Mwakyembe aipasua serikali; Pinda amtaka azungumzie hali yake! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakyembe aipasua serikali; Pinda amtaka azungumzie hali yake!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jan 26, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  na Mwandishi wetu - Mwanahalisi

  SERIKALI imetoa msimamo wake kuwa haiko tayari kuzungumzia ugonjwa unaomsumbua Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kwani ni kinyume cha maadili ya utabibu.

  Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari ofisini kwake jana, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisisitiza kuwa hata kama yeye anaujua ugonjwa unaomsumbua, hawezi kuuzungumzia na badala yake mwenye wajibu wa kufanya hivyo ni Dk. Mwakyembe mwenyewe.

  "Hili la Mwakyembe kwamba anaumwa ugonjwa gani, siwezi kuuzungumzia. Mimi nadhani tumwachie aseme mwenyewe na kama si yeye mwenyewe, basi hata madaktari wake wanaweza kusema, lakini serikali hatuwezi kuusemea ugonjwa wake, kwa sababu ni kinyume cha maadili," alisema Waziri Mkuu Pinda.


  Akisisitiza msimamo huo wa serikali, Pinda alisema mengi yamesemwa juu ya ugonjwa unaomsumbua naibu waziri huyo na kwamba wapo waliokwenda mbali kwa kusema amelishwa sumu.


  Lakini wakati Pinda akitoa kauli ya kupinga kuzungumzia ugonjwa wa Dk. Mwakyembe, serikali ilikwisha kuwahi kutoa taarifa ya magonjwa yaliyowasumbua baadhi ya viongozi waliopata kutibiwa nje ya nchi, akiwamo Rais Jakaya Kikwete.


  Kwa muda mrefu Dk. Mwakyembe amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa ajabu ambao hadi sasa umefanywa siri, licha ya madaktari waliomtibu katika Hospitali ya Apollo nchini India kuandika ripoti ndefu inayohusu ugonjwa wake.


  Hali ya naibu waziri huyo inaendelea vizuri licha ya ukweli kwamba amenyonyoka nywele, kope na vinyweleo, huku ngozi yake ikiwa imeharibika kutokana na ugonjwa unaomkabili unaodaiwa umesababishwa na sumu.


  Katika mkutano huo, Pinda alizungumzia mzozo wa posho mpya za wabunge na kuunga mkono kwamba zinapaswa kuongezwa.


  Alisema Rais Jakaya Kikwete amelikabidhi faili la mapendekezo ya posho mpya kwake (Pinda) na kuanzia sasa ndiye mwenye mamlaka ya kusaini au kutosaini.


  Pinda alisema wapo wabunge ambao mwisho wa mwezi hawabaki na kitu, kwani fedha zao zote za mishahara zimekatwa kulipia madeni waliyoingia kwa ajili ya kusaidia majimbo yao.


  "Rais amerejesha lile faili kwangu, kwa hiyo nimepewa mamlaka ya kusaini au kutosaini. Lakini ukweli ni kwamba posho za wabunge ni ndogo na zinapaswa kuongezwa," alisema Waziri Mkuu Pinda.


  Akizungumzia hatima yake kisiasa na wanaonyukana kisiasa kutaka urais, Pinda alisema anashangazwa na makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wanaoukosa usingizi kuutaka urais bila kujua kwamba urais ni mzigo.


  "Mimi nimeshasema sitagombea ubunge, wala urais mwaka 2015, lakini mtu anayehaha kuutaka urais hawezi kuwa na akili nzuri hasa kama kweli anajua Ikulu anakwenda kufanya nini.


  "Wakati Mwalimu Julius Nyerere anang'atuka siku moja tulikwenda nyumbani kwake Msasani.

  Tukiwa tumekaa naye, alikuwa anamtania John Malecela, akamwambia, ‘John, hapa nilipo naona kama kuna kitu kikubwa kimetoka mwilini mwangu, najiona mwepesi sana.'


  "Alipoulizwa kwanini unajisikia hivyo, alisema, ‘Nimeutua mzigo wa urais.' Sasa kama mtu unajua kabisa Ikulu ni mzigo, unawezaje kujitokeza kuutaka mzigo huo?


  "Nimekaa hapa kama waziri mkuu, najua mateso na mzigo wa kuwa waziri mkuu. Najua uzito wa mzigo wa urais unaomkabili Rais Kikwete.

  Wengine wakimwona hivi wanajua anapata raha. Kila mtu anakusema wewe, mara hili, mara lile, yote hayo ni mizigo yako, unawezaje kuutaka urais wakati unajua unakwenda kubeba mzigo mzito?" alihoji Pinda.


  Mbali ya kuzungumzia afya ya Dk. Mwakyembe na kinyang'anyiro cha urais, Pinda alizungumzia maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru, hatua iliyofikiwa katika mchakato wa Katiba mpya, mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam, mwenendo na viashiria muhimu vya uchumi, hali ya chakula, hali ya umeme, upatikanaji wa gesi asilia, sekta ya mifugo, uvuvi, ufugaji nyuki na mambo mengine yanayolihusu taifa.


  Mchakato wa Katiba mpya

  Kuhusu mchakato wa kuelekea kupata Katiba mpya, Waziri Mkuu Pinda alisema baada ya Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2011 kupitishwa na Bunge katika Mkutano wake wa Tano Novemba, 2011 na Rais Kikwete kuuridhia, sheria hiyo ilianza kutumika Desemba mosi mwaka jana.

  Hata hivyo alisema licha ya rais kusaini sheria hiyo, baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wameendelea kukutana naye na kutoa maoni yao kuhusu utekelezaji bora wa sheria hiyo na mabadiliko hayo na huenda yakafanyiwa kazi katika kikao kijacho cha Bunge.


  Katika kuonesha kwamba serikali imepania kuandaa Katiba Mpya, Pinda alisema Wizara ya Katiba na Sheria imeunda kamati ya kiutawala ambayo pamoja na mambo mengine jukumu lake kuu ni kuandaa mazingira ya tume kuanza kazi mara itakapoundwa na wajumbe wake kuteuliwa na Rais Kikwete.


  Aliyataja baadhi ya majukumu ya tume hiyo kuwa ni pamoja na kupendekeza mahali panapofaa kuwa makao makuu ya tume na kutafuta ofisi za tume, kuandaa rasimu ya bajeti ambayo tume itaanzia kazi, kuainisha mahitaji ya vitendea kazi na kufuatilia upatikanaji wake kama magari, samani za ofisi na vifaa vya ofisi.


  Alitaja kazi zinazopaswa kufanywa kuanzia sasa hadi Juni mwaka huu kuwa ni pamoja na uchapishaji wa nakala 2,000 za Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, 2011 kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na tayari nakala 250 za sheria hiyo zimepelekwa Zanzibar kwa ajili ya matumizi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


  Ukuaji wa uchumi

  Katika mwaka 2011, Waziri Mkuu Pinda alisema kuwa kiwango cha ukuaji wa uchumi kilikadiriwa kuwa asilimia 6.0, ikilinganishwa na ukuaji halisi wa asilimia 7.0 mwaka 2010.

  Alisema makadirio hayo yalizingatia kwamba mwaka 2011 umekumbwa na changamoto nyingi, ikiwamo hali mbaya ya ukame iliyojitokeza katika sehemu mbalimbali nchini, pamoja na ukosefu wa nishati ya umeme ya uhakika, ambayo imesababisha kupungua kwa uzalishaji wa bidhaa za viwandani na shughuli nyinginezo zinazohitaji nishati hiyo.


  Kwa mujibu wa Pinda, katika nusu ya kwanza ya mwaka 2011, uchumi wa Tanzania ulikuwa na mwenendo mzuri tofauti na ilivyotarajiwa licha ya kuwapo kwa changamoto ya hali ya hewa isiyoridhisha na upungufu wa umeme.


  "Katika robo ya kwanza ya mwaka 2011 (Januari-Machi 2011), takwimu za awali za ukuaji wa uchumi zinaonesha kuwa ukuaji wa uchumi ulikuwa asilimia 5.8 na katika robo ya pili ya mwaka (Aprili-Juni) uliongezeka na kufikia asilimia 6.7.


  "Aidha, katika kipindi cha robo ya tatu (Julai – Septemba 2011), uchumi ulikua kwa kiwango cha asilimia 6.4. Hivyo, wastani wa ukuaji wa uchumi katika kipindi cha Januari hadi Septemba 2011 ulikuwa asilimia 6.3, kiasi ambacho ni zaidi ya makadirio ya awali ya ukuaji wa asilimia 6.0 kwa mwaka 2011 na pungufu ya kiwango cha ukuaji wa asilimia 7.1 katika kipindi kama hicho mwaka 2010.


  "Viashiria vingi vya kiuchumi kama vile ukusanyaji wa mapato ya ndani, uagizaji nje wa bidhaa za uzalishaji (malighafi), na uuzaji wa bidhaa nje, vilikuwa na mwenendo mzuri katika kipindi hiki cha robo tatu ya mwaka 2011 ukilinganisha na kipindi kama hicho mwaka 2010. Kwa mwenendo huu kuna uwezekano lengo la ukuaji wa asilimia 6.0 kwa mwaka 2011 likafikiwa na hata zaidi," alisema Pinda.


  Pamoja na changamoto hiyo, Waziri Mkuu Pinda alisema wataalamu wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) waliofika nchini mwaka jana kufanya tathmini ya hali ya uchumi wa Tanzania, waliipongeza Tanzania kwa uchumi wake kuendelea kukua kwa kasi inayoridhisha na juhudi zinazofanywa kukabili misukosuko ambayo nchi nyingi katika Bara la Afrika, la Ulaya na hata Marekani nazo zinakumbana nayo.


  Mfumuko wa bei

  Pinda alisema umekuwa ukiongezeka kutoka asilimia 13.0 Julai, 2011 hadi asilimia 16.8 Septemba 2011 na kuendelea kuongezeka hadi kufikia asilimia 19.8 Desemba 2011.

  "Kasi hiyo ya ongezeko la bei imefanya wastani wa mfumuko wa bei wa taifa kwa mwaka 2011 kufikia asilimia 12.7 ikilinganishwa na asilimia 5.5 mwaka 2010. Matatizo ya mfumuko wa bei yamezikumba pia nchi jirani za Afrika Mashariki, ikiwamo Uganda na Kenya, ambazo zimekuwa na mfumuko wa bei wa juu. Mfano, Mwezi Desemba 2011 mfumuko wa bei nchini Uganda ulifikia asilimia 27.0 na Kenya asilimia 18.9, ikilinganishwa na mwezi Novemba 2011 ambapo ulifikia asilimia 29.0 (Uganda) na asilimia 19.7 (Kenya)," alisema.


  Thamani ya shilingi

  Alisema katika kipindi cha hivi karibuni, thamani ya shilingi ya Tanzania ikilinganishwa na dola ya Kimarekani imekuwa na mwenendo wa kupanda na kushuka, kwani ilikuwa sh 1,578 mwishoni mwa mwezi Julai 2011 na kupungua thamani hadi sh 1,609 mwezi Agosti 2011 na hatimaye kuimarika kwa thamani kufikia sh 1,599 mwishoni mwa Desemba 2011.

  Uzalishaji umeme

  Alisema kuwa mwaka 2011 serikali iliweka mkakati mahususi wa kuondokana na tatizo la upungufu wa umeme katika i kipindi cha muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu.

  Alisema katika kipindi cha muda mfupi kuanzia mwishoni mwa Agosti hadi Desemba 2011, serikali iliahidi kupata megawati 300 za umeme wa dharura kutokana na mitambo ya kutumia mafuta mepesi na mazito.


  Alisema hadi kufikia Desemba 2011, TANESCO ilifanikiwa kuzalisha jumla ya MW 270 za umeme kwa kutumia mitambo mbalimbali. Aliitaja mitambo hiyo kiwango chake cha uzalishaji kwenye mabano kuwa ni pamoja na IPTL (MW 80), Symbion Phase I (MW 37), Aggreko (MW 100), Symbion Phase II (MW 50) na kufanya jumla ya megawati 270. Hivyo, serikali ilifanikiwa kutimiza asilimia 90 ya ahadi ya kuzalisha MW 300 na hivyo bado MW 30.


  Aliongeza kuwa kina cha maji katika Bwawa la Mtera kimepanda kutoka kina cha chini cha mita 688.95 juu ya usawa wa bahari kilichofikiwa Desemba 9, 2011 na kufikia kina cha mita 691.02.
   
 2. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Amekula....ameshiba, akistaafu atakuwa anapata posho asilimia 80 ya mshahara wa waziri mkuu atakayekuwepo wakati huo. So he has nothing to loose especially kwenye age yake ya 70+
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Jan 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kwanini Pinda bado anaishi kama Police state? kila kitu ni Usiri siri, ndio Maana nchi yetu ni Masikini na wananchi wengi hatujaendelea

  Miaka 10 Usafiri wa Kigamboni bei haijapanda, lakini bei zingine zimepanda; ukingalia maeneo yote ya kigamboni yameuzwa kwa matajiri si karibuni hao wananchi watapotea na hiyo feri hatutakuwa na wapandaji masikini hiyo ndio janja ya CCM
   
 4. m

  mhondo JF-Expert Member

  #4
  Jan 26, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Sehemu alıyofanyıa kazı kabla ya kuıngıa kwenye sıasa ımemuathırı.
   
 5. manenge

  manenge JF-Expert Member

  #5
  Jan 26, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 280
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ashibae hamjui mwenye njaa. Kama anasema posho za wabunge ni kidogo basi sio mtoto wa mkulima tena.
   
 6. m

  mzalendowaukwel Member

  #6
  Jan 26, 2012
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Pinda wala hana miaka 70+....alishawahi kusema kuwa by 2015 atakuwa na miaka 67+
   
 7. fikrapevu sungura

  fikrapevu sungura Senior Member

  #7
  Jan 26, 2012
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Keshashiba huyu.
   
 8. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #8
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Dr. Mwakyembe anapaswa kulaumiwa kwa unafiki wake! Hilo ni pigo la pili wanamkosakosa! Alipopata pigo la kwanza la ajali, alisema kwamba anamwachia Mungu!!

  Safari hii amepata pigo la pili; wamemchua kwa mafuta ya kinyonga! Yote anamwachia Mungu! Anakaa kimya ili kukinusuru chama chake kinachotaka kumtoa roho! Huyu mtu, si wa kuonea huruma hata kidogo!!

  Angekuwa mwanamapinduzi wa kweli angekwishaweka mambo yote hadharani na kisha kuchukua msimamo na uamuzi wa dhati kuhusu hatima ya maisha yake!! Lakini Kwa mtindo huo wa kinafiki, asubiri tu pigo la tatu; hapo ndipo atakapomwachia Mungu yote kikwelikweli!!
   
 9. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #9
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,330
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  kwanini mnahonga wapiga kura! kwanini mna creat mitandao/makundi ndani ya Chama kimoja. Danganya unyayo wa mguu wako sio macho na fikra zetu upo son of peasant!
   
 10. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #10
  Jan 26, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,939
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Jamaa ni usalama wa taifa hivyo kila kitu kwake ni siri!
   
 11. H

  House1932-1951 Member

  #11
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waziri mkuu naye ni kiongozi wa madeal tu,baada ya kuangaika na mambo ya msingi anajidkia eti kupewa rungu la posho hovyo kabisa.
   
 12. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #12
  Jan 26, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  badala ya kueleza namna ya kutatua matatizo yeye anaeleza na kuorodhesha matatizo...mengi aliyoongea yeye aliyaongea kikwete kwenye salamu za mwaka mpya.......nchi hii haijawahi kuwa na waziri mkuu wa hovyo kama huyu...


  kuhusu mwakyembe zaidi naweza sema unafiki unamponza....
   
 13. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #13
  Jan 26, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  mwakyembe acha kuitega serikali zungumza mwenyewe chanzo cha hali mbaya ya afya yako kama ulivyoambiwa na madaktari kule India. Tiba ina sheria zake serikali haiwezi kuwa msemaji wa afya yako. Pinda yuko sahihi
   
 14. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #14
  Jan 26, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Taito zingine majaribu
   
 15. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #15
  Jan 26, 2012
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Na ukweli ni kuwa madaktari waridhike kwani hali ya uchumi ni mbaya. Onyo kwa madaktari msiende katika maduka wanayonunulia vitu wabunge huko ni ghali! Tafuteni maduka ya hadhi yenu yenye bei ndogo!
   
 16. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #16
  Jan 26, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kukaa kimya kwa mwakyembe kunaonyesha kwamba madaktari kule India walimwambia chanzo cha ugonjwa wake tofauti na kauli za kulishwa sumu na ndio maana anapata kigugumizi kuwaambia watanzania lakini pia kumuokoa Sitta aliyedai kwamba Mwakyembe kalishwa sumu
   
 17. vipik2

  vipik2 JF-Expert Member

  #17
  Jan 26, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,175
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Mgonjwa (Mwakyembe) mbona arishatoa ruhusa kwa serikali kueelezea watanzania ripoti yake aliyoipata toka kwa daktari wake? nini kimeisibu serikali kukataa kuitoa hadharani? kinachoogopwa hasa ninini? au ndio mchawi kuataa kulea mwana kwani akifa msiba atakuwa kausababisha yeye?

  Naye Mwakyembe alikosea sana kwenye ripoti ya Richmond pale aliposema mambo mengine wameyahifadhi kunusuru chama, sasa kinachompata yeye ndio kile kile cha kunusuru chama... RIP Mwakyembe kwani umeingia choo chao cha kike na hutoki!
   
 18. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #18
  Jan 26, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Masaburi yaliyopinda. Hivi tuna viongozi au mavuta bangi tu?
   
 19. mbogoshi ya boganga

  mbogoshi ya boganga Member

  #19
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kabla mikono nyuma,wakati alipopata KILIMO kwanza,Sasa POSHO za wabunge hazitoshi,Kesho MI MUDA WANGU UMEISHA,baada ya kumaliza muda wake NIKIWA WAZIRI MKUU NLISAIDIA SANA, THAT IS HOW TZ POLITCS MOVE
   
 20. tbl

  tbl Senior Member

  #20
  Jan 26, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  "Posho za wabunge ndogo zinatakiwa kuongezwa" risk allowance za madaktari hakuna,.aah nilisahau kumbe nae mbunge heh
   
Loading...