Mwakyembe acha siasa, waache wanasheria wachague rais wao wa TLS

Euphransia

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
937
778
Hakika Nchi hii ina viongozi wa ajabu sana. Kiongozi msomi, mwanasheria badala ya kuwa mfano wa kuigwa kwa kutumia taaluma yake anakuwa kiongozi asiyejua kutumia taaluma badala yake analeta siasa na UCCM kwenye chombo cha kisheria.

Nilitegemea Bw. Mwakyembe angesimamia kuhakikisha wote wanaogombea hawaleti siasa lakini badala yake anataka kumweka mwanaCCM kuwa Kiongozi wa Taasisi hiyo. Bw.Mwakyembe ameonyesha dhahiri kuwa hamtaki Tundu Lissu kuongoza chombo hicho.

Ombi Kwa wanasheria: Chagueni kiongozi atakayewafaa bila kujali itikadi msikubali kuchaguliwa Rais wenu na Bw. Mwakyembe.
 
Mh, inasikitisha kuwa unatishia kuifuta TLS iwapo Tundu Lisu atachaguliwa kuwa Rais wake, Mh, Mwakyembe, you are not final and the Executive is not final either! There is another arm of the government , and that is the Judiciary! This is where justice is dispensed! This will be our final destination!
 
naona kama series mpya imeanza TLS vs Wenye inji.Tutaona mengi
 
Mh, inasikitisha kuwa unatishia kuifuta TLS iwapo Tundu Lisu atachaguliwa kuwa Rais wake, Mh, Mwakyembe, you are not final and the Executive is not final either! There is another arm of the government , and that is the Judiciary! This is where justice is dispensed! This will be our final destination!
Nadhani alisahau kidogo kwamba mheshimiwa lema alipokuwa Patimo alipata muda wa kutosha kufanya maombi kwa ajili ya mihimili yote mitatu na Mungu ameyapokea na keshayafanyia kazi. Mahakama na Bunge wameanza kuelewa majukumu yao sasa
 
Mwakyembe busara zake ni za kuazima lakini kichwani hamnaga kitu. Peke yake hawezi anahitaji wa kumuongoza. Yawezekana hata hayo anayoyakomalia ukimuuliza kesho akasema kuwa alishinikizwa. Ni kama roboti linaloongozwa kwa rimoti. Bendera fuata upepo
 
Mh, inasikitisha kuwa unatishia kuifuta TLS iwapo Tundu Lisu atachaguliwa kuwa Rais wake, Mh, Mwakyembe, you are not final and the Executive is not final either! There is another arm of the government , and that is the Judiciary! This is where justice is dispensed! This will be our final destination!
Well said
 
Mwakyembe busara zake ni za kuazima lakini kichwani hamnaga kitu. Peke yake hawezi anahitaji wa kumuongoza. Yawezekana hata hayo anayoyakomalia ukimuuliza kesho akasema kuwa alishinikizwa. Ni kama roboti linaloongozwa kwa rimoti. Bendera fuata upepo
Jamaa huyu nilikuwa naamini anafaa kuwa PM kumbe nilikuwa nafanya makosa makubwa sana.
 
Mtoa Mada rekebisha kidogo kwenye Heading badala ya MWAKYARE ni MWAKYEMBE.
Hivyo alivyoandika sawa tu, hii yote ni umimi na ubinafsi. Viongozi wetu wengi hawawajali watanzania zaidi ya wao na familia zao wanapokuwa madarakani. Lakini pindi wakiondolewa aaaah, huwezi kuamini kama ndio wale, yaani wanakuwa wakosoaji wakubwa wa serikali.
 
TLS ni taasisi huru isiyopaswa kuingiliwa na Chombo chochote, Sasa waziri mzima anayetumikia wanamchi wote anafuata nini huko? Serikali inaingiliaje taasisi isiyokua ya umma? Hivi waziri huyu hata aibu hana? Anaona ni sawa tu?

Kama anaona kuna watu wanataka kuingiza ajenda zao kwenye taasisi hiyo basi asubiri aone, kama kuna mtu atafanya hivyo basi ndio utakua muda mwafaka kumchukulia hatua za kisheria.Hiki kitendo cha serikali kutaka kuingilia taasisi huru isiyokua ya umma ni aibu na fedheha kubwa sana kwa taifa.

Kuna wafungwa wangapi wanalia kule gerzani kesi zao kupigwa kalenda kila siki?Ofisi ya mwendesha mashtaka ina lawama lukuki, Ni lini ameshughulika na hayo badala ya kuhangaika na uchaguzi wa TLS?
 
Back
Top Bottom