Mwakaleli na maji(rungwe mashriki) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakaleli na maji(rungwe mashriki)

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kinampanda, May 26, 2011.

 1. k

  kinampanda Member

  #1
  May 26, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Awali ya yote napenda kuipongeza serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzani kupitia cha tawala cha kujivua magamba kwa kutuletea mradi wa maji tena mkubwa katika bonde letu la Mwakaleli.

  Pia nitakuwa mchoyo wa fadhira nisipo mshukuru mbunge wetu,madiwani wetu,maafisa watendaji pamoja na wananchi wote wa jimbo letu jinsi walivyoshirikiana na viongozi wao kuratibu na kuuendeleza mradi mkubwa wa mji.

  Kwa wale ambao hawaifahamu mwakaleli au jimbo la Rungwe mashariki linaongozwa na prf.James Marko Mwandosya ambaye pia ni waziri wa maji, hali ya hewa ni mvua nyingi kuanzia mwezi disemba mpaka mwezi wa machi na mei, tuna mito mingi ambayo haikauki (parmanent rivers) ikitoke kwenye safu za milima ya Livingstone na Rungwe, kuanzia mwezi wa sita ni baridi sana.

  Kama kichwa cha habari inavyo jieleza mwakaleli na maji,maji ni kweli ni muhimu sana kwa maisha ya ya binadamu ,wanyama na mimea ,kihistoria mwakaleli hatuna shida ya maji kabisa nadhani wenyeji wa huko mtaniunga mkono.

  Maswali ya kujiuza je mbunge wetu anajua matatizo yanayo wakabiri wananchi wake? kifupi mbunge wetu hajui vipaumbele vya jimbo lake.

  Sasa ninamshauri mheshimiwa mbunge awe na mikutano ya marakwa mara na wannchi, pia ajribu kukaa na vijana ambao ndio taifa la leo, kuliko kila wakati kukutana na wazee maarufu, matajiri wa hapa Mwakaleli, pia jimbo lake limebahatika kuwa na wasomi wengi kuanzia ngazi ya shahada na kuendelea. Namwomba Mh. atambue na atafute takwimu ya wasomi hao ili aweze kupata maoni kwa wasomi hao kuliko kutegemea mawazo ya wazee maarufu na matjiri wa jimboni hapo,

  Ikumbuwe kuwa wakliomuweka madarakani ni wananchi wa jimbo hilo na sio wazee maarufu na matajiri wa hapo ambao ni maskini wa fikra.

  Mh. Rungwe mashariki ni yetu na tuiendeleze kwa kuangalia vipaumbele na sio kukurupuka kama walevimradi wa maji haukufaa uanze bali vifuatavyo vingeanza.

  1. Nyumba za walimu
  2. kujenga hostel za kulala wanafunzi
  3. kuboresha huduma za afya
  4. miundombinu mfano barabara ya tky -katumba
  5. kutoa mikopo kwa wananchi
  6. kuchukua maoni kwa wananchi wote bila kuangalia jinsia na uwezo
  MUNGU IBARIKI TANZANIA , MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI RUNGWE MASHARIKI
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Sasa mkuu badala ya kuwasiliana na mbunge wako unakuja kulalamika humu JF?
   
 3. k

  kajembe JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 756
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Mpe ushauri huo moja kwa moja badala ya kulalamikia hapa JF! sasa tutajadili nini hapo?
   
 4. h

  hans79 JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  mtu hak yake anaona kama kitu cha ajabu,pole kwa kutojua hak zako
   
 5. S

  Songasonga Senior Member

  #5
  May 26, 2011
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huku Mwakalili Hakuna CDM?
   
 6. O

  Ogah JF-Expert Member

  #6
  May 26, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Niliwahi kufika kule kunako-VUNWA gesi..........cha ajabu sana hata barabara ya kwenda huko ni utata.........nikauliza mbunge wa huku ni nani sikuamini nilipoambiwa ni Prof. Mwandosya..........yaani Prof anapita hii barabara MBOVU MBOVU kila wakati na rasilimali zote zile zilizopo kwenye jimbo lake.........
   
Loading...