizi ya kawaida.
Alisema kamati imepitisha bajeti ya wizara hiyo baada ya kuridhishwa nayo, kutokana na fedha nyingi kuelekezwa kwenye miradi ya maendeleo na kidogo kwenye matumizi mengine.

Serukamba, ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kukutana na viongozi na watendaji wa wizara hiyo, katika ofisi ndogo za Bunge, jijini Dar es Salaam jana.
Alisema katika fedha za maendeleo, Sh. bilioni 255.6 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa viwanja vya ndege na usarifi wa reli.

"Bajeti hii ni nzuri kwa kuwa fedha nyingi zimeelekezwa kwenye miradi ya maendeleo. Tofauti na miaka iliyopita fedha zilielekezwa kwenye matumizi ya kawaida. Matumaini yetu ni uboreshaji wa miradi husika," alisema Serukamba.

Alisema pia Sh. bilion 12 zimetengwa kwa ajili ya kuwalipa wafanyakazi wastaafu wa Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara) waliokuwa wanaidai serikali kwa muda mrefu.

Vilevile, alisema katika bajeti hiyo, zaidi ya Sh bilioni 86 zitaelekezwa kwenye upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kituo cha tatu (teminal three).

Alisema katika mwaka wa fedha uliopita, kamati yake ilitoa mapendekezo mbalimbali, ambayo yameanza kufanyiwa kazi, ikiwamo upanuzi wa bandari, ujenzi wa magati katika ziwa Nyasa, Victoria na Tanganyika.

Kwa mujibu wa Serukamba, mengine ni matengenezo ya meli katika ziwa Nyasa, Victoria na Tanganyika na uboreshaji wa usafiri wa treni za jijini Dar es Salaam, kwa kununua za kisasa kwani zilizopo zimepitwa na wakati.

"Usafiri wa Treni ni moja ya mapendekezo yetu. Na serikali imelifanyia kazi. Lakini tumeitaka kuboresha zaidi kwa kununua treni ya kisasa na si zilizopitwa na wakati," alisema Serukamba.

Alisema yote yamefanyiwa kazi na kinachopaswa ni usimamizi thabiti kuhakikisha fedha zilizoelekezwa kwenye maeneo hayo zinatumika inavyotakiwa.

Hata hivyo, aliitaka serikali kupeleka asilimia 55 ya fedha za bajeti kwa mwaka uliopita ya wizara hiyo ili kuiwezesha kutekeleza majukumu iliyojiwekea kwa mwaka huo.

Alisema ikiwa imebaki miezi mitatu mwaka wa fedha wa 2012/13 kumalizika, asilimia 25 ya fedha za ndani na asilimia 30 ya fedha za nje ndizo zimepelekwa wizarani humo.

"Tunaitaka serikali kulipa fedha za mwaka jana ili miradi ya maendeleo ya mwaka jana isikwame, imepita miezi tisa, Wizara haijapata fedha zote kutoka Wizara ya Fedha, imebaki miezi mitatu kumaliza mwaka wa bajeti, haya ni mapungufu" alisema
Kamati hiyo leo itaendelea na mapitio ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka 2012/13 na
2013/14.

at 5:04 AM - Source VIJIMAMBO

Bora angalau kwake yeye tunaona pesa zinakwenda wapi... yeah tunahitaji Mabehewa Mazuri ndani ya JIJI...
 
Bora angalau kwake yeye tunaona pesa zinakwenda wapi... yeah tunahitaji Mabehewa Mazuri ndani ya JIJI...

Mkuu hutaona chochote manake hata mwaka jana bajeti ilikuwa na mabilioni kibao lakini unaona waziri analalamika kupokea chini ya 50%. Hali ilikuwa hivyo mwaka wa jana na huenda itakuwa hivyo mwaka kesho!

Bajeti za siku hizi ni usanii mtupu, utasikia trioni 17 lakini mwisho wa mwaka wanasema trion 11 ndo zilipelekwa kwenye wizara zetu!

Je kwanini tusiwe tunasema bajeti ni trioni 11 tokea mwanzo?
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Wamesema ya Mwaka Jana waliipunguza... hawakumpa iliyoombwa kama nimesoma vizuri hii habari
 
nivizuri ukawa na uhakika kabla hujapost.

Mkuu hutaona chochote manake hata mwaka jana bajeti ilikuwa na mabilioni kibao lakini unaona waziri analalamika kupokea chini ya 50%. Hali ilikuwa hivyo mwaka wa jana na huenda itakuwa hivyo mwaka kesho!

Bajeti za siku hizi ni usanii mtupu, utasikia trioni 17 lakini mwisho wa mwaka wanasema trion 11 ndo zilipelekwa kwenye wizara zetu!

Je kwanini tusiwe tunasema bajeti ni trioni 11 tokea mwanzo?
 
Bajeti Tanzania ni changa la macho, kinachotangazwa Bungeni ni tofauti kabisa na kile kinachofikishwa Mawizarani, ikifika August/September unasikia baadhi ya Wafanyakazi mishahara mpaka tarehe 57. Unajiuliza jamani mwaka mpya wa fedha si ndio umeanza miezi miwili iliyopita!? Iweje Wafanyakazi waanze kukosa mishahara ndani ya miezi miwili ya mwaka mpya wa fedha!? Chezeya Serikali ya kisanii weye!!!

Back
Top Bottom