Ni kawaida yetu Waafrika tulio wengi, mzazi anapofariki (kama ana miliki biashara), basi na biashara alioiacha nayo itakufa! Dalili zimeshaanza kuonyesha, kuhamishwa kwa Mh. Mwakyembe kwenda wizara nyingine, kutafifisha miradi na sera zake zote.....na pengine kumvunja moyo huyu muheshimiwa!
Ni siku ya pili leo tangia Mh. Mwakyembe awe ameanza kufanya kazi katika Wizara yake Mpya, lakini pia ni siku ya pili leo tangu Treni ya abiria inayofanya shughuli zake za kubeba abiria kati ya Stesheni na Ubungo kutofanya hivyo, tena bila maelezo yeyote kwa wateja wake!
Ukiziona nyuso za abiria wanaosubiri treni hiyo kwa usafri, hakika ni za uzuni mkubwa sana! Na hawana imani tena juu ya ubunifu huu wa Mwakyembe kwa swala la treni, kama utadumu! Mh. Mwakyembe alikuwa mkali sana kuhakikisha huduma hii ya kuwakomboa wananchi wengi wa jiiji la Dar es Salaam na adha ya usafiri inasimama imara, hivyo siamini kabisa kama Mh. Sitta ataweza kufanya the same!
Sisi wapenzi wa soka, tunafananisha kitendo cha kumwamisha Harrison Mwakyembe kutoka Wizara ya Uchukuzi na kwenda Wizara ya Africa Mashariki ni sawa na kumwambia Critiano Ronaldo aache kushambulia na kufunga mabao, na aende golini kudaka kuwa kipa!