Mwakyembe ageukwa

Kwani ATCL ina ndege ngapi inawafanyakazi wangapi.? Kuna biashara yoyote inayuhusiana na hilo shirika ukiachana na usafirishaji.?
 
hawana jipya dawa nikuwafukuza ili wajue ushenzi wanaoufanya sio wakufumbia macho inaonekana wanafurahia ujinga aliokuwa anaufanya jamaa
 
kilaza bibiyo
 
Taarifa imekaa mkao wa kimbeya mbeya ni ajabu kidogo pamoja na kukaa mkao wa kimbeya bado imevuta wanajamvi kibao.

There are currently 198 users browsing this thread. (50 members and 148 guests)
 
Wakati Paul Chizi anateuliwa kukaimu nafasi ya kaimu CEO wa ATCL niliandika hapa nikipinga namna Waziri alikosea. Lakini sasa nikiri kwamba inawezekana Nundu alijua akifuata taratibu hawezi pata mtu aina ya Paul Chizi. Majizi yaliyojazana serikalini yangemkwamisha kupata mtu sahihi. Jamaa amepiga kazi na kwa uzalendo wa hali ya juu. Nikiri kwamba nilikosea kipindi kile kupinga uteuzi wa Chizi.
 

Zimo kweli au ndo wani jibi! Yaani unajiamini vipi kuuliza swali la kitoto namna hiyo, au tukutajie mpaka namba za mikia za hizo B 737-500s? Acha papapapapaaaaaaa! Yaani hicho kidege kimoja cha kukodi ambacho mmeshindwa hata kubadili namba ya mkia (REG) ndo una ona bonge ya ishu?
 
hao wanaogopa kupunguzwa kazi tu, sababu atcl ina wafanyakazi wengi wakati haizalishi kuweza hata kujiendesha yenyewe, tayari washajua kinachofuata hapo ni kitu gani!

Kweli kabisa mkuu, eti shirika lina wafanyakazi zaidi ya 300 wakati lina ndege moja. Kodi za kwenye mishahara yetu ndo wao wanalipwa mishahara bila kuzalisha. Kibaya zaidi wengi wao wameajiriwa kwa vimemo. Sasa wanahaha kuona jembe (Mwakyembe) limepiga hodi hapo!
 
Redundance ni muhimu sana apo ATCL bse they are too many for nothing tena anza na hao walikugeuka
 
Kimweli wewe ni kama mimi. Aliniudhi sana. Ameweka maslahi mbele yeye na Sita wake. Mara waoneshe misimamo mara walegee
 
Nahisi kua huyu bwana Paul angekua muislamu yani lile picha la muamsho ndio lingezidi utamu kule kwetu kulee
 
Hata ni kufaulisha, kwa nini basi ufanisi unakuwa chini kiasi cha madege kama Qatar Airways, Ethiopian Airline, Kenya Airways, Emirates KLM yasiishie huko sisi tukawa tuko busy kufaulisha abiria na kujijengea nafasi nzuri ya kujitanganza? Kuna vitu ni kukaa chini unaumiza kichwa kidogo hata mwezi haufiki utatoka na kitu cha maana, say a proposal which interlinks our Airline companies with various international flights strategically, watu wakapata ajira na uazoefu. Sasa tumeachia wakenya kila kitu kutuingiza mkenge hata kwenye bunga za wanyama, milima achilia mbali kutuuzia madini yetu kwa bei poa kuliko kwetu.
Utashangaa mjapan ananunua tanzanite nchini Finland kwa bei nzuri kuliko Tanzania.
 
Kuna tatizo moja nimeona ktk posts nyingi,ni uelewa mdogo wa kwanini baadhi yetu tunapinga hatua ya Mwakyembe,na tunaiona ni kurudisha nyuma ATCL. Walioua ATC ni wanasiasa na watendaji serikalini kuanzia wizara mama,wizara ya fedha na Ikulu! Mnaowalaumu wafanyakazi sijui kama mnaelewa matatizo ya shirika letu la ndege!
 
Taarifa imekaa mkao wa kimbeya mbeya ni ajabu kidogo pamoja na kukaa mkao wa kimbeya bado imevuta wanajamvi kibao.

There are currently 198 users browsing this thread. (50 members and 148 guests)
Mkuu Ngongo, linakera hili shirika. Hawadesign ndege wao kazi yao ni kuzitumia kibiashara kwa kutoa huduma kwa watanzania, na bahati mbaya siasa zinaliua.
 

Ungetoka Hong Kong ungejibuje? Hawana ndege ya Taifa laking wana Cathay Pacific.

Mimi naona aibu sana kukumbushwa kuwa tuna shirika la ndege lisilo na ndege hata moja. Ni kioja kikubwa.
 



Ungetoka Hong Kong ungejibuje? Hong Kong hawana ndege ya Taifa laking wana Cathay Pacific.

Mimi naona aibu sana kukumbushwa kuwa tuna shirika la ndege lisilo na ndege hata moja. Ni kioja kikubwa.
 

Mwakyembe sio jembe, mimi nakataaa kabisa mtu aniambie Mwakyembe ni jembe hadi atakapoprove kwa kufanya kitu. Watanzania tumezoea kusikiliza makelele na wapiga makelele tunawaona jembe. Angekuwa Jembe asingefanya haya maamuzi ya kitoto ya kumuondoa CEO na kuweka rubani aongoze shirika. ATC watu wamerithishana matatizo kiasi kwamba ni bora walivunje tuendelee kupanda ndege za wafanyabiashara. Kupunguza wafanyakazi inatakiwa kuwalipa, wazee wa Afrika Mashariki hadi leo hawajalipwa, wamedhulumiwa. Mfumo wetu wa kuweka ndugu anaoendeleza Mweakyembe ndo umesababisha shirika kuwa na wafanyakzi wengi na yeye kaongeza...
 

Mkuu hata kama siyo jembe lakini angalau analeta matumaini ktk kazi yake. Kama mtu ameteuliwa bila kufuata utaratibu ni lazima uteuzi wake ubatilishwe. Haya mambo ya kupeana madaraka kishkaji ndo yanatufikisha hapa tulipo.
Hata hao wafanyakazi lukiki wa ATCL wameajiriwa hivyo hivyo kishkaji kishkaji. CEO akiulizwa anajibu oooho sasa mtu amekuja na kimemo cha mkubwa mi nitamkataliaje! unataka mi ndo nipoteze nafasi yangu! Yaani kifupi ni madudu tupu hapo ATCL. Ni afadhali kuchukua hatua ili kuokoa hilo shiriko. Ni heri hao wafanyakazi wakalipwa haki zao wakatambaa kuliko kuendelea kukaa hapo bila kuzalisha huku wanakulipwa kodi zetu!

Hilo swala la kuweka ndugu litakuja kupungua tu soon, ilivyo sasa ni vigumu mno kulithibiti. Ndo maana kwenye katiba mpya tunataka nafasi kama hizo watu wawe wana-apply based on qualifications and competence. Si kupeana kishkaji namna hiyo!
 
Ugonile kaka Mwakyembe
Nimestushwa sana na uamuzi wako wa kumuondoa CEO Chizi.Pamoja na kuwa inaweza kuwa taratibu za ajira hazikufuatwa vizuri ingekuwa bora kwanza ukaunda Bodi ya ATCL.Hii ndio ingekuwa na jukumu la kupendekeza na kuishauri serikali na hata kuajiri CEO.Sidhani katka kipindi cha muda mfupi utakuwa umeshapata mapungufu ya utendaji kazi wa Chizi.Kwa upande mwingine CEO huyu alishaanza kuonyesha matunda ya kazi yake na ATCL iko hewani .Tuna taarifa kuwa katibu mkuu wako alikwamisha ndege isuruke mpaka waziri mkuu alipoingilia kati.Sasa huyu KM haaminiki machoni kwetu kama hana maslahi binafsi na hivyo kutengeneza mazingira ya kumuondoa Chizi.Kaka naomba uwe makini sana na watu kama Chambo usingizwe mkenge .Basi itisha kikao cha wadau wa mambo ya ndege utapata ushauri mzuri na usitegemee sana ushauri wa hapo wizarani kwani baadhi wanaweza kuwa ndio chanzo cha mashirika haya ya reli na ndege kudidimia.
 
Kama Mwakyembe atadumu na hiyo Wizara hadi 2015 inaweza kuwa kama Bima, NBC au TBS zamani, full wanyakyusa. Huyu Mwakyembe akili kama nduguye Ephraim Kibonde....

Nilishawahi kwenda ofisi za NIC miaka ya 1996 nikakuta wafanyakazi wanagonga kinyakyusa LIVE, wako ukummanya utupak afwileee, utupak akomile muKalifonia Lavu... hapo wanasimuliana kifo cha Tupak
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…