Mwakyembe Ataka Mdahalo na akina Rostam

Hizi zote ni kelele tu za kuelekea kwenye majimbo ya uchaguzi hakuna kipya. Nchi kimaadili ya uongozi iko taabani. Nakumbuka wakati taarifa hii (Richmond) inatolewa kwa mara ya kwanza pale bungeni nilijua sasa nchi imeamka ki maadili. Lakini kumbe si lolote si chochote tuko palepale.

Kelele zote tunazopiga ni sawa na za mbwa asiye na kucha wala meno, inashangaza kuona jinsi serikali inavyocheka na wezi huku ikiwa imetumia pesa za walipa kodi wa nchi hii kutafuta habari ambayo baada ya ukweli kujulikana hakuna hatua yoyote iliyo na inayo chukuliwa, huu ni usaliti dhidi ya ustaarabu kimaadili ya uongozi.
 
Hivi jamani naomba kuuliza.... Mbunge ni nani na anapaswa kufanya nini kama mbunge?
 
Rostam hawezi kukubali mdahalo maana anajua kitakachomshukia huko. Atapiga porojo kupitia waandishi wa habari tu, ambao atawapa kodogodogo ili wachapie zaidi story ionekane kumfaa yeye zaidi. Sifa ya ufisadi weacha tu. Wamebobea.

Leka
 
Kama ameona hayajafanyiwa kazi basi ngoma ni 0-0.A seti mambo mengine kwenye mtandao(Achague ustarabu mwingine).watu tumechoka sasa na hizi ngongera.mpaka wapiga kura wake wanamwita amefulia.Sasa yeye atakaa hapo hapo na ngongera zake akisubiri mambo yafanyiwe kazi?.Ndiyo kufilisika kwenyewe.

Sweeping statements hazifai! Wapigakura wa Kyela si wote wanaoweza kumwita ama kumwambia 'mpiganaji'/Mbunge wao 'amefulia'. Mwakyembe amedhihirisha kwa vitendo kwamba anao uchungu wa dhati wa nchi yake. Mwakyembe ana guts ambazo wengi humu JF na nje ya JF hatuna. Vile vile naamini kabisa kwamba hata kama Mwakyembe hatakuwa Mbunge, popote atakapokuwa ataendelea kuwa 'mpiganaji' na mkereketwa wa nchi hii.

Laiti mngeliona alivyoshangiliwa na ukumbi mzima pale Karimjee hall wakati anataka huo mdahalo na Rostam mngelijua jinsi ambavyo wananchi wamechoshwa na yote yanayoendelea nchini. Kongamano lililoandaliwa na MNF ni kongamano la aina yake ambalo lilihudhuriwa na watu wa aina zote. Walikuwepo wazee wa nchi hii - akina Job Lusinde, Edwin Mtei, Ndejembi, Mwakawago, vijana akina Nape, Maaskofu, Masheikh, Viongozi wa Vyama vya Siasa, Maprofesa akina Baregu, Shivji na wasomi kadha wa kadha, viongozi wa Serikali kama Hawa Ghasia aliyeharibu hali ya hewa, Mkuchika naye alihudhuria siku ya mwisho. Walikuwepo wananchi wa kawaida kutoka Dar es Salaam na vitongoji vyake halikadhalika walikuwepo waliosafiri kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania wakiwemo wajasiriamali kutoka maeneo kama Maswa Shinyanga walioamua kuja kwenye Kongamano baada ya kusikia kwenye vyombo vya habari kwamba kuna Kongamano hilo linahusu Mustakabali wa Taifa,n.k, n.k. Watu kutoka makundi yote hayo walipata nafasi ya kuzungumza na wote walizingumzia matatizo ya mmomonyoko wa maadili na kukiukwa kwa misingi mizuri walituwekea waasisi wa taifa hili, Hiyo ilidhihirisha ni jinsi gani wananchi wengi wanaona hali ya nchi yao ilivyo na jinsi walivyochoka kuona hali hiyo ikiendelea.

Kuwakandia wale wanaojaribu kupigania kuinusuru nchi yetu kutokana na janga linalotunyemelea litakaloletwa na mmomonyoko wa maadili, ni sawa na kuisaliti nchi yetu. Whatever the style, kama lengo ni kutaka tufike kule kunakodhamiriwa sioni sababu yoyote ya kuwakatisha tamaa wanaojaribu kuthubutu. Tabia ya kukandia wengine wanaojitokeza kusema haijengi bali inazidi kubomoa na inadhahirisha kwamba hatuna nia ya dhati ya kutaka kurekebisha matatizo yaliyopo nchini.
 
MBUNGE wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM), ametaka kuitishwa kwa mdahalo wa wazi wa saa tatu katika kituo chochote cha televisheni kati ya wajumbe wa iliyokuwa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza utata katika mkataba wa Richmond na watuhumiwa wa kashfa hiyo wanaolalamika kuonewa. Mwakyembe ambaye alikuwa mwenyekiti wa kamati hiyo teule ya Bunge alitoa wito huo wa aina yake jana wakati akichangia mada kwenye kongamano la kumbukumbu ya miaka 10 tangu kufa kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere linaloendelea leo jijini Dar es Salaam.

Katika hali inayoweza kuibua maswali na mjadala, Mwakyembe ambaye ni daktari wa falsafa katika taaluma ya sheria, alisema baada ya mdahalo huo, washiriki wote watapaswa kupita Kariakoo kupima maoni ya wananchi kuhusu ukweli wa sakata hilo.

Bila ya kumtaja jina, mwanasiasa huyo alieleza kushangazwa na hoja za Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz za kutaka kuundwa kwa tume ya majaji kuchunguza ripoti ya Richmond akisema suala hilo halina sababu ya kuchukua mkondo huo.

“Nawashauri wanunue ‘airtime’ kwa sababu wana pesa… wao wake upande huu na sisi (yaani Kamati ya Kudumu ya Bunge iliyochunguza mkataba dhalimu wa Richmond), tukae upande mwingine. Hapo kila upande utoe hoja zake halafu tuwaachie wananchi watuhukumu kwa haki, tukitoka hapo tupite Kariakoo tuone kama watarudi na nguo za ndani,” alisema.

Mbunge huyo alisema pia kwamba, kuyumba kwa serikali iliyopo madarakani kunatokana na viongozi kutokubali kuwajibika, ikiwa ni pamoja na kushindwa kuchukua maamuzi magumu hali inayotokana an mmomonyoko wa maadili.

“Tatizo la viongozi wetu kushindwa kuchukua maamuzi magumu ni mmomonyoko wa maadili. Siku hizi kiongozi kukiri kosa anaonekana amefulia. Enzi za Mwalimu kiongozi kujiuzulu ilikuwa ni heshima sana.
“Mheshimiwa Mwenyekiti, viongozi wetu hawana ‘political responsibility’, wamejiuzulu lakini hadi leo wanalia wamekosa ‘dili’. Wameanzisha magazeti kwa ajili ya kumtukana Spika wa Bunge na wajumbe wa kamati teule. Hawa watu wanazo hela hawa, sasa mimi nawashauri watumie fedha zao kununua airtime tujadili hoja,” alisema.

Aidha, mbunge huyo, alimtaka Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na timu yake kujiuzulu ili kuonyesha uwajibikaji kutokana na kulidanganya taifa kuhusu mkataba wa Richmond.

Alisema, taasisi hiyo imelitia aibu taifa kwa kufunika uoza uliokuwepo kwenye mkataba wa kampuni hewa ya kufua umeme ya Richmond.
Mwaka 2007, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Edward Hoseah, alizungumza na vyombo vya habari baada ya kukamilisha uchunguzi uliofanywa na taasisi hiyo na kueleza kwamba kulikuwa hakuna ushahidi wa kufanyika kwa makosa ya rushwa katika mkataba uliosainiwa kati ya Shirika la Umeme (TANESCO) kwa niaba ya serikali na wamiliki wa kampuni hiyo.

Awali, akizungumza katika kongamano hilo jana, Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, alisema wakati wa viongozi kuchukua maamuzi magumu katika kashfa mbalimbali zikiwamo zile za Richmond, Kagoda na Deep Green umefika.

Aidha, alibainisha kwamba tatizo la ufisadi ambalo taifa linakabiliana
nalo hivi sasa, linasababishwa na namna viongozi wa taifa hili wanavyopatikana kwa njia ya kuwanunua wananchi maskini.

Kwa upande wake, Dk. Salim ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere iliyoandaa kongamano hilo, alisema rushwa katika nchi hii haitamalizika kwa msimamo wa chama ama serikali pekee, bali ni kwa Watanzania wote kuikataa kwa vitendo.

Hata hivyo, alisema suala hilo ni gumu iwapo wananchi wataendelea kubaki kwenye umaskini walionao na akaitaka TAKUKURU kuitikia wito uliotolewa kwao na Rais Jakaya Kikwete wa kuitaka ifanye kazi kwa haki.

Dk. Salim alibainisha kwamba hivi sasa taifa limeelemewa na matatizo mengi, yakiwamo chuki, mauaji ya kinyama, ubaguzi, siasa chafu, udini na vitendo vya watu fulani kujiona kuwa ni wazalendo kuliko wengine.

“Baada ya miaka 10 ya kuondokewa na Baba wa Taifa letu, kuna mambo mengi yametokea na yanayoendelea kutokea katika nchi yetu. Mambo ambayo yanatutaka sisi kama wadau wa taifa hili kuwa na uthubutu na ujasiri wa kuanzisha mchakato wa kujitazama, kujichunguza na kukubaliana jinsi gani tunaweza kujinasua katika matatizo ambayo kama yakipuuzwa yanaweza kugeuka majanga na kuliweka taifa letu mahali pabaya,” alisema.

Naye Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, alisema Watanzania wamekiuka ahadi yao kwa Mwalimu Nyerere ya kuenzi kwa vitendo mambo yote aliyoyasimamia hali inayosababisha taifa kufika lilipo sasa.

Alisema mfumo wa utawala na kuporomoka kwa maadili miongoni mwa viongozi, unakaribisha wakoloni wapya kuingia Tanzania, hasa kutokana na kushindwa kuzuia rushwa. “Kuna hatari ya Tanzania kuja kutawaliwa tena iwapo hatutaondokana na rushwa kwa matendo…”

Kongamano hilo la siku tatu linatarajiwa kumalizika leo ambapo viongozi mbalimbali wa kitaifa, wabunge, mabalozi, wanazuoni, viongozi wa dini, wanajeshi wakuu wastaafu na wanaharakati kutoka sehemu mbalimbali nchini wanashiriki.
Source: Tanzania Daima Dec 02, 2009.

Kwani ni lazima huo mjadala uwe kwenye media?si wakakae huko wabishane?si tunataka kuona ufumbuzi wa tatizo inapatikana na si ushindani wakujenga hoja
 
FMES,

Karibu Kyela uje umsaidia Dr. Mwakyembe kwenye kampeni yake.

Ila jiandae maana kwa yale ninayoyaona hapa Kyela, mpambano utakuwa mkali sana kwake.

Pia mshauri jamaa yako atumie muda wake kuongelea maendeleo ya Kyela pia, Richmond, Richmond kila siku haitamsaidia.

Wenzake wanafanya mambo ya maana huku kimya kimya na yanaonekana. Itakuwa ngumu sana kwake kuwaambia wawaache hao wengine waendelee kumwamini yeye ambaye huku tunamwita mbunge wa taifa au msanii.

- Heshima yako mkuu, sina urafiki naye, isipokuwa ninasuuzika sana anapotoa hoja on masilahi ya taifa, kuhusu Kyela labda utuwekee tu mapungufu yake hapa mimi ninamuheshimu sana kwenye masilahi ya taifa tu ya Kyela sijui!

Respect.

FMEs!
 
Sweeping statements hazifai!

Kuwakandia wale wanaojaribu kupigania kuinusuru nchi yetu kutokana na janga linalotunyemelea litakaloletwa na mmomonyoko wa maadili, ni sawa na kuisaliti nchi yetu. Whatever the style, kama lengo ni kutaka tufike kule kunakodhamiriwa sioni sababu yoyote ya kuwakatisha tamaa wanaojaribu kuthubutu. Tabia ya kukandia wengine wanaojitokeza kusema haijengi bali inazidi kubomoa na inadhahirisha kwamba hatuna nia ya dhati ya kutaka kurekebisha matatizo yaliyopo nchini.

- Haya ni maneno mazito sana katika kujali masilahi ya taifa, it cool na I am down mkuu!

Respect.


FMEs!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom