Mwakyembe akesha na abiria Tazara

Wabongo watu wa "Hewallah bwana", ukute hili tatizo limeanza siku nyingi safari zinakwua hazina mpangilio safari ya kuondoka leo inaondoka kesho matokeo yake Treni siku moja zitagongana halafu watu watashangaa. Sababu hao jamaa wa TAZARA sidhani kama wana mawasiliano mazuri na vituo vyote, plus wafanyakazi inaonesha hawana moyo kabisa.
 
wapendwa,

hakukuwa na haja ya waziri kwenda kule, usiku na tena akijitangaza kuwa katokea india! kama ni uzembe wa tazara ana muda mzuri tu wa kushughulika nao na sio kwenda 'kufoka stesheni" uongozi wa mtindo wa maghufuli huu, haufai na hauleti tija yoyote zaidi ya cheap polarity.

any way, labda ndio karata zenyewe zinachangwa

mbarikiwe sana

Glory to God!
Ilikuwa ni wajibu wa Waziri kwenda kutatua tatizo la wananchi hata kama ni usiku wa manena. Swala la cheap popularity wakati watanzania wanapata taabu sio mahala pake. Waziri Hongera sana Tunataka viongozi wanaojali na kusilikiza shida za wananchi bila kujali ni muda gani
 
wapendwa,

hakukuwa na haja ya waziri kwenda kule, usiku na tena akijitangaza kuwa katokea india! kama ni uzembe wa tazara ana muda mzuri tu wa kushughulika nao na sio kwenda 'kufoka stesheni" uongozi wa mtindo wa maghufuli huu, haufai na hauleti tija yoyote zaidi ya cheap polarity.

any way, labda ndio karata zenyewe zinachangwa

mbarikiwe sana

Glory to God!


Judith, nakuheshimu sana lakini sikujua kuwa upeo wako wa kufikiri ni mwisho wa pua yako. Sasa kama Waziri kaitwa na wapiga kura wake wanaoteseka muda huo, ulitaka afanye nini? Akatae, halafu kesho yake vyombo vyote vya habari vimtuhumu yeye? Au hasira yako ni kwa kuwa hukupata nafasi ya kukesha naye??? Pole mama, try next time.
 
...... sasa na mimi siku ATCL wakinichelewesha nikimpigia simu saa sita usiku atakuja "kushughulikia" pia?

alikua ametoka India..ina maana alikua airport y Dsm, ambayo akitaka kurudi kwake Kunduchi anaweza pitia TAZARA pale kama uungwana..sioni kama ni popularity move. Anajulikana na kuheshimika tayari, haitaji kwenda TZR kuongea na wananchi wachache awe maarufu zaidi...kuhusu wewe uikwama ukiwa Mwanza, Dar, Kigoma au popote pale anaweza akaja akiwa njiani na maeneo hayo.
 
Abiria wamelipa nauli kwa nini mafuta yasinunuliwe?

Vile kwa Tanesco unakuta watumiaji wa LUKU ni wengi sana lakini etu shirika linakosa mafuta ya kuendeshea mitambo!!!

Hizi LUKU mawakala wanagonga sana hela kuliko hata TAnesco yenyewe....na viwandani hawalipi umeme wao wa mita.
 
Cheap popularity?! Mnafikiri uwaziri ni kulala tu na kutoa maagizo kwa watu wa chini? Ni muhimu kujionea shida wanazopata wananchi ndipo uchukue maamuzi sahihi kwa watu wa chini.
Marehemu Sokoine (rip) alikuwa na kawaida ya kuibuka mahali hata usiku wa manane, bila taarifa, akisikia kuna uozo au utendaji mbovu. Mtu akionyesha uchapakazi mnasema "cheap popularity", mmerogwa!?
 
Mwakembe anatafuta umaarufu kijinga ametumia ugonjwa sasa kahamia kushobokeea stesheni usiku pambaf

kweli wabongo haturidhiki...waziri wasipofanya kazi wanalalamika, wakifanya kazi wanaitwa wanajipendekeza au wanataka umaarufu...yaani nimegundua mtanzania kamwe hutamridhisha..tutabakia kulalamika tu siku zote za maisha yetu
 
Big up mwakyembe. Wachache wanataka kukuchafua Hapa JF , Nadhani wanaufinyu WA mawazo
 
wapendfwa,

kwanza nisahihishe nilipoandika "polarity" nikimaanisha "popularity"

pili, mie kwa kweli angekuwa mbunge wangu, nisingemchagua tena!! manake ameonyesha upeo mdogo sana kwa kazi ya waziri

nisameheni wapendwa, God is Great!

Glory to God!
 
Nachukia sana upumbavu huu!
wahusika wameuchapa usingizi, wewe waziri tena mgonjwa badala ya kwenda kupumzika unatafuta umaarufu usio na maana kabisa.
huo si uwajibikaji, unamnyima mkeo haki yake ya msingi.
kama waziri mzima unakesha station wakati wahusika wakuu wapo ambao ungeweza kuwaamuru muda wowote waje hapo kushughulikia hilo tatizo, akili yako haina akili! CHEAP POPULARITY itawamaliza nyie wakuu.
kuna sababu kweli ya kuwa na viongozi chini yako!?
Chickenshit!
sumu yataka upumzike ili ipotee ktk body yako. Have a plenty of time to relax and recline. Bado tunakuhitaji
Mnalalamika kila siku Jakaya hakai nyumbani kushughulikia matatizo,mfano alioutoa Mwakyembe ni wa kuigwa Jakaya alishasema viongozi wasikae maofisini kusubiri waletewe taarifa wanadanganywa sana hivi leo Mkurugenzi wa Tazara atamdanganya nini Waziri wa Uchukuzi wakati hali halisi alishaiona? Watanzania tusiwe wepesi wa kulaumu tu Hongera Mwakyembe huo ni mwanzo mzuri!
 
Hizo ishu kwa hii serikali yetu imekuwa kawaida sana, Labda Mh. Mwakyembe atabadilisha baadhi ya mambo ktk wizara yake
 
Ms Judith nadhani una chuki binafsi na Mwakyembe. Nimefurahishwa sana na kitendo chake hicho cha uzalendo kwa wateja wake wanaomlipa mshahara kila mwisho wa mwezi hiyo ndio inaitwa accountability Kama hujui.
 
Hata hivyo, Waziri Mwakyembe kabla ya ombi hilo la abiria alikuwa ameahidi kuwa hataondoka eneo hilo hadi treni litakapoondoka.
Halafu ikawaje? Alitatua tatizo?

Bifu yangu kubwa ni dhidi ya hili press bovu bovu la Tanzania, unatoka kama ulivyokuja kabla hujaanza kusoma taarifa, na wala haileweki nani TAZARA aliyesema tatizo ni treni halina mafuta na kwa nini halina mafuta na whether walikimbia kuleta mafuta, na yalitoka wapi hayo mafuta, au treni limelala mpaka sasa???

Badala yake wanajikita kueleza drama za walinzi wa TAZARA walivyokurupushana na Waziri magetini, ludicrous.

Huwezi kutafuta dawa kabla ya kujua ugonjwa, hata muarobaini wa kila ugonjwa wa Babu wa Liliondo ulishindwa.


 
Back
Top Bottom