Mzizi wa Mbuyu
JF-Expert Member
- May 15, 2009
- 7,325
- 6,813
"Hili la Mwakyembe kwamba anaumwa ugonjwa gani, siwezi kuuzungumzia. Mimi nadhani tumwachie aseme mwenyewe na kama si yeye mwenyewe, basi hata madaktari wake wanaweza kusema, lakini serikali hatuwezi kuusemea ugonjwa wake, kwa sababu ni kinyume cha maadili," alisema Waziri Mkuu Pinda.
Aiseee!! ndo hao wabunge walioshutumiwa wanakwepa kuwalipa posho madereva wao na leo tunaambiwa wana fadhili familia za majimbo yao kama vile wapiga kura wao ni omba omba - Matusi hayo!! mambo hajanyooka hayo na hayatanyooka hayo.Pinda alisema wapo wabunge ambao mwisho wa mwezi hawabaki na kitu, kwani fedha zao zote za mishahara zimekatwa kulipia madeni waliyoingia kwa ajili ya kusaidia majimbo yao.
Jamaa ni usalama wa taifa hivyo kila kitu kwake ni siri!
Mimi ni mmoja ya watu wanaoshangaa magazeti na watu wanaoushupalia ugonjwa wa mwakyembe, mtu mwenyewe yupo hapa ila anusubiria ugonjwa wake mwenyewe eti wamsemee wengine, hii haiingii akilini hata kidogo. mbona zitto alisema anachoumwa hata kitandani akiwa hajaweza kuinuka? huyu mwakyembe yy anasubiri nn? au anaona raha magazeti yanavyomwandika kila siku? mawaziri wengine wanaboa sana
Tusubiri kujua ukweli wa mambo?
Yapo maandiko yanayosema watu wangu wanahangaika kwa kukosa maarifa.
Tusubiri kujua ukweli wa mambo?
Ashibae hamjui mwenye njaa. Kama anasema posho za wabunge ni kidogo basi sio mtoto wa mkulima tena.