Mwakyembe Ataka Mdahalo na akina Rostam

Obi

JF-Expert Member
Jul 6, 2009
374
79
MBUNGE wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM), ametaka kuitishwa kwa mdahalo wa wazi wa saa tatu katika kituo chochote cha televisheni kati ya wajumbe wa iliyokuwa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza utata katika mkataba wa Richmond na watuhumiwa wa kashfa hiyo wanaolalamika kuonewa. Mwakyembe ambaye alikuwa mwenyekiti wa kamati hiyo teule ya Bunge alitoa wito huo wa aina yake jana wakati akichangia mada kwenye kongamano la kumbukumbu ya miaka 10 tangu kufa kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere linaloendelea leo jijini Dar es Salaam.

Katika hali inayoweza kuibua maswali na mjadala, Mwakyembe ambaye ni daktari wa falsafa katika taaluma ya sheria, alisema baada ya mdahalo huo, washiriki wote watapaswa kupita Kariakoo kupima maoni ya wananchi kuhusu ukweli wa sakata hilo.

Bila ya kumtaja jina, mwanasiasa huyo alieleza kushangazwa na hoja za Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz za kutaka kuundwa kwa tume ya majaji kuchunguza ripoti ya Richmond akisema suala hilo halina sababu ya kuchukua mkondo huo.

“Nawashauri wanunue ‘airtime’ kwa sababu wana pesa… wao wake upande huu na sisi (yaani Kamati ya Kudumu ya Bunge iliyochunguza mkataba dhalimu wa Richmond), tukae upande mwingine. Hapo kila upande utoe hoja zake halafu tuwaachie wananchi watuhukumu kwa haki, tukitoka hapo tupite Kariakoo tuone kama watarudi na nguo za ndani,” alisema.

Mbunge huyo alisema pia kwamba, kuyumba kwa serikali iliyopo madarakani kunatokana na viongozi kutokubali kuwajibika, ikiwa ni pamoja na kushindwa kuchukua maamuzi magumu hali inayotokana an mmomonyoko wa maadili.

“Tatizo la viongozi wetu kushindwa kuchukua maamuzi magumu ni mmomonyoko wa maadili. Siku hizi kiongozi kukiri kosa anaonekana amefulia. Enzi za Mwalimu kiongozi kujiuzulu ilikuwa ni heshima sana.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, viongozi wetu hawana ‘political responsibility’, wamejiuzulu lakini hadi leo wanalia wamekosa ‘dili’. Wameanzisha magazeti kwa ajili ya kumtukana Spika wa Bunge na wajumbe wa kamati teule. Hawa watu wanazo hela hawa, sasa mimi nawashauri watumie fedha zao kununua airtime tujadili hoja,” alisema.

Aidha, mbunge huyo, alimtaka Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na timu yake kujiuzulu ili kuonyesha uwajibikaji kutokana na kulidanganya taifa kuhusu mkataba wa Richmond.

Alisema, taasisi hiyo imelitia aibu taifa kwa kufunika uoza uliokuwepo kwenye mkataba wa kampuni hewa ya kufua umeme ya Richmond.

Mwaka 2007, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Edward Hoseah, alizungumza na vyombo vya habari baada ya kukamilisha uchunguzi uliofanywa na taasisi hiyo na kueleza kwamba kulikuwa hakuna ushahidi wa kufanyika kwa makosa ya rushwa katika mkataba uliosainiwa kati ya Shirika la Umeme (TANESCO) kwa niaba ya serikali na wamiliki wa kampuni hiyo.

Awali, akizungumza katika kongamano hilo jana, Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, alisema wakati wa viongozi kuchukua maamuzi magumu katika kashfa mbalimbali zikiwamo zile za Richmond, Kagoda na Deep Green umefika.

Aidha, alibainisha kwamba tatizo la ufisadi ambalo taifa linakabiliana
nalo hivi sasa, linasababishwa na namna viongozi wa taifa hili wanavyopatikana kwa njia ya kuwanunua wananchi maskini.

Kwa upande wake, Dk. Salim ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere iliyoandaa kongamano hilo, alisema rushwa katika nchi hii haitamalizika kwa msimamo wa chama ama serikali pekee, bali ni kwa Watanzania wote kuikataa kwa vitendo.

Hata hivyo, alisema suala hilo ni gumu iwapo wananchi wataendelea kubaki kwenye umaskini walionao na akaitaka TAKUKURU kuitikia wito uliotolewa kwao na Rais Jakaya Kikwete wa kuitaka ifanye kazi kwa haki.

Dk. Salim alibainisha kwamba hivi sasa taifa limeelemewa na matatizo mengi, yakiwamo chuki, mauaji ya kinyama, ubaguzi, siasa chafu, udini na vitendo vya watu fulani kujiona kuwa ni wazalendo kuliko wengine.

“Baada ya miaka 10 ya kuondokewa na Baba wa Taifa letu, kuna mambo mengi yametokea na yanayoendelea kutokea katika nchi yetu. Mambo ambayo yanatutaka sisi kama wadau wa taifa hili kuwa na uthubutu na ujasiri wa kuanzisha mchakato wa kujitazama, kujichunguza na kukubaliana jinsi gani tunaweza kujinasua katika matatizo ambayo kama yakipuuzwa yanaweza kugeuka majanga na kuliweka taifa letu mahali pabaya,” alisema.

Naye Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, alisema Watanzania wamekiuka ahadi yao kwa Mwalimu Nyerere ya kuenzi kwa vitendo mambo yote aliyoyasimamia hali inayosababisha taifa kufika lilipo sasa.

Alisema mfumo wa utawala na kuporomoka kwa maadili miongoni mwa viongozi, unakaribisha wakoloni wapya kuingia Tanzania, hasa kutokana na kushindwa kuzuia rushwa. “Kuna hatari ya Tanzania kuja kutawaliwa tena iwapo hatutaondokana na rushwa kwa matendo…”

Kongamano hilo la siku tatu linatarajiwa kumalizika leo ambapo viongozi mbalimbali wa kitaifa, wabunge, mabalozi, wanazuoni, viongozi wa dini, wanajeshi wakuu wastaafu na wanaharakati kutoka sehemu mbalimbali nchini wanashiriki.

Source: Tanzania Daima Dec 02, 2009.
 
Ninachokifahamu ni kuwa MNF ilikuwa na "mgombea" wake, Dr SAS. Maneno makali wanayoyatoa kwenye kongamano lao hili ni muendelezo tu wa yale tuliyoyasikia mwaka 2005. Vinginevyo wafanye kweli, waondoke CCM.
 
mdahalo sidhani kama unaweza kusaidia kitu...............ukweli upo wazi kuwa lowasa na rostam walijiundia kampuni hewa wakijua sasa nchi ni yao na hawatajulikana wakaipa jina la RichMond(yaani Richard(mtoto wa lowasa) from Monduli(kwao lowasa)) hata pesa zilikuwa zinaingia kwenye akaunti za rostamu hata address walikuwa wanatumia ya rostamu hata mawasiliano na maagizo yote yalipitia kwa rostamu...pamoja na hayo yote rais alijua kinachoendelea na diri zima ndio maana hawezi kuwawajibisha wahusika na hajawahi kusikika akiongea kwa uchungu na kujuta kuwa richmond ilikuwa ni kampuni ya kinyonyaji........nnacho muomba mwakyembe atoboe ile siri aliyosema akiitoa serikali itatikisika kwa haraka haraka uaona kuwa kati ya watu wa ngazi za juu ambae hakuguswa ni rais..............
 
Mpiganaji huyu! Mwakyembe hatutaki midahalo! wewe si una hakika kuwa hao wezi wapelekeni mahakamani, kama hutaki au utasema ni jukumu la wengine kaa kimya!

CCM bwana wanawachota watu kiakili, anachozungumza hapa Mwayembe ni pumba tupu, samahani washabiki wake, wengi wetu hatuna uwezo wala pa kuanzia kuwapeleka hawa watu mahakamani!

Mwakyembe si mbunge tu bali pia mwanasheria mahiri, kama tatizo pesa we itisha mchango kuwa unataka pesa za kuendeshea kesi uone kama hautachangiwa

Kama swala ni kuongea watu wameshaongea mwaka wa tano sasa! hatujaona fisadi wakienda jela na kurudisha mali ya watanzania! yet Mwakyembe needs a debate

Hii inaashiria hata yeye hawawezi hawa jamaa!

Siogopi kusema kjuwa what going on now ni mbinu ya CCM kuchota akili za watanzania wengi, wanaofurahia tu wakisikia RA fisadi, basi mtu anasuuzika moyo Rostam fisadi! hii hulka ya magazeti ya akina Shigongo imewafanya CCM wafanye watakavyo, waongee chochote, watu wakiamini kuwa CCM wanagombana!

Mwakyembe ili apitishwe kuwa mgombea ubunge wa CCM Kyela hao hao akina Rostam wanakaa kumpitisha! AKILI MUKICHWA!

Tapeli la karne hili!! kulialia na kutaka kupendwa na watu!
 
haya ni mawazo finyu sana, test tube way of thinking, ina maana kwa kuwa walikuwa na mtu wao hawaruhusiwi kukemea pale nchi inapoyumba? nchi inaangamia na watu kama wewe wako kwenye lindi la usingizi mzito wa chagua la Mungu yaani kikwete
 
IKifikia mpaka Dr anawaza midahalo, tusio ma DR. tutawaza nini? sio ndio akina nani wale wananunua PhD kwa sababu hizi hizi! hawaoni tofauti!
 
Watu wazima kama wale( wengi wao wako above 70) hawawezi kusema kuwa Nchi imeanza kuyumba leo. Mzee Mwinyi ameunda serikali mara nne katika miaka 10 alookuwa madarakani tena na akina Warioba. Mkapa alifanya kiburi tu kutounda serikali yake zaidi ya mara mbili za kawaida.
Wazee hawa baada ya kuwa watazamaji wamekuwa mbogo kwelikweli. Waondoke CCM.
 
we unadhani ni PhD unazozifahamu...hizi zingine ni zile Pure Head Damage.
IKifikia mpaka Dr anawaza midahalo, tusio ma DR. tutawaza nini? sio ndio akina nani wale wananunua PhD kwa sababu hizi hizi! hawaoni tofauti!
 
Mpiganaji huyu! Mwakyembe hatutaki midahalo! wewe si una hakika kuwa hao wezi wapelekeni mahakamani, kama hutaki au utasema ni jukumu la wengine kaa kimya!

CCM bwana wanawachota watu kiakili, anachozungumza hapa Mwayembe ni pumba tupu, samahani washabiki wake, wengi wetu hatuna uwezo wala pa kuanzia kuwapeleka hawa watu mahakamani!

Mwakyembe si mbunge tu bali pia mwanasheria mahiri, kama tatizo pesa we itisha mchango kuwa unataka pesa za kuendeshea kesi uone kama hautachangiwa

Kama swala ni kuongea watu wameshaongea mwaka wa tano sasa! hatujaona fisadi wakienda jela na kurudisha mali ya watanzania! yet Mwakyembe needs a debate

Hii inaashiria hata yeye hawawezi hawa jamaa!

Siogopi kusema kjuwa what going on now ni mbinu ya CCM kuchota akili za watanzania wengi, wanaofurahia tu wakisikia RA fisadi, basi mtu anasuuzika moyo Rostam fisadi! hii hulka ya magazeti ya akina Shigongo imewafanya CCM wafanye watakavyo, waongee chochote, watu wakiamini kuwa CCM wanagombana!

Mwakyembe ili apitishwe kuwa mgombea ubunge wa CCM Kyela hao hao akina Rostam wanakaa kumpitisha! AKILI MUKICHWA!

Tapeli la karne hili!! kulialia na kutaka kupendwa na watu!
Dr Mwakyembee una walakini sanaa na kauli zako..Nahisi alichelewaa kupata umaarufuu kwa hiyoo sasa anautafuta kwa kila namna..

Huyu ni msomi, kiongozi tena mwenye hadhi katika jamii lakini amekuwaa mtu wakulialia tuuuuuuuuuu...

Tunatambuaa kamati ile ndo imekujenga zaidi kisiasa na huenda ikakubomoaa piaa kisiasa...
 
Huyu naye aache ushamba wake, anang'ang'ania TOPIC moja tuuuuu kama Mrema na dhahabu alizokamata Airport? sio nukalie SINGLE moja, TOA ALBUM baba......

Ukiona umaarufu unapungua unamwagilia maji, kwani hiyo kamati ulifanya kazi wewe peke yako??? au kwakuwa inaitwa YAMWAKYEMBE????
 
Mpiganaji huyu! Mwakyembe hatutaki midahalo! wewe si una hakika kuwa hao wezi wapelekeni mahakamani, kama hutaki au utasema ni jukumu la wengine kaa kimya!

CCM bwana wanawachota watu kiakili, anachozungumza hapa Mwayembe ni pumba tupu, samahani washabiki wake, wengi wetu hatuna uwezo wala pa kuanzia kuwapeleka hawa watu mahakamani!

Mwakyembe si mbunge tu bali pia mwanasheria mahiri, kama tatizo pesa we itisha mchango kuwa unataka pesa za kuendeshea kesi uone kama hautachangiwa

Kama swala ni kuongea watu wameshaongea mwaka wa tano sasa! hatujaona fisadi wakienda jela na kurudisha mali ya watanzania! yet Mwakyembe needs a debate

Hii inaashiria hata yeye hawawezi hawa jamaa!

Siogopi kusema kjuwa what going on now ni mbinu ya CCM kuchota akili za watanzania wengi, wanaofurahia tu wakisikia RA fisadi, basi mtu anasuuzika moyo Rostam fisadi! hii hulka ya magazeti ya akina Shigongo imewafanya CCM wafanye watakavyo, waongee chochote, watu wakiamini kuwa CCM wanagombana!

Mwakyembe ili apitishwe kuwa mgombea ubunge wa CCM Kyela hao hao akina Rostam wanakaa kumpitisha! AKILI MUKICHWA!

Tapeli la karne hili!! kulialia na kutaka kupendwa na watu!

Kaka, i beg to differ. Kabla sijaandika zaidi naomba nikueleze hili, you hate CCM to much kiasi ambacho hutaweza kuangalia na kuchambua vizuri jambo hili.

Kesi yeyote ya jinai, mlalamikaji ni Jamhuri na si mtu binafsi au Taasisi. Mtu au Taasisi au kikundi cha watu kinaweza kwenda polisi, bungeni, pccb nk ili kuomba wahusika wachukue hatua za kulalamika mahakamani. Kamati ya bunge ilifanya kazi yake kwa kupeleka taarifa bungeni. Hiyo ndo ilikuwa kazi yao. Kwasasa wanajiunga nasisi kupiga kelele (pressure group) ili Serikali ichukue hatu.

Hakuna ukweli wowote kwamba kila mwanaCCM hafai kusikilizwa mawazo yake au hana mchango wa kuleta mageuzi ya kisiasa. wapo akina Butiku, ninazo heshma kubwa sana kwa watu kama Seleli nk.

Suala la Dr. Mwakyembe kutokumweza Rostam lipo wazi. Kwani nani anamweza Rostam? Jamaa ameteka dola, sasa utamweza vipi?
 
.

Sasa kama anajua hamwezi analialia nini?Jaji Warioba amewaeleza kwa kirefu '' kuwa haoni sababu kwa Watanzania kuendelea na mjadala kuhusu Richmond akisema kwamba, watuhumiwa wa kashfa hiyo, wakiwamo baadhi ya mawaziri pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa waliwajibika kwa kujiuzulu na pia, Baraza la Mawaziri lilivunjwa.''Au mnataka Rais awajibike?,” alihoji Jaji Warioba na kuongeza kuwa wanaoshikia bango suala hilo wanatafuta njia ya kupata madaraka.''
Huo ndiyo ushamba wa mwakyembe.yeye ni richard monduli tu, richard monduli mpaka lini?.
 
Webeloya kumbuka yale ni mawazo yake na sio msimamao wa chama wala kikundi chochote,sasa unaposema hatutaki mdahalo huoni kuwa nawe wew ni wazo lako na usingelisema kama Mwakyembe asingetoa iyo hoja.
Jamani jaribuni kuwa critical kidogo otherwise mtaonekana mnatapika kwa kuto amjibu ya jazba
 
.

Sasa kama anajua hamwezi analialia nini?Jaji Warioba amewaeleza kwa kirefu '' kuwa haoni sababu kwa Watanzania kuendelea na mjadala kuhusu Richmond akisema kwamba, watuhumiwa wa kashfa hiyo, wakiwamo baadhi ya mawaziri pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa waliwajibika kwa kujiuzulu na pia, Baraza la Mawaziri lilivunjwa.''Au mnataka Rais awajibike?,” alihoji Jaji Warioba na kuongeza kuwa wanaoshikia bango suala hilo wanatafuta njia ya kupata madaraka.''
Huo ndiyo ushamba wa mwakyembe.yeye ni richard monduli tu, richard monduli mpaka lini?.

Warioba alimweza Rostm lini? Warioba amekubali yaishe. Endapo Rostam na Lowasa wangekubali na kuruhusu hatua zaidi kuchukuliwa wala kusingekuwa na tatizo kila mmoja angebaki kimya.

Hawa jamaa wameunda mtandao wa kuwasafisha na kuikandia kamati ya bunge. Sasa tuwaache waendelee kufanya hayo?

By the way, maamuzi ya bunge bado hayajatekelezwa.
 
mdahalo sidhani kama unaweza kusaidia kitu...............ukweli upo wazi kuwa lowasa na rostam walijiundia kampuni hewa wakijua sasa nchi ni yao na hawatajulikana wakaipa jina la RichMond(yaani Richard(mtoto wa lowasa) from Monduli(kwao lowasa)) hata pesa zilikuwa zinaingia kwenye akaunti za rostamu hata address walikuwa wanatumia ya rostamu hata mawasiliano na maagizo yote yalipitia kwa rostamu...pamoja na hayo yote rais alijua kinachoendelea na diri zima ndio maana hawezi kuwawajibisha wahusika na hajawahi kusikika akiongea kwa uchungu na kujuta kuwa richmond ilikuwa ni kampuni ya kinyonyaji........nnacho muomba mwakyembe atoboe ile siri aliyosema akiitoa serikali itatikisika kwa haraka haraka uaona kuwa kati ya watu wa ngazi za juu ambae hakuguswa ni rais..............

Yaonekana mpwa leo una hasira na RichMonduli teh teh

Mwakyembe akito ile siri wewe umejipanga vipi mpwa una passport ya iloiukifika huko uombe kibari cha polotical Asylum? maana hapato kalika hapa mkuu kaa ujue hilo. kwa wanao lijua ndio maana wamekaa kimyaaa

Huyu naye aache ushamba wake, anang'ang'ania TOPIC moja tuuuuu kama Mrema na dhahabu alizokamata Airport? sio nukalie SINGLE moja, TOA ALBUM baba......

Ukiona umaarufu unapungua unamwagilia maji, kwani hiyo kamati ulifanya kazi wewe peke yako??? au kwakuwa inaitwa YAMWAKYEMBE????

wewe naye pumbafu tu
 
Kama swala ni kuongea watu wameshaongea mwaka wa tano sasa! hatujaona fisadi wakienda jela na kurudisha mali ya watanzania! yet Mwakyembe needs a debate

Wanasiasa ndivyo walivyo --- THEY DON'T SAY WHAT THEY MEAN, THEY DON'T MEAN WHAT THEY SAY
 
haya ni mawazo finyu sana, test tube way of thinking, ina maana kwa kuwa walikuwa na mtu wao hawaruhusiwi kukemea pale nchi inapoyumba? nchi inaangamia na watu kama wewe wako kwenye lindi la usingizi mzito wa chagua la Mungu yaani kikwete

Mwikimbi
Nasema JF si ile ambayo mimi ni mwanacha wake namba maana najua wakatu huo hata 1o hatukufika kama kuna ubishi mkuu Roboti weka data hapa .Yaani mawazo ya ajabu naamini kwamba ukiwa huwezi kuchangia kaa kimya ili tuendelee .JF yangu inashuka hadhi kila siku jamani
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom